Mtoa mada umeileta hii hoja ki masihara lakini huo ndio ukweli mtupu, mie nafikiri elimu yetu sio nzuri tena kwa muda mrefu sasa. Mie naishi huku ughaibuni, nilishangaa sana siku moja jamaa rafiki yangu sana ambae nimesoma nae form 1 - 4 ila yeye alikua ana akili sana na tulimuita genius. Yeye yupo bongo na muajiriwa wa shirika kubwa hapo dar la umma. Siku moja kaniletea message ndeeefu eti anaulizia vipi ajiunge na hao Qnet eti anataka aweke kama 2m tshs atapata double ya hio pesa na ushee, na akakazia watu wengi sana ofisini kwao wamepiga pesa kupitia hao jamaa. Nilimuonya tu asithubutu ataliwa vihela vyake hivyo vya akiba vyote.Sijui kama alinisikia ila nilichogundua ambacho na wewe mtoa mada umekiongea Watanzania wengi ni wapumbavu na wanaamini kupata utajiri kupitia short cut...wanasahau kua hakuna Free Lunch popote pale duniani. Na hizi dini na hawa manabii wa uongo akina Masanja ndio janga la kitaifa kabisa. Yaani waseme wafungue mipaka leo ya East Afrika wabongo ndio watakuwa watumwa maana wenzetu Kenya, Uganda, rwanda na wengineo wametuzidi kimaarifa na akili. Wabongo wanaendekeza sana ujinga ujinga na kuamini upumbavu mwingi wa hawa manabii wa uongo.