Kila mauaji hushuhudiwa na macho matano


Hii kesi hapa chini huwa napenda kui-site. Inathibitisha ulichoandika hapa. Jani la mti lilidondoka kwenye cabin ya pick-up ya mtuhumiwa, na hilo ndiyo likawa mwanzo wa taarifa zote

 
Mkuu Mshana Jr kwanini wahangaike vyote hivyo si wangeteua tu kitengo maalum Cha watu wakaenda China ku_Open The Third Eye ingesaidia Sana katika mambo ya upelelezi maana hiyo nasikia mtu anaona na anasimulia tukio Kama alikuwepo vile. VP serikali haijaliona Hilo au haiamini haya mambo? Nazani ingesaidia zaidi
 
Vitengo vyote ni muhimu sana na vingine ni kama backup...BTW kutrain 3rd eye kwa intelligence service ni gharama mno ndio maana wazungu wameamua kufanyya human cloning
 
Mahakamani Kuu Kanda ya Iringa ambayo imefanya kikao mkoani Njombe imemuhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Katekista wa Kanisa katoliki jimbo la Makambako Daniel Philipo Mwelango mwenye umri wa miaka 43 kwa kosa la mauaji baada ya kukutwa na hatia.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Februari 8, 2022 kwa kumuua Daniel Elias Myamba mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa mtaa wa Kahawa Makambako kesi Na MC 74/2022 katika mtaa wa Bwawani mjini Makamabako.

Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Jaji Mhe. Said Kalunde.

Akisoma hukumu hiyo Jaji wa Mahakama kuu Kanda ya Iringa amesema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote kwamba mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo.

Jaji Kalunde amesema siku ya tukio mshitakiwa alifanya maandalizi kwa kuandaa Panga,Chuma pamoja na mifuko minne ya Kinga njaa,mifuko miwili ilikuwa kwa ajili ya kuzuia damu isisambe na miwili mingine kwa ajili kuhifadhi mwili wa marehemu.

Baada ya hapo akampiga na chuma kwenye kisogo baada ya kuona ameanguka chini na kufariki alimkata vipande viwili na kuvipaki katika mifuko ya kinganjaa ili iwe rahisi kubeba mwili huo na kwenda kuutupa mbali,baada ya kuona mke wa marehemu anapiga simu mara kwa mara kwenye simu ya Maherehemu pamoja mwenyekiti wa kigango alishindwa kuubeba mwili huo na kuamua kuondoka huku akiwa amelibeba panga na kwenda kulitumbukiza katika shimo la choo cha shule ya msingi Makambako na chuma alichotumia kumpiga nacho alikificha kwenye gata karibu na duka na yeye kutorokea Dar es Saalam.
 
ASANTE KWA SOMO NAAMINI KAMA BEN SAANANE ALIUAWA IPO SIKU MACHO 5 YALIYOSHUHUDIA YATAONYESHA WAUAJI WAKE

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
mbaya zaidi ukute haina hatia. Inanuka kama ya habili.

Damu ya mtu hunuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…