Kila Mtanzania mwenye uchungu na elimu yetu aandamane Machi 25, 2013

Kila Mtanzania mwenye uchungu na elimu yetu aandamane Machi 25, 2013

mkuu mbona wewe mwenyewe unaonekana kama ulifeli?? maana hata kuandika neno feli hujajua hadi leo hii, hebu angalia neno argument wewe umeandika vipi? Rudi darasani maandamano hayatakusaidia

Huu ndo upofu na ukiziwi wa wakuu wenu wa serikali, badala ya kuangalia maudhui ya taarifa au maoni unaangalia spelling na matamshi kama ndivyo wamasai na wengi wengineo amabao matamshi kwa asili wengi hayaendi sawia na kiswahili au hiyo english, usingeelewana nao. Huu ni ukilaza tena wa hali ya juu. Unaonesha huna cha kujadili bali mzembe flani vile.

wale wazungu wako wanakuja pale UDsm kutoka Germany au Portugal na English fyongo huwa wamefeli eti? na hawana elimu? unaakili za ovyo kama kawambwa. nini hujaelewa?
 
Sielewi tatizo liko wapi?

Unaongelea asilimia ngapi ya kuferi watoto? na unalinganisha kwa takwimu gani unafanya urgument kwa misingi gani hasa?

Tunaongelea Taifa kupata zaidi ya 90% failure hili ndilo tatizo, kuferi kwa mbowe kulikuwa asilimia ngapi?

we hujamuelewa. mie nimemsoma sana. kila mzazi anajijua kwa nini mtoto wake amefeli. na kila aliyefeli anajijua kuwa kwa nini amefeli. si issue ya kukaa na kuilaumu serikali
 
Safi sana Wamogori nimeipenda sana comment yako..fateni hii na sio kurumbana jamani humu tuna elimishana na sio kutupiana maneno.
 
Jumatatu machi 25, 2013,
lazima tuionyeshe serikali ya chama cha mapinduzi kuwa imeshindwa
kusimamia elimu yetu na sisi kama wananchi hatuko tayari kuona kizazi
cha waliokosa elimu bora kinazalishwa.

Watoto wetu zaidi ya asilimia 90 wamefeli. Elimu inayotolewa madarasani
ni mbovu, mitaala mibovu au hakuna kabisa. Hakuna mipango yeyote ya
kuimarisha elimu.

Waalimu wamesahauliwa na kuachwa kwenye mazingira magumu na
kuwasababisha msongo wa mawazo hivyo kukosa mori na ari ya kufundisha.

Waalimu wanadaharaulika na serikali kuwaona kama hawana kazi muhimu
kwenye taifa letu.

Fedha za vitabu zinaliwa na wajanja wachache na hakuna wa kuwajibika.

Madahara ya watoto kufeli yameanza miaka mingi na wengi tayari wako
mitaani wakiwa hawana la kufanya.

Tuandamane kwa amani, lazima tujue umuhimu wa kuandamana , serikali zote
za kidikteta duniani huongoza kwa nguvu na huwajibishwa kwa nguvu,
mazungumzo ya amani kwao ni kama kumsemesha chizi. Kilio cha wananchi
kwao ni maji ya kisima hawaoni matatizo yao. Kwao kila mwenye manufaa
nao ndio wakwao.

Wananchi wote wenye kuelewa na kuona madhara ya elimu yetu, kina mama na
baba ambao watoto wetu wamefeli baada ya kujitoa kwa miaka zaidi 10
ttwendeni barabarani kuonyesha serikali hatukubali kuona na wadogo za
hawa hawafeli tena.

Tunao watoto sasa mashuleni, kuanzia darasa la kwanza je tupo tayari
kuwaona nao wanafeli???

Jumatatu Nguvu ya umma lazima iongee, sisi ni wengi kuliko majeshi sisi
tunasauti kubwa kwani wananchi ndio wamiliki wa nchi yao.

Kila kanda lazima watoke kwa wingi, kila mwananchi lazima aone umuhimu
wa kuilazimisha serikali kutoa kipaumbele kwenye elimu.

Tukiwa na mitaala bora na elimu bora, tutakuwa na wataalamu wetu,
wabunifu, wajasiriamali wasomi, wagunduzi, nk.

Haya sime tushikamane kwa hili, mpigia baba, mama, dada, binamu nk simu
mwambie ukombozi wa elimu yetu upo mikononi mwetu. Bila kujali itikadi,
elimu inatuadhiri wote.

Chief Mkwawa
Elimu ni bora kuliko siasa.

mkuu na sisi tuliofeli kutokana na upumbavu wetu wa kuchora akina zombi na messi tuandamane?
 
Kweli maandamano sasa yanatumika vibaya, mimi nadhani tungeanza kuandamana kuwalaumu wazee wanaowarubuni wanafunzi, tungerudisha maadili kwa vijana wetu kwenda na kuhudhuria vipindi badala ya kuwaona kwenye fukwe za bahari na maeneo ya starehe wakati wa vipindi, tungewakanya kuachana na muda mwingi kwenye mitandao kwa mambo ya kipuuzi na badala yake wautumie kusoma. wanafunzi, wazazi na jamii ni chanzo cha kufeli kwa wanafunzi ila serikali ni mbuzi wa kafara tu. hebu jiulize wewe kama mzazi au mwanajamii umetoa mchango gani kwa wanafunzi pale ulipoona wakifanya mambo kinyume na maadili. Isije kuwa mkaota vigimbi kwa kuandamana na bado tatizo likaendelea.

Kiongozi

1. Hizi internet na mitandao, masimu nk vipo tanzania pekee kenya hakuna? kama kenya pia vipo tuambie kwanini hakuna 90% failure huko kwa wakenya?

2. Wakenya walizua mgogoro kati ya walimu na serikali kuhusu maslahi bora kwa walimu na serikali ilikaa na walimu wakatatua. Je serikali yako ya Tanzania imekaa na kutatua madai ya walimu kuhusu kuboresha maslahi yao? kama hapana unadhani walimu wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi? kama hapana kwanini watoto wasifeli?

Ni hayo tu kiongozi.
 
mkuu na sisi tuliofeli kutokana na upumbavu wetu wa kuchora akina zombi na messi tuandamane?

Ndiyo unatakiwa kuandama tena uwe mstari wa mbele.

Sababu ni kwamba usipofanya hivyo wadogo zako, ndugu zako, jirani zako na baadaye watoto wakuzaa wewe mwenyewe watafeli endapo hatutashinikiza mabadiliko ya sera ya elimu na uwajibikaji ili kuwandallia wanao mazingira mazuri wasijefedheheka kama wewe.
 
Mie nina uchungu lkn kuandamana mhhh?!Sidhani ni njia sahihi.Njia sahihi ni kupambana kumuondoa mkoloni anayekalia elimu yetu

me nadhani walioandaa maandamano hawakuwa na muda wa kujipanga na kuona ni nini na wapi tusimamie.kuna swali dogo tu mtu mwenye busara atajiuliza,tunaandamana waziri ajiuzulu,je akijiuzulu ndio wanafunzi watafaulu?jamani ni bora muda huu tunaotumia kuhamasisha fujo tungeutumia kutoa elimu kwa jamii itambue kuwa chanzo cha matatizo yote haya ni mifumo mibovu ya serikali ya ccm so solution ni kuiondoa madarakani.maandamano na fujo za kipuuzi vitawafanya wenye busara zao kuamini propaganda mbovu kuwa cdm ni chama cha vurugu na wanaharakati wasiokuwa na sifa ya kuongoza dola.
 
we hujamuelewa. mie nimemsoma sana. kila mzazi anajijua kwa nini mtoto wake amefeli. na kila aliyefeli anajijua kuwa kwa nini amefeli. si issue ya kukaa na kuilaumu serikali

Unafahamu kwanini elimu ni lazima kuliko chochote kile katika uhai wa mwanadamu?

Unafahamu kwanini Nyerere alibinafsisha mashule ya taasisi za dini?

Unafahamu ili taifa lisonge mbele linahitaji nini? na kwanini?

Unazifaha haki za msingi ambazo serikali lazima itekeleze kwa raia wake? unaweza kuzitaja?

Kama tutaendela na 70%.......kufelisha watoto madaktari, wahandisi wananga nk watatoka wapi? china eti?

Watanzania suala la elimu ni nyeti halihitaji majibu laini laini maana mwisho wa siku tutaliangamiza Taifa letu.
 
Wakati Mbowe anapata zero pia sera ya elimu ilikuwa mbovu?


wakati ni sasa. Ya mbowe hayatuhusu, ya kipindi icho ilikuwa ni kwa kizazi husika. Hiki ni kizazi kingne mkuu.

Kufeli kwa mbowe hakujustfy failure ya wizara na wasimamizi wake kwa wakati huu mkuu.
 
Sielewi tatizo liko wapi?

Unaongelea asilimia ngapi ya kuferi watoto? na unalinganisha kwa takwimu gani unafanya urgument kwa misingi gani hasa?

Tunaongelea Taifa kupata zaidi ya 90% failure hili ndilo tatizo, kuferi kwa mbowe kulikuwa asilimia ngapi?


jamaa anataka kututoa kwenye mada. Analeta ushabiki
 
kama kawaida yao wameshatangaza kuwa maandamano hayaruhusiwi.
Hata kama watazuia maandamano, ila wajue mwakani watafeli kwa 80% endapo wataendelea kutoa sababu za kufeli za ajabu kama walizotoa juzi.
  • 2010 waliofeli ilikuwa 20% (Tume iliundwa na majibu yalitolewa)
  • 2011 waliofeli ilikuwa 40%
  • 2012 waliofeli ilikuwa 60%

Kulikuwa na haja ya kuwa na Tume tena.

Kwa aliyeona madodoso ya tume ya Pinda, anajua kuwa serikali haijadhamiria kutatua tatizo la wanafunzi kufanya vibaya kwa sababu madodoso yale yanalazimisha mtu akubaliane na sababu walizonazo wao na si sababu anazohisi mtu.

Kwan upungufu wa vitabu umeanza leo?Tangu zamani tatizo la vitabu lilikuwepo ila walimu ndio waliokuwa na moyo wa kufundisha na ndio waliotufanya tufanye vizuri.
 
Issue ni kufeli, ambapo na yeyd Mbowe yupo kwenye kundi la waliozunguka round about.

Hata ukieleweshwa mpaka mtondogoo hutaelewa maana umejiandaa kupinga tu. Pole maandamano 25th march
 
So mlitaka hiyo asilimia 90 waziri ndio awafaulishe? Sababu ya wanafunzi kufeli si ubovu wa sera ya elimu pekee. Zipo sababu nyingi sana, lakini kwa sababu Chadema hamu yao ni kuingia madarakani wanaikuza sera ya ubovu wa elimu kama ndio sababu kuu, na kwa vile watu kama wewe mnashabikia kila kinachosemwa na viongozi wa Chadema, basi hamuangalii sababu zingine na kuhisi kwamba maandamano ndio yatawafanya wanafunzi wafaulu.



mkuu km huhusiki kuandamana, tuachie tunaohusika. Story zako peleka lumumba
 
NIPO MBEYA.
NITAKUWA MSTARI WA MBELE.
Hatuwezi kuwaruhusu wachina wawekeze, wakati tunazarisha mamburura mashuleni.
TUKOSE HATA KIBARUA CHA KUCHANGANYA KOKOTO?
Tutaandamana.
 
Yap ni zaidi ya zero. Naona mwenzangu ni chini ya zero.

Mimi nawashangaa wanajibizana na wewe kwa sababu hata username yako inajionyesha jinsi ulivyo.Wenzangu wa Iringa wanajua MABOSO ni nini?
 
Back
Top Bottom