Fumadilu Kalimanzila
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 1,770
- 5,423
Kwa muda mrefu nimekuwa nikijua kuwa dalili mojawapo ya Taifa masikini ni kuwa na wakulima wengi!
Tanzania ina wakulima kati ya 65% hadi 80% katika population ya watu milioni 60, hivyo hili ni Taifa masikini sana!
Marekani yenye watu zaidi ya milioni 300 ina wakulima wasiozidi asilimia 10%.
Kitu ambacho nimekigundua na ndo msingi wa mada yangu ni kwamba kiashiria kingine cha Umasikini wa Taifa ni pale kila mtu anapotaka kuwa mwanasiasa.
Leo katika Taifa letu kila mtu anataka kuwa mwanasiasa kuanzia matapeli, waganga wa kienyeji, wafanyabiashara,wasomi hadi maprofesa, vila.za na wengine wengi ambao hawana hata sifa za uongozi.
Ukichunguza kwa makini hata quality ya mijadala katika Bunge letu inadhihirisha kuwa wengi walioko Bungeni wako kimaslahi binafsi zaidi.
Hoja hazijengwi tena katika namna bora ya kupata majawabu ya changamoto mbalimbali za wananchi bali ni kuangalia mtoa hoja ni nani na zaidi afanyiwe " character assassination " basi!
( Rejea idadi ya waliojitokeza katika kura za maoni za CCM 2020 kuomba kuteuliwa kuwa wagombea ubunge katika majimbo mbalimbali).
Kinachowasukuma wengi ni maslahi ya kibunge ambayo hayazidi "in totality" milioni 15 kwa mwezi sawa na kama dola za marekani $6,452 kwa mwezi au dola za marekani $ 215 kwa siku ( Exchange rate: USDTZS = 2325).
Mtu mwenye hadhi ya Uprofesa kukimbilia mapato ya dola za marekani $ 215 kwa siku ni uwezo mdogo wa kufikiri na kwa mtazamo wangu watu wa model hiyo hawawezi kulikomboa Taifa hili!
Kingine ni kwamba maeneo mengine ya uzalishaji kama vile kilimo ,biashara yamevurugwa na watu hawa wenye maarifa na upeo mdogo lakini wapenda uongozi.
Unakuta Mkuu wa Mkoa anasema publicly kuwa hawezi kufuata sheria na taratibu katika manunuzi ya Serikali na anaagiza mtaalamu wa manunuzi akae pembeni mpaka ujenzi utakapokamilika.Sasa sijui nani atajibu hoja za ukaguzi pale ubadhirifu utakaponyika.
Mbunge wa Mtama Mhe.Nape Nnauye anapata wasiwasi na deni la Taifa na anataka ukaguzi tujue kiasi tulichokopa na kama zimeenda zote katika miradi iliyokusudiwa lakini Waziri wa Fedha Dr.Mwigulu Nchemba anatoa majibu kama vile deni la Taifa atalilipa yeye na familia yake!
Wabunge wengine wametoa macho kumzodoa mtoa hoja na kumhusisha na mambo ya ajabu ajabu kama vile chuki kwa uongozi wa awamu ya tano chini ya Rais Magufuli n.k.
Wabunge hawa watashtuka pale Serikali itakapowambia hakuna pesa za kulipa mishahara na marupurupu yao au wapunguziwe.
Ni dhahiri tuko hoi bin taabani kama Taifa, kama tunakusanya kwa mwezi 1.5 trillion na Bilioni 800 zinakwenda kila mwezi ku- service mikopo na tunabakiwa na bilioni 700 na ukitoa wage bill ( mishahara ya watumushi) kama bilioni 600 tunabakiwa na bilioni 100!!!!
Sisi ni masikini wa kutupwa! Taifa kubwa lenye rasilimali nyingi lakini halina uongozi wenye vision!
Umasikini wetu umejidhihirisha kwenye tu hela hutu Rais Samia amekopa kutoka IMF kukabili athari za COVID-19,kila kiongozi "amepagawa" ,huyu anasema hili ,huyu anasema lile!
Kama Taifa tunahitaji kuwa serious na kutafuta viongozi serious wenye maarifa wanaoweza kutukwamua hapa tulipo na si blah blah hizi!