Kila la heri Simba sc leo, Ninaimani zaidi na Yanga kesho inshaallah!

Kila la heri Simba sc leo, Ninaimani zaidi na Yanga kesho inshaallah!

SALOK

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2011
Posts
3,364
Reaction score
2,001
Leo Mnyama Simba a.k.a watukutu wa Kariakoo wanarusha kete yao ya kwanza dhidi ya Club ghali, bora zaidi Afrika Al-ahly ya Misri, ktk mashindano ya klabu bingwa Afrika, ikiwa ni ktk hatua ya robo fainali mzunguko wa kwanza.
Wanaume hao wanatoana jasho leo ktk dimba la Mkapa lililopo Temeke Dar es salaam. Kama Taifa, naiunga mkono Simba sc, ishinde mechi hii. lakini ikitokea wamefungwa sitakuwa sehemu ya huzuni, hapa lazima tuelewane uzalendo ni ktk ushindi tu ama matanga kila mmoja aanue ya kwake!
Kesho Inshaallah, wananchi wataishangaza Dunia, Mamelod sundown watakula si chini ya goli nne, moyo wangu unaniambia kuwa Yanga hii ya Gamond inashinda goli tano, yaani zikipungua ni nne. Maana yake safari ya nusu fainali Yanga anajihakikishia kesho inshaallah, Muda ni hakimu nzuri tusubiri na tuone!
Wananchi dua zote za ushindi kwa Yanga sc.
 
JamiiForums1381953234.jpg
 
Back
Top Bottom