Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Katika miaka ya hivi karibuni watanzania walio wengi wanaonekana kuelemea upande wa sanaa katika kila kitu.Sanaa ipendwayo zaidi siyo ile ya uchongaji vinyago na uchoraji vibonzo ,La ! bali ni kuimba na kucheza muziki na kubwatuka kwenye maigizo. Fedha nyingi za masikini na matajiri zinaishia huko.Na muda mwingi wa kufanya kazi unatumika kuangalia mambo hayo.
Hata mimi nilwahi kutumia senti zangu za kwendea shule niingie kwenye ukumbi kumuona Hemedi Maneti.Hata shule siku hiyo ya mwanzo wa muhula sikufika. Nilichokiona kikifanyika kule ndani mpaka leo naijutia siku ile.Na mpaka leo nikiangalia mabadiliko ya kisanii Tanzania na wasanii wenyewe sijapata jawabu. Je, Tanzania imeendelea au imerudi nyuma. Na je huko mbele ni furaha au ni balaa.