Misri na Ghana ni vinara wa kufika hatua ya Fainali AFCON tangu hii michuano iasisiwe. Lakini Misri ni kinara wa kutwaa ubingwa wa AFCON(mara 7), Ghana ipo nafasi ya 3 kutwaa ubingwa(mara 4).
Misri
Imeshinda taji ×7 (1957, 1959, 1986, 1988, 2006, 2008, 2010)
Imekuwa mshindi wa pili x2.
Kwa hiyo imefika hatua ya fainali mara 9.
Ghana
Imeshinda taji ×4 (1963, 1965, 1978, 1982)
Imekuwa mshindi wa pili x5.
Kwa hiyo imefika fainali mara 9.
Ni miaka 37 imepita tangu Timu ya Taifa ya Ghana(Black Stars) ilipotwaa taji lake la 4(1982), imekuwa ikilisaka taji la 5 bila mafanikio huku ikiwa kinara wa kuwa mshindi wa pili, ambapo mara ya mwisho kuwa mshindi wa pili ilikuwa mwaka 2015 ilipomenyana na Ivory Coast(The Elephants) na Ivory Coast kubeba taji lao la pili chini ya nyota zake(Gerivinho, Solomon Kalou, Yaya Toure).
Sambamba na hapo, Cameroon na Nigeria zinafuatia kufika hatua ya fainali AFCON baada ya Misri na Ghana, zimecheza fainali mara 7.
Cameroon
Imeshinda taji ×5 (1984,1988, 2000, 2002, 2017)
Imekuwa mshindi wa pili x2.
Nigeria
Imeshinda taji ×3 (1980, 1994, 2013)
Imekuwa mshindi wa pili x4.
DR Congo ni timu pekee ambayo haijawahi kupoteza nafasi ya fainali iliyowahi kucheza. Imecheza fainali mara 2(1968, 1974).
Timu zilizowahi kushinda taji mara moja ni Zambia (2012), Tunisia (2004) na Sudan (1970), na pia zimewahi kushika nafasi ya pili mara moja moja.
Timu zilizowahi kufika fainali mara moja na kushinda nafasi hiyo ni Afrika kusini (1996), Algeria (1990), Ethiopia (1962), Morocco (1976), na Congo (1972)
Je Misri ataweza kuendelea kuwa kinara wa mataji ya AFCON? (Ndio ataendelea kuwa kinara).
Je Misri na Ghana wataendelea kuwa vinara wa kufika hatua ya Fainali? Stay tuned!.
Je Ghana ataweza kuongeza taji lake la 5 la AFCON na kuwa katika nafasi ya pili kwa ushindi wa mataji sambamba na Cameroon? Stay tuned!
Je Cameroon na Nigeria wataendelea kuwa vinara namba 2 kufika hatua ya Fainali? Stay tuned!
Je Cameroon ataweza kutetea nafasi yake ya pili ya kutwaa taji la AFCON? Stay tuned!
Je Nigeria itaweza kunyakua taji lake namba 4 na kuwa sawa na Ghana katika nafasi ya 3 kwa ushindi wa mataji ya AFCON? Stay tuned!.
Je Cameroon ataweza kunyakua taji lake 3 la AFCON? Stay tuned!
Je DR Congo itaweza kuongeza taji lake la 3? Stay tuned!
"Avumaye baharini ni papa kumbe na wengine wapo" Tunisia, Afrika kusini, Morocco na Algeria zitafurukuta kusaka na kunyakua mataji yao ya 2 ? Stay tuned!
Taifa Stars je.....