Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
Yawezekana unakonda na kukosa raha huku ukifikiria hivi kweli fulani ndio kanifanyia hivi? Jibu ni ndio huyo ni yeye halisi na wala hawamzingizii bali huo ndio uhalisia wake.
Kosa lipo kwako kumuamini zaidi ya anavyostahili kuaminika, Ulimuamini zaidi ya jinsi alivyo ndio maana kafanya vile alivyo mbele ya uwezo wake kuaminika umebaki kushangaa.
Duniani huwezi kuishi bila kuamini mtu ila unaweza kuweka mipaka katika kuwaamini watu yaani kila mtu mpe mipaka yake na hili utaliweza kupitia uzoefu na jinsi unavyomsoma kila rafiki yako.
Usiamini kuwa hawezi kukusaliti hapo utakuwa umejitafutia kesi ya mauaji kwa sababu siku ukimfumania kama sio kujiua wewe basi utamuua yeye au vyote kwa pamoja na hilo ni sababu ulimuamini kiasi kwamba hukuona kama anaweza kukusaliti , ulimuamini zaidi ya uwezo wake kuaminika.
Kuna mtu unaweza kumuacha ndani kwako na ukakuta kila kitu ni salama ila kuna mwingine kosa tu kumuacha kuna mapungufu utayakuta ndani maana yake huyo umemuamini zaidi ya anavyostahili kuaminika ilitakiwa umuamini ila mpaka wake uwe usiruhusu abaki ndani mwenyewe.
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako