Kila Mtanzania mwenye uchungu na elimu yetu aandamane Machi 25, 2013

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Posts
1,334
Reaction score
1,466
Jumatatu machi 25, 2013, lazima tuionyeshe serikali ya chama cha mapinduzi kuwa imeshindwa kusimamia elimu yetu na sisi kama wananchi hatuko tayari kuona kizazi cha waliokosa elimu bora kinazalishwa.

Watoto wetu zaidi ya asilimia 90 wamefeli. Elimu inayotolewa madarasani ni mbovu, mitaala mibovu au hakuna kabisa. Hakuna mipango yeyote ya kuimarisha elimu.

Waalimu wamesahauliwa na kuachwa kwenye mazingira magumu na kuwasababisha msongo wa mawazo hivyo kukosa mori na ari ya kufundisha.

Waalimu wanadaharaulika na serikali kuwaona kama hawana kazi muhimu kwenye taifa letu.

Fedha za vitabu zinaliwa na wajanja wachache na hakuna wa kuwajibika.

Madahara ya watoto kufeli yameanza miaka mingi na wengi tayari wako mitaani wakiwa hawana la kufanya.

Tuandamane kwa amani, lazima tujue umuhimu wa kuandamana , serikali zote za kidikteta duniani huongoza kwa nguvu na huwajibishwa kwa nguvu, mazungumzo ya amani kwao ni kama kumsemesha chizi. Kilio cha wananchi kwao ni maji ya kisima hawaoni matatizo yao. Kwao kila mwenye manufaa nao ndio wakwao.

Wananchi wote wenye kuelewa na kuona madhara ya elimu yetu, kina mama na baba ambao watoto wetu wamefeli baada ya kujitoa kwa miaka zaidi 10 ttwendeni barabarani kuonyesha serikali hatukubali kuona na wadogo za hawa hawafeli tena.

Tunao watoto sasa mashuleni, kuanzia darasa la kwanza je tupo tayari kuwaona nao wanafeli???

Jumatatu Nguvu ya umma lazima iongee, sisi ni wengi kuliko majeshi sisi tunasauti kubwa kwani wananchi ndio wamiliki wa nchi yao.

Kila kanda lazima watoke kwa wingi, kila mwananchi lazima aone umuhimu wa kuilazimisha serikali kutoa kipaumbele kwenye elimu.

Tukiwa na mitaala bora na elimu bora, tutakuwa na wataalamu wetu, wabunifu, wajasiriamali wasomi, wagunduzi, nk.

Haya sime tushikamane kwa hili, mpigia baba, mama, dada, binamu nk simu mwambie ukombozi wa elimu yetu upo mikononi mwetu. Bila kujali itikadi, elimu inatuadhiri wote.

Chief Mkwawa
Elimu ni bora kuliko siasa.
 
Mie nina uchungu lkn kuandamana mhhh?!Sidhani ni njia sahihi.Njia sahihi ni kupambana kumuondoa mkoloni anayekalia elimu yetu
 
Ntakuwa wa kwanza,Mungi arusha hapa tupeni utaratibu
 
Waziri akifanya madudu ni jukumu la wazi kabisa awajibike, aondoke madarakani wenye uchungu na uwezo waongoze wizara.

Nani anapenda watoto wetu waendelee kuchomwa moto mitaani na kufunwgwa magerezani kama vibaka?

Nani anapenda mtoto wake awe mchimba mitaro akijuwa fika ameferi kwa uzembe wa serikali?

Jukumu la kudai elimu bora kwa watoto wetu ni la kila mtanzania bila kujali itikadi za vyama vya siasa wala imani zetu.

Watoto wa wanasiasa wanasoma mashule maalum kwa gharama kubwa ambazo masikini hawawezi kuzimudu.

Lazima tuidai elimu bora, na lazima wahusika wa wizara husika watoke madarakani, hii sera ya kulindana imeanza kitambo lazima tuitokomeze. Tunahitaji uwajikaji sio kulindana tunajifedhehesha na tunalifedhehesha Taifa la tanzania kwa kukumbatia viongozi dhaifu na wazembe.
 
Mh hamuogopi kung'olewa meno ,kunyofolewa kucha na kutobolewa macho? manake ndo issue siku hizi.
 
Issue ni kufeli, ambapo na yeyd Mbowe yupo kwenye kundi la waliozunguka round about.


Sielewi tatizo liko wapi?

Unaongelea asilimia ngapi ya kuferi watoto? na unalinganisha kwa takwimu gani unafanya urgument kwa misingi gani hasa?

Tunaongelea Taifa kupata zaidi ya 90% failure hili ndilo tatizo, kuferi kwa mbowe kulikuwa asilimia ngapi?
 

So mlitaka hiyo asilimia 90 waziri ndio awafaulishe? Sababu ya wanafunzi kufeli si ubovu wa sera ya elimu pekee. Zipo sababu nyingi sana, lakini kwa sababu Chadema hamu yao ni kuingia madarakani wanaikuza sera ya ubovu wa elimu kama ndio sababu kuu, na kwa vile watu kama wewe mnashabikia kila kinachosemwa na viongozi wa Chadema, basi hamuangalii sababu zingine na kuhisi kwamba maandamano ndio yatawafanya wanafunzi wafaulu.
 

mkuu mbona wewe mwenyewe unaonekana kama ulifeli?? maana hata kuandika neno feli hujajua hadi leo hii, hebu angalia neno argument wewe umeandika vipi? Rudi darasani maandamano hayatakusaidia
 

Unazifahamu sababu zilizopelekea watu kudai maandamano?

sababu kubwa ni moja, pale inapoonekana waziri anapwaya na kufanya vibaya anatakiwa either awajibike kwa kuwapisha wengine au awaqjibishwe kwa kutolewa madaraka na bosi wake.

Kwasababu viongozi wanalindana na kulipoteza taifa na kuliangamiza ndiyo sababu ya huu mgogoro, nakama viongozi watajenga utamaduni wa kujiuzuru hususani kawambwa na mulugo pasingekuwa na shinikizo wala maadamano maana wangelitendea haki taifa wametufedhehesha na kutuabisha kama taifa.

Sidhani kama unaelewa 90% inamaanisha nini kama ungelewa usingethubutu kuinuwa kichwa chako kutetea upuuzi huu.

Turudi nyuma Kuferi kwa mbowe ni asilimia ngapi na nini significance effect yake ukilinganisha na 90% tunayoijadili hapa? maana umemuingiza mbowe kwa ushabiki na ujinga tu bila kuelewa tunajadili nini.
 
Kweli maandamano sasa yanatumika vibaya, mimi nadhani tungeanza kuandamana kuwalaumu wazee wanaowarubuni wanafunzi, tungerudisha maadili kwa vijana wetu kwenda na kuhudhuria vipindi badala ya kuwaona kwenye fukwe za bahari na maeneo ya starehe wakati wa vipindi, tungewakanya kuachana na muda mwingi kwenye mitandao kwa mambo ya kipuuzi na badala yake wautumie kusoma. wanafunzi, wazazi na jamii ni chanzo cha kufeli kwa wanafunzi ila serikali ni mbuzi wa kafara tu. hebu jiulize wewe kama mzazi au mwanajamii umetoa mchango gani kwa wanafunzi pale ulipoona wakifanya mambo kinyume na maadili. Isije kuwa mkaota vigimbi kwa kuandamana na bado tatizo likaendelea.
 
Wakati Mbowe anapata zero pia sera ya elimu ilikuwa mbovu?

matanzania mlivyo majinga,watu wanataka kuwasaidia kuondoa matatizo kwenye elimu hafu mnauliza maswali ya kipumbavu! Hv wewe kama baba yako ni masikini akitaka kukuambia mikakati ya kutafta hela,utamuuliza kwa nn asitumie hyo mikakati! Hamna adabu na wavivu wa kufikiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…