Kila mtu aliyekusudia kumjua Mungu na mambo yake kwa dhati, Mungu humfanyia hiki...

Kila mtu aliyekusudia kumjua Mungu na mambo yake kwa dhati, Mungu humfanyia hiki...

Joined
Jun 30, 2023
Posts
11
Reaction score
38
Atafanya juu chini kuhakikisha hiyo nia yako njema inatimia. Watu wengi wanateseka kwa sababu wameingia katika nyumba za sala lakini hawako siriasi na Mungu kama anavyotarajia. Hivyo wengi wameachwa wajiendee wanavyotaka.

Mifano ya watu waliokuwa na usiriasi na Mungu hata kama hawana uhakika naye, Mungu hakuwaacha..

1: Mzungu Kornelio, alitoa sadaka na sala lakini hakumjua vizr Mungu. Mungu alifanya mazingira ya kumkutanisha na mtume petro. Jamaa na familia yake wakasaidiwa.

2: Muafrika Towasi tajiri, alikuwa anakomaa kusoma gombo la isaya ila aelewi. Hiyo bidii yake ilimfanya Mungu amchukue kimuujiza shemasi Filipo kutoka Samaria hadi gaza amtangizie njiani huyo muethiopia ili amsaidie kujua neno. Na akabatizwa.

3: Mwanamke asiye myahudi Ruth alipokana miungu yake na kujiapiza kuambatana na Mungu wa Israel. Mungu alifanya connection hadi huyo binti mjane akaolewa na boazi, na akawa bibi kizaa bibi wa bibi wa bibia yake Yesu wa Nazareti.

4: Kahaba Rahabu, alipoonyesha kuwa na imani na Mungu wa Israel kuliko waru wote Yeriko, Mungu alimfanyia mazingira hadi akajiunga na waisrael wakati nchi yake yote inaangamizwa. Hata waisrael walipomtenga na kumbagua Mungu alimtumia kiongozi wao mkubwa Yoshua kumchukua na kumrudisha tena kambini. Na leo Rahabu ni moja ya mzazi wa wazazi waliopelekea Yusuph Baba yake Yesu kuzaliwa.

Fundisho:
Ukiona watu wanafanya usanii katika majumba ya sala, waache, usiinge. Ukiamua kumtafuta na kumfuata Mungu kwelikweli atakutengenezea mazingira hadi dhamira yako njema itimie bila kujali wanaokuzunguka wamepinda au la.
 
Back
Top Bottom