GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kama umezaliwa kijijini kwenu, ukakulia kijijini kwenu, ukasomea kijijini kwenu, na shughuli zako zote ukazifanyia kijijini kwenu, ni rahisi kuamini kuwa mila na desturi zenu ndizo bora kuliko zingine zote. Lakini wakati huo huo, kwa watu wa tamaduni zingine, wanaweza wakawa wanawashangaa jinsi mlivyo na utamaduni wa ajabu.
Na, kwa muktadha wa Uzi huu, utamaduni wako si lazima uwe na asili ya kabila lako, bali utamaduni wo wote ule ulioukubali na kuwa sehemu ya maisha yako.
Kuna mila zingine, kwa mfano, ambazo wakati wahusika wakijitahidi kuzikumbatia, watu wa nje na huo utamaduni wanawaonea huruma kwa kuwaona kuwa wanateseka. Mfano, ukeketaji kwa wanawake, kutahiri vijana wa kiume bila ganzi, n.k.
Ikitokea mtu amesoma, na kubaini kuwa baadhi ya mila zao ni "mbaya" na hivyo kuamua kuachana nazo, wenzake wa Jamii yake humhesabu kuwa kapotoka huku yeye akiwa na kuwa ni wajinga.
Tamaduni huwafanya watu waliozikubali kuwa watu wa wake.
Na, kila mtu ni mtumwa wa utamaduni aliouridhia.