Kila mtu alitishwa na mwendazake, Mbowe usijifanye hujui hili

Kila mtu alitishwa na mwendazake, Mbowe usijifanye hujui hili

Ingekuwa enzi zake yaliyofukunyuliwa na CAG tusinge yasikia,yangesikika kipindi kile hakuna adhabu ambayo angepewa CAG zaidi ya kupelekwa msitu wa mabwepande.
 
Hakuna wa kumlaumu maana kwa yule mzee ungejaribu kumpinga usingebaki salama, waulize wa kina Kinana na Makamba kilichowakuta ilibidi na waufyate na wao waje kuimba mapambio ya kumsifu tu
Hakuna baiskeli yaweza kuendeshwa kwa pedal zote mbili kuwa upande mmoja, moja iwapo juu nyingine huwa chini, nyingine iwapo mbele zazima nyingine iwe nyuma ndiyo kanuni ya mwendo
 
Magu hakuwa na kawaida ya kumuogopa mtu ata kipindi cha kampeni hakuwa mtu wa kuogopa, nakumbuka 2015 akiwa kwenye kampeni aliwah sema kuwa "kuna tajiri kajenga sehemu ambayo inatakiwa lipite bomba la maji huko kimara, alafu wenzie wote wameondoka ila yeye kaenda Mahakamani, Mahakama haitaki kuamua inapiga karenda! Sasa subiri niwe Rais!" Huyu ndo alikuwa Magu
Hiyo tabia imelicost taifa, na imemcost yeye binafsi.
 
Mwendazake alinyenyekea-nyenyekea kipindi cha uteuzi pale na kampeni baada ya kukalia kiti hamkuheshimu mtu, hadi wanaCCM nao wakapigwa na butwaa wakajiuliza eh huyu ndio yule yule, Viongozi wakuu waastaafu wa nchi hawakuheshimiwa, Viongozi wenzake wa serikali, bunge na mahakama nao walibaki kusema ndio mzee, alishauri washauri wake ikitokea umetoa maoni tofauti basi cha moto utakiona, kila mtu aliweka mikono nyuma na kuinamisha kichwa chini, sasa utawalaumu CCM hapo, utawalaumu Viongozi wastaafu hapo, utawalaum washauri wake hapo, utawalaumu viongozi waandamizi hapo.

Hakuna wa kumlaumu maana kwa yule mzee ungejaribu kumpinga usingebaki salama, waulize wa kina Kinana na Makamba kilichowakuta ilibidi na waufyate na wao waje kuimba mapambio ya kumsifu tu.

Kwa hiyo Mr Mbowe utalaumu watu bure wakati wewe mwenyewe unajua aliyekuwa ameshika rungu alikuwa yukoje.

MY TAKE: BINADAMU ACHA KUPENDA SIFA, SIFA ZOTE PELEKA KWA MUNGU, NA HATA UKIPATA CHEO CHA KUONGOZA DUNIA HESHIMU MAWAZO YA WENZIO, UTAISHI VIZURI SANA MAISHA YAKO YOTE ILA USIJIFANYE WEWE MWAMBA, MWAMBA NI MUNGU TU.
Asante mleta hoja. Tofauti yako na Mbowe ni moja, nayo ni yeye (Mbowe) kathubutu kusimama hadharani mchana kweupe katusemea. Tofauti nyingine ni Wana CCM wengine kwanza walijiona raia daraja la kwanza na kuwaumiza sana, kuwatesa sana, kuwaita wakala wa mabeberu, kuwateka na hata kuwaua wa-Tanzania waliokuwa na mtazamo tofauti na mwendazake. Nionavyo mimi, tutajivunia sana vyeo, misuli, na hata mali tulizonazo kwa sababu hatujui anayetumiliki wote na aliyetuleta tukazaliwa mahali hapa. Tutambue kuwa kila moja wetu ana haki zote za kuishi alipozaliwa kutoka kwa MUNGU Muumba wetu sote, na siyo kwa Binadamu hata angekuwa na cheo cha aina gani. Ndiyo sababu, hatima yetu iko kwake (MUNGU), Rais mwenye fedha, maskini ataondoka hapa duniani bila mchango wa hali yake (Cheo, utajiri, umaskini...). Tenda wema kwa watu wote bila kubagua kwa sababu wote unaowaona ni watoto wa BABA yetu (MUNGU).
Nakushukuru sana kwa hitimisho lako. Mwenyezi Mungu atangulizwe MOYONI na siyo mdomoni
 
Hivi we mke wa Mbowe una hakika Mbowe aliumizwa kuliko mtu yeyote kwa ushahidi upi?


Au Mbowe ana kipi Cha kuumizwa kuliko mtu yeyote?

Au hiyo kukkosa wabunge?.


MSIMCHAFUE MH.MBOWE
Nawe mjane wa mwendazake kwanini upinge?
 
Shetani huyu alinyang'anya fedha hadi wana CCM wenzie.

Mfano MoDewji

Ali Mafuruki alikufa baada ya kufanyiwa kama Mbowe.

IMG_20210411_210541_348.JPG
 
Back
Top Bottom