Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
Washabiki wa soka wa Ujerumani, wamekuwa na kumbukumbu mbaya za hivi karibuni juu ya madhila ya wachezaji wa Timu hiyo: kuumia, kuachwa ama kupewa kadi uwanjani; hali ambayo imekuwa ikiwaweka kwenye wakati mgumu.
Ilianza mwaka 2002, wakati Mchezaji wao mpya tegemeo, Michael Ballack, alipopewa kadi ya pili ya njano kwenye Semi dhidi ya S. Korea na hivyo kuikosa game la final dhidi ya Brazil, ambayo iliifunga Ujerumani 2-0 kupitia kwa (the original) Ronaldo.
Kuelekea Fainali za SA 2010, Ballack akiwa nahodha na tegemeo aliumizwa vibaya wakati akiichezea Chelsea na hivyo kuzikosa Fainali za South Africa. Bahati mbaya zaidi, Golikipa wao Na. 1 (baada ya Kahn na Lehmann kustaafu), Rene Adler aliumia na hivyo kulazimika kumuita Golikipa underground Manuel Nuer aliyeziba vyema pengo hilo na kudominate nafasi hiyo moja kwa moja. Hata hivyo, Timu ilifika SF na kutolewa na Spain kabla ya kuishinda Uruguay ya Suarez kuchukua Na. 3.
Mwaka 2014, Wunderkid kutoka BvB 04, Marco Reus, aliumia dakika za mwisho na kuzikosa Fainali za Brazil 2014 (aliumia pia Euro 2016). Bahati nzuri, Timu ilitwaa Kombe kwa kuifunga Argentina 1-0 kupitia kwa swahiba wa majeruhi Reus, Mario Gotze.
Mwaka huu umeonyesha kusikitisha zaidi ulimwengu wote wa soka baada ya kuachwa kwa dogo mkali wa Man City, Leroy Sane, pamoja na wengine Mario Gotze (na Sandro Wagner). Kocha Msaidizi Miroslav Klose, alieleza kuwa, madhaifu ya Sane yalitokana na yeye kutocheza kitimu, hivyo Kocha akamteua Julian Brandt wa Bayer 04.
Kuachwa kwa Sane, Gotze na Wagner, kutawahamasisha walioteuliwa kuacha "ego" zao na kucheza kitimu ili kujihakikishia namba hata baada ya Russia 2018 kwa kuwa, Joachim Low, ataendelea kuwa na Timu hiyo mpaka 2022. So, ninatarajia Ujerumani itakuwa ni Compact Team, as always, they have tended to demonstrate.
Updates:
Moderator pliz, Title isomeke: Kila Mashindano ya WC, Wachezaji Muhimu wa Ujerumani huumia: Je, hutolewa kafara ili kuhamasisha Timu?