game over
JF-Expert Member
- Jan 1, 2016
- 10,727
- 24,840
Japo watu wengi husema mpira ni dakika 90, au mpira unadunda, lakini kuilinganisha Taifa stars na Senegal, ni ngumu sana kukubaliana na Maneno hayo.
Bahati mbaya sana, mashindano ya mpira sio kama ngumi, ambapo hawawezi kushindanisha bondia wenye uzito tofauti, kitendo cha kushindanisha Senegal ambayo ipo nafasi ya 22 duniani, na Tanzania nafasi ya 131 na kutegemea matokeo tofauti, ni lazima mtu awe na moyo wa mwendawazimu.
Yote kwa yote " Ukikubali kuolewa, pia ukubali kula bila nguo". Kila la kheri Taifa stars, tupo nyuma yenu, lolote litakalotokea, tumeshajiandaa kisaikolojia.
Lakini mkuu, naamini unajua kwenye Soccer ushindi kwa sehemu kubwa Ni Mindsets? Huu uzi wako what was the intention by the way?
Naziamini sana fikra zako komavu, Ila huu uzi naona kama una demoralize na kushusha ari na Morale,
Kuna vitimu vya ajabu huangusha timu kubwa duniani Sembuse senegal hawa waafrica?
Kwani wewe ulitegemea Zimbabwe wakewapa upinzani Egypt mbele ya Mashabiki zao? Au Burundi jana Dhidi ya Nigeria?