Pendaelli
JF-Expert Member
- Feb 13, 2014
- 13,075
- 38,625
NA MUITA KRISTO BWANA ATAKAYE NI HUKUMU , ASHUHUDIE KWAMBA KURA YANGU IMETOLEWA KWA YULE AMBAYE KULINGANA NA MUNGU NAAMINI ANA FAA KUCHAGULIWA.
Hayo ni maneno ambayo kila kadnali anayerusiwa kupiga kura ya kumchagua Papa hutamka mbele ya altare akiwa amesimama na karatasi ya kura yake kabla ya kuiweka kwenye chombo kinacho takiwa.
Uchaguzi wa Pope ni wa kipekee usio kuwa na kampeni ambao nyuma yake umetanguliwa na mafungo, maombi, sala na dua kutoka kilaahali panapo husika na kanisa katoliki na kwingineko.
Siku tisa ya za maombolezo pamoja na sala na ibada baada ya kufariki papa zinapokamilika sambamba maandalizi ya uchaguzi wa papa huwa yamekamilika .
Maandali hayo ni pamaja na mikutano kadhaa ya makadnali wakitathimini kanisa na ulimwengu kwa ujumla wake na namna gani papa ajae anavyo weza kukabiliana na hali husika.
Ulimwengu kwa sasa una changamoto mpya mpya nayo ni teknolojia ya akili undwe , vita vya hapa na pale, msukumo wa watu wenye kujihusisha na mpenzi ya jinsia moja kutaka kutambuliwa rasmi na jamii, uhalalisho wa utaji mimba , wahamiaji wanaokimbia vita na majanga mbali mbali, injili mambo leo, marejeo ya Kristo vyote hivi na vingi vingi sana vinahitaji papa ambae atasimama mahali pa kusema hapa ndio na hapa no hapana, papa anae simama na ukweli katika uhalisia wake na si asie fungamana na chochote.
Ulimwengu wa sasa hauitaji mtu anaye simama katikati bali anae simama upande sahihi.
Katika mambo yote sauti ya kanisa huchukuliwa kwa uzito usio wa kawaida ndio maana tinadhibutu kusema anahitajika sasa kiongozi wa kanisa anae sema ndio katoka ndio na hapana katika hapana.
Ni katika muktadha huo kila mwenye mapenzi mema haacho kuwatakia uchaguzi mwema na wenye manufaa makdnali wanapoelekea kumchagua kingozi mkuu wa kanisa kwa dunia upande wa wakatoliki ambao ushwawishi na athari zao kwa ulimwengu ni kubwa kiasi chake.
Naamini haitachukua muda mrefu kumpata papa , nasi kwa unyenyekevu tunawatakia kila la heri