Kila mtu awajibike badala kisingizio cha simba inapendelewa kuwa kichaka cha kuficha wanaofeli majukumu yao

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
HATUWEZI kuwa na timu ambayo zinapendelewa halafu tukafanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa. Kama tutakuwa na ligi yenye kiwango sahihi, basi tuna kila sababu ya kuwa na timu imara.

Kama Ligi Kuu Bara ina timu 20, tunaamini kumekuwa na ushindani mkubwa katika mechi nyingi hasa zile zinazoonyeshwa kwenye runinga ya Azam TV ambayo tunapaswa kuipongeza kwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye mpira wa Tanzania baada ya mechi nyingi kuanza kurushwa moja kwa moja.

Umesikia watu wengi ambao ni wadau wa karibu kama wachezaji, makocha na kadhalika wamekuwa wakisema kuwa mechi nyingi zinazoonyeshwa moja kwa moja huwa hazina upendeleo.

Wanasema mechi nyingi zisizoonyeshwa, timu wenyeji wamekuwa wakipewa upendeleo wa wazi kuhakikisha wanabeba pointi za nyumbani maana yake si kwa uwezo wa mpira, jambo ambalo ni bayana linaudumaza mpira wa Tanzania ambao tunaupigania kukua.

Ili soka likue, lazima liwe na haki na nafasi kwa watu kuchezeshwa kwa haki, haki itawale na kutengeneza uimara unaotokana na ushindani sahihi kabisa.

Nimeamua kuandika makala haya baada ya kuona kuna kampeni ya chinichini ambayo haina faida kwa mpira wa Tanzania na inaonekana tumekuwa tunaoneana haya kwa kisingizio cha fulani shabiki wa timu fulani.

Kampeni za kusema Simba inapendelewa, Simba imekuwa ikipewa nafasi ya kushinda na kadhalika. Lakini wanaosema wamekuwa hawana uthibitisho wa zaidi ya asilimia 90 wa wanayoyasema.

Kinachoshangaza ni kuona na watu wengine ambao hawajaribu kutafakari yanayozungumzwa, wanayachukua na wao kuyazungumza kutoka kwa waliyoyasikia bila sababu au hoja sahihi.

Simba inapendelewa katika mechi ipi, kama imefunga mabao halali, vipi inapendelewa. Kuna bao ilipendelewa, jibu hapana, ila ilichezeshwa saa 8 badala ya saa 10 kama ilivyoelezwa. Kwani aliyecheza naye alicheza saa ngapi, naye alicheza muda huo pia. Sasa kupendelewa kunatokana na nini hasa?

Sote tunajua, Simba ndio wana timu bora kabisa katika Ligi Kuu Bara kwa msimu huu na hili linadhihirishwa na takwimu zao kwa maana ya wastani lakini hata hatua waliyofikia kimataifa na kuitangaza Simba mbali barani Afrika.

Pamoja na hivyo, unaona Simba iliyoifunga Al Ahly, AS Vita, JS Saoura na kutoka sare na TP Mazembe, imekwenda kufungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar ambayo inapambana kuepuka kuteremka daraja katika Ligi Kuu Bara!

Hapo unaweza kujiuliza, kwamba kama ni hivyo, Simba inayopendelewa inafungwa vipi na Kagera Sugar, inahenyeshwa vipi na KMC lakini kabla ya hapo tuliiona ikipata shida kubwa dhidi ya Coastal Union pale Tanga.

Wanaofanya kampeni za kutengeneza lawama ni kampeni chafu na za kipuuzi, kampeni zinazoonyesha wameshindwa kufanya kazi zao na baada ya hapo wanasambaza maneno yatakayowalinda siku wakianza kuhojiwa kutokana na kufeli majukumu waliyokabidhiwa.

Kwa wale mnaosikia, vipi uamini vitu tofauti na ambavyo unaviona. Mtu hadi akuaminishe tofauti wakati na wewe uliona kabisa kila kitu kilivyo, vipi mtu mwingine akuaminishe tofauti na wewe uamini.

Wanaosambaza kile kisicho sahihi, vizuri kuwahoji kwa hoja badala ya kukubali kubeba wanachokisema hata kama ni pumba na kukisambaza pia.

Hatuwezi kuwa tayari kuona timu moja, mfano Simba inapendelewa halafu tukakaa kimya. Lakini kama si hivyo, basi mimi sitakaa kimya ili suala la mechi zinazochezwa tujadili mambo ya msingi na si haya ya kubabaisha kutokana na kuwapinga wanaobabaisha mambo.

Pia haitakuwa sahihi kuwasikia Simba sasa nao wakisema Yanga wanapendelewa baada ya ndani ya mechi tatu, kupoteza na kushinda moja wakati matarajio ilikuwa ni kushinda zote.

Tuache mpira uchezwe na kama kuna malalamiko yawe ya msingi badala ya kusambaza upuuzi.
 
Kuondolewa kwa Kambuzi na wapuuzi wenzie kwenye orodha ya marefa kumekupa picha gani?
 
Hili la marefa kuindolewa kuchezesha ligi kuu ndo linafanyika kwa mara kwa mara ya kwanza? Na je wamesemwa kwamba wameondolewa kwa sababu wameipendelea Simba? Yanga imefunfishwa tabia ya hovyo kabisa na Zahera, kulalamika badala ya kuipush timu yao ifanye vizuri. Kwa namna hii ni kama wameshakubali kishindwa na sasa wanajiliwaza kwa kushindwa kwao!
 
mkuu acha kujivua nguo mechi ya kagera ziliongezwa dk 5 ila refa kapeleka hadi dk 98 sijui alikuwa anataka nini? (nahisi ni droo),mechi ya kmc ndo aibu kuu imejionesha anzia penati ya 2 rudi ile back pass unagundua kabisa kuna mazingira yanatengenezwa

kuliko kuwachoshwa wachezaji na timu kupoteza hela za maandalizi ni vyema wakatoa ushindi wanapoona imewapendeza
 
Hili la marefa kuindolewa kuchezesha ligi kuu ndo linafanyika kwa mara kwa mara ya kwanza? Na je wamesemwa kwamba wameondolewa kwa sababu wameipendelea Simba? Yanga imefunfishwa tabia ya hovyo kabisa na Zahera, kulalamika badala ya kuipush timu yao ifanye vizuri. Kwa namna hii ni kama wameshakubali kishindwa na sasa wanajiliwaza kwa kushindwa kwao!
Hujaona barua ya TFF inasema dhahiri walishindwa " kuhimili" mchezo wa KMC vs Simba
 
Kuna miaka yanga walikuwa wanafanya vzr ligi kuu hata kuchukua ubingwa mfulilizo ingawa hawakuweza kufanya vzr kimataifa japo walikuwa na slogan yao ya...wakimataifa...nakumbuka miaka hio malalamiko haya haya kuwa yanga walikuwa wanapendelewa mara wananunua mechi mara wanahonga marefa n.k yaliibuka sana. Nikikumbuka hivyo nawaza kimoyomoyo kama ndio hulka ya wabongo au kila timu inatesa kwa zamu? Hebu jaribu kuwaza alafu ukiona unateseka ujue ni kwa zamu.
 
Hivi nani alisema Refa alipuliza filimbi ya offside baada ya ile video.??mlijuaje kama ni offside??Mimi niliona beki wa Simba alipiga mpira ukambambatiza forward wa KMC mkononi ndio refa akapiga filimbi.Wekeni video
wale marefa wameondolewa kuchezeshwa kwa ajili ya nini?
 
Back
Top Bottom