Kila Mtanzania mwenye uchungu na elimu yetu aandamane Machi 25, 2013

Kila Mtanzania mwenye uchungu na elimu yetu aandamane Machi 25, 2013

Walimu walikataliwa na serikali kuboreshewa mishahara na kupewa posho za mazingira magumu sikusikia watu wakihamasisha maandamano kuishinikiza serikali isikie kilio cha walimu. Sasa mambo yameharibika ndo tunahamasishwa tuandamane. Mmmm, tunakumbuka shuka wakati kumeshakucha! Kujiuzulu kwa waziri hakutatatua mlolongo wa mapungufu yaliyopo katika mfumo wa elimu Tanzania.
 
Jumatatu machi 25, 2013, lazima tuionyeshe serikali ya chama cha mapinduzi kuwa imeshindwa kusimamia elimu yetu na sisi kama wananchi hatuko tayari kuona kizazi cha waliokosa elimu bora kinazalishwa.

Watoto wetu zaidi ya asilimia 90 wamefeli. Elimu inayotolewa madarasani ni mbovu, mitaala mibovu au hakuna kabisa. Hakuna mipango yeyote ya kuimarisha elimu.

Waalimu wamesahauliwa na kuachwa kwenye mazingira magumu na kuwasababisha msongo wa mawazo hivyo kukosa mori na ari ya kufundisha.

Waalimu wanadaharaulika na serikali kuwaona kama hawana kazi muhimu kwenye taifa letu.

Fedha za vitabu zinaliwa na wajanja wachache na hakuna wa kuwajibika.

Madahara ya watoto kufeli yameanza miaka mingi na wengi tayari wako mitaani wakiwa hawana la kufanya.

Tuandamane kwa amani, lazima tujue umuhimu wa kuandamana , serikali zote za kidikteta duniani huongoza kwa nguvu na huwajibishwa kwa nguvu, mazungumzo ya amani kwao ni kama kumsemesha chizi. Kilio cha wananchi kwao ni maji ya kisima hawaoni matatizo yao. Kwao kila mwenye manufaa nao ndio wakwao.

Wananchi wote wenye kuelewa na kuona madhara ya elimu yetu, kina mama na baba ambao watoto wetu wamefeli baada ya kujitoa kwa miaka zaidi 10 ttwendeni barabarani kuonyesha serikali hatukubali kuona na wadogo za hawa hawafeli tena.

Tunao watoto sasa mashuleni, kuanzia darasa la kwanza je tupo tayari kuwaona nao wanafeli???

Jumatatu Nguvu ya umma lazima iongee, sisi ni wengi kuliko majeshi sisi tunasauti kubwa kwani wananchi ndio wamiliki wa nchi yao.

Kila kanda lazima watoke kwa wingi, kila mwananchi lazima aone umuhimu wa kuilazimisha serikali kutoa kipaumbele kwenye elimu.

Tukiwa na mitaala bora na elimu bora, tutakuwa na wataalamu wetu, wabunifu, wajasiriamali wasomi, wagunduzi, nk.

Haya sime tushikamane kwa hili, mpigia baba, mama, dada, binamu nk simu mwambie ukombozi wa elimu yetu upo mikononi mwetu. Bila kujali itikadi, elimu inatuadhiri wote.

Chief Mkwawa
Elimu ni bora kuliko siasa.

itakuwa vyema coz ile tume iliyoundwa na pinda ilishatoa ripoti na hakuna jipya yote waliyoeleza yaliyoelezwa yalikuwa yanajulikana
 
Matusi, jaziba na gazabu wakati wote inasemekana ndiyo silaha pekee anayoitumia asiye na hoja na haswa mwovu. sishauri kuandamana haswa kwa mambo ya kitaaluma!!! na mbaya zaidi tungali tunanajua wanasiasa (wabunge) ni chanzo cha hapa yulipofika!!!! posho, mishahara mikubwa, vyote vipo kwao lakini kwa walimu hakuna kitu.
 
Kiongozi wa maandamano shule ilimshinda,yeye angesoma kwanza halafu akafanya haya.

Ndo maana anataka mtoto wa dada yako apate elimu iliyo bora.
Jikomboe hakuna mtu mwingine atakayekukomboa ktk zama hizi za digitali! Ukoloni wa ki-akili au kifikra hautakuacha salama kama utawaza kwa viwango vya TANU na Afro Shiraz.
Tafakari.
 
Asiye jua maana haambiwi maana. Swali la msingi ni hili? Kwa nini mhe.Mbatia aligoma kujiunga na tume ya kuchunguza hayo hayo matokeo? Ni kweli watoto ni digitali bt nadhani na serikali ina mchago wake ktk hili. Maandamano sawa lakini yawe na tamko kwa serikli
 
Pamoja na porojo zote za kwenye mitandao; napenda kuwakumbusha ya kuwa maadamano ya kuisimamisha nchi yatafanyika kesho kutwa Jumatatu tarehe 25/03/2013, hivyo ni vyema endapo wote tutajitokeza katika maeneo yetu kuunga mkono maandamano haya kwa mstakabali wa elimu yetu na kwa vizazi vijavyo, na siyo kujificha nyuma ya key board zenu huku mkiendeleza porojo zisizo kuwa na msaada wowote katika kutatua tatizo la elimu nchini.
 
Matusi, jaziba na gazabu wakati wote inasemekana ndiyo silaha pekee anayoitumia asiye na hoja na haswa mwovu. sishauri kuandamana haswa kwa mambo ya kitaaluma!!! na mbaya zaidi tungali tunanajua wanasiasa (wabunge) ni chanzo cha hapa yulipofika!!!! posho, mishahara mikubwa, vyote vipo kwao lakini kwa walimu hakuna kitu.

so una ushauri gani wenye kuweza kufikisha hisia zetu na kusikilizwa mkuu??
 
Tunataka uwajibikaji hapa isiletwe siasa!magamba watambue tanzania tuipendayo! Ile ya wasomi! Heti waziri anadiriki kukalia wadhifa wakati wadogo zetu matokeo si mazuri! Uganda na kenya zaidi ya 90% wamefaulu! Tanzania giza tupu! Hacheni kupalilia matumbo yenu wakati watoto wetu ata elimu wanakosa!
 
Mie nina uchungu lkn kuandamana mhhh?!Sidhani ni njia sahihi.Njia sahihi ni kupambana kumuondoa mkoloni anayekalia elimu yetu

Zion Daughter, njia pekee ya kumuondoa mkoloni anayekalia elimu yetu ni haya maandamano. Mimi sio mwanachama wa CDM lakini naunga mkono juhudi na harakati hizi. Viongozi wa nchi wangeheshimu tu kilio chetu watanzania juu ya anguko la elimu na kuwawajibisha viongozi husika. Kusingekuwa na sababu ya maandamano. Lakini inaonyesha kabisa kuwa kuna nia ya kimakusudi katika uongozi wa nchi yetu ya kutotaka kutatua tatizo la elimu Tanzania. Hivyo maandamano ya amani ndiyo njia pekee ya kidemokrasia kuionyesha hisia na uchungu tulio nao watanzania. Kama jeshi la polisi litafanya kazi yake ya kutulinda hakutakuwa na vurugu yeyote. Lakini wakifanya kazi kwa kufuata maagizo ya viongozi waovu wasio na uchungu na taifa letu basi wao ndiyo watakuwa chanzo cha vurugu na sio waandamaji.
 
Kuandamana ni njia mojawapo ya wananchi kuonyesha ghadhabu zao dhidi ya serikali...lakini suala la kushindwa mitihani kwa wasomi wetu si jambo la kulala na kuamka....ni jambo lilosabishwa na mambo ambayo yalikuwa bayana kwa kila macho....wengi walipiga kelele lakini wakapuuzwa kana kwamba matokeo yalikuwa yakisubiriwa ili tuandamane.......tuandamane tukajadiliane namna ya kuboresha elimu yetu???...mbona watoto wa wanasiasa wetu hawasomi shule zetu hizi??? wengine hata mitihani ya baraza hawafanyi....wanatumia mitaala ya uingereza......hata serikali nzima ikijiuzulu kesho ndiyo tutakuwa tumetatua tatizo letu??? ...tusifanye tatizo hili la kufeli wasomi wetu kama mtaji wa kisiasa....tukae wote kwa pamoja .....tuondoe ubaguzi wa elimu.....tuongeze bajeti katika elimu kwa kuondoa matumizi ya anasa kwa wanasiasa wetu tuyahamishie kwenye elimu....tatizo hili la elimu halitatuliwi katika majukwaa ya kisiasa.....na si tatizo la kisiasa....tutaendelea kulumbana huku watoto wetu wakiendelea kushindwa kafaulu.....au watoto wetu watapata daraja la I huku wakiwa hawajui kusoma na kuandika.....tusifanyie siasa elimu ya vijana wetu....
 
nyie andamanen tuu ila akifa mtu tusisikie makelele, kwan hakuna njia nyingine za kupresent hzo idea zenu? Kuna data zipo zinaonyesha sahv uwezo wa waalim umeshuka sana tena waalim hawa wanaoajiriwa kwa wingi hv karbun ni kajanjaaa
 
Malaya walinisomesha na walijua majukumu yao katika kuniwezesha kupata elimu bora.

Huna lolote na usomi wako hausaidii chochote katika nchi hii, bora hata ambao hawakusoma,
Anyway - kama huyo mnaemwita hakusoma anawapeni shida mpaka hamlali na ma degree yenu ya kupeana jee angesoma ingekuwaje? Na jee wananchi wanapaswa kumpa nani credit. Wewe unayejisifu kusoma wakati hauna input ktk taifa au yule hakusoma lakini ana input ??
Na kama kila mtu akija na vyeti vyake hapa wewe chako utaficha wapi.
 
input yake ni kumiliki danguro
 
Kuna tofauti kubwa kati ya mtu aliyesoma na aliyeelimika. Wewe mwenzangu naona suala kuelimika kwako ni zero.
 
Back
Top Bottom