Kila Mashindano ya WC, Wachezaji muhimu wa Ujerumani: Je, hutolewa kafara ili kuhamasisha Timu?

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
2,869
Reaction score
3,187
Washabiki wa soka wa Ujerumani, wamekuwa na kumbukumbu mbaya za hivi karibuni juu ya madhila ya wachezaji wa Timu hiyo: kuumia, kuachwa ama kupewa kadi uwanjani; hali ambayo imekuwa ikiwaweka kwenye wakati mgumu.
Ilianza mwaka 2002, wakati Mchezaji wao mpya tegemeo, Michael Ballack, alipopewa kadi ya pili ya njano kwenye Semi dhidi ya S. Korea na hivyo kuikosa game la final dhidi ya Brazil, ambayo iliifunga Ujerumani 2-0 kupitia kwa (the original) Ronaldo.
Kuelekea Fainali za SA 2010, Ballack akiwa nahodha na tegemeo aliumizwa vibaya wakati akiichezea Chelsea na hivyo kuzikosa Fainali za South Africa. Bahati mbaya zaidi, Golikipa wao Na. 1 (baada ya Kahn na Lehmann kustaafu), Rene Adler aliumia na hivyo kulazimika kumuita Golikipa underground Manuel Nuer aliyeziba vyema pengo hilo na kudominate nafasi hiyo moja kwa moja. Hata hivyo, Timu ilifika SF na kutolewa na Spain kabla ya kuishinda Uruguay ya Suarez kuchukua Na. 3.
Mwaka 2014, Wunderkid kutoka BvB 04, Marco Reus, aliumia dakika za mwisho na kuzikosa Fainali za Brazil 2014 (aliumia pia Euro 2016). Bahati nzuri, Timu ilitwaa Kombe kwa kuifunga Argentina 1-0 kupitia kwa swahiba wa majeruhi Reus, Mario Gotze.
Mwaka huu umeonyesha kusikitisha zaidi ulimwengu wote wa soka baada ya kuachwa kwa dogo mkali wa Man City, Leroy Sane, pamoja na wengine Mario Gotze (na Sandro Wagner). Kocha Msaidizi Miroslav Klose, alieleza kuwa, madhaifu ya Sane yalitokana na yeye kutocheza kitimu, hivyo Kocha akamteua Julian Brandt wa Bayer 04.
Kuachwa kwa Sane, Gotze na Wagner, kutawahamasisha walioteuliwa kuacha "ego" zao na kucheza kitimu ili kujihakikishia namba hata baada ya Russia 2018 kwa kuwa, Joachim Low, ataendelea kuwa na Timu hiyo mpaka 2022. So, ninatarajia Ujerumani itakuwa ni Compact Team, as always, they have tended to demonstrate.

Updates:
Moderator pliz, Title isomeke: Kila Mashindano ya WC, Wachezaji Muhimu wa Ujerumani huumia: Je, hutolewa kafara ili kuhamasisha Timu?
 
Kuachwa kwa gotze ni sawa kabisa maana kiwango kishashuka sana
Ni kweli, nakubaliana na Wewe kuwa kiwango chase kimeshuka sana. Bila kupepesa macho, Mimi nafurahia sana kuachwa kwake ili kulipiza kisasi cha yeye kuondoka BvB, mwaka 2014 kwenda Bayern na kuiacha Dortmund ikisuasua tangia hapo. Wao ndio wameharibu Bundesliga kwa kukimbilia Timu tajiri kabisa nchini Ujerumani ya Bayern na kuzifanya Timu nyingine za Bundesliga kuwa wasindikizaji.
 
upo sahihi kabisa
 
nenda kwanza jkt ukirudi utajua kuchambua mpira vzr
 
Sane sio messi wala sio ronaldo! Acha kutujazia povu kisa sane...umetafuta pa kupitia ili tu umuongelee sane.

Hahahaa yani sane simkubali kabisa national team, asubiri akuwe kidogo, may be 2022 akafikiriwa na kocha wake 😀😀
 
Ni kweli, nakubaliana na Wewe kuwa kiwango chase kimeshuka sana. Bila kupepesa macho, Mimi nafurahia sana kuachwa kwake ili kulipiza kisasi cha yeye kuondoka BvB, mwaka 2014 kwenda Bayern na kuiacha Dortmund ikisuasua tangia hapo. Wao ndio wameharibu Bundesliga kwa kukimbilia Timu tajiri kabisa nchini Ujerumani ya Bayern na kuzifanya Timu nyingine za Bundesliga kuwa wasindikizaji.
Ni kweli mkuu umeongea point kubwa kabisa.... bundesliga imekuwa haina ushindani tena kama zamani maana wapinzani wote wa bayern wanajiunga nao..... Sasa hummels lewandowski na gotze wote wakahamia bayern mwisho wa siku wameua ligi kabisa
 
Siwezi kuficha hisia zangu kuwa, nawachukia sana wachezaji wote waliokuwa wanacheza Bundesliga waliohamia Bavaria. Mungu anawaona wachezaji hao maana wametunyima furaha sisi manazi wa timu zisizo na majina makubwa Ulaya - Schalke 04 & BvB 04.
 
Nakumbuka kuna msimu mmoja wao alibeba UEFA CUP na mwingine akabeba Champions league ilikuwa 1997 kma sikosei.... Ilikuwa hatari sana enzi hizo wakikutana pale signal iduna park huku koller na amoruso upande wa pili kuna kina Ebbe sand hatari sana....
 
Ni kweli mkuu umeongea point kubwa kabisa.... bundesliga imekuwa haina ushindani tena kama zamani maana wapinzani wote wa bayern wanajiunga nao..... Sasa hummels lewandowski na gotze wote wakahamia bayern mwisho wa siku wameua ligi kabisa
Ni bora wangeenda nje ya Bundesliga, hapo ingekuwa angalao kidogo, japokuwa bado haiondoi hasira ya manazi wa timu zinazoondokewa kuchukia.
Niliwaombea mabaya masuper star wa Dortmund waliokimbia back then 2012 - Nuri Sahin 2011); Lucas Barrios (2012); Shinji Kagawa (2012); Mario Goetze (2013); Robert Lewandowski (2014), Ilkay Gundogan (2016); Mats Hummels (2016); Ousmane Dembele (2017); na Pierre-Emerrick Aubameyang (2018).
Cha ajabu, ni Lewandowski na Hummels (na kidogo Gundogan) pekee waliofanikiwa kwenye Timu zao lakini wengine wameonyesha ku-struggle zaidi ya matarajio yao walipotoka BvB.
Hili ni somo sana, kuwa kutamba Dortmund hakukutokana na ubora wao tu bali mazingira na sapoti ya Jamii ya Ruhr.
Gotze gone, Lewandowski going – but Sahin proves Dortmund stars should think twice before leaving | Goal.com
 
Back
Top Bottom