Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania, moja kwa moja niende kwenye mada,
Inshort nimekuwa ni mtu wa kusafiri safiri kikazi, hivyo nimebahatika kuzitembelea baadhi ya nchi za Africa zisizopungua kumi, safari ya mwisho nimekaa Nairobi mwezi mmoja, then nikarudi nyumbani kama siku tatu zimepita sasa.
Cha ajabu na kustaabisha nimekuwa nikiota nimekaa na Raisi wa Kenya anaemaliza muda wake pamoja na huyu mwingine anaeingia Ikulu, tukipiga story mtu tatu na kukumbatiana kwa vicheko, na kizuri zaidi wananimpa mpaka technique walizotumia kumumaliza kabisa Baba yule aliyeenda mahakamani kupinga matokea.
Baada ya hapo tunapiga selfie na picha za kutosha then tunaagana kila mtu anaelekea upande wake, nikishtuka nakuta nipo kitandani tu nimelala, hii imetokea mara ya pili leo. Kwa wenye kujua, hii ndoto inamaanisha nini?
Turudi nyuma kidogo, Mwaka 2020 mwezi wa tano kulikua na event pale dodoma ya chama kikubwa tu cha wafanyakazi, alikuwepo hayati (Raisi) aliyetangulia mbele za haki na PM wa sasa, pia na viongozi wengi ne wengi wa serikali wakati huo mkuu wa wilaya akiwa ni huyu Naibu Waziri wa wizara fulani.
Baada ya event ile nilikumbwa na ndoto mfuatano za kukutana na kuzungumza na bwana yule (hayati) mambo nyeti yanayoihusu nchi, huku tukifurahi pamoja na kupeana hugs za hapa na pale, na si ndoto ya mara moja, mpaka bwana yule alipotangulia mbele za haki, na ilibidi nifike msibani kwa kua nilihisi kuna msukumo ndani yangu wa kufanya hivyo.
Na nimekuwa nikisumbuka na ndoto nyingine nyingi za kukutana na kuzungumza na viongozi wakubwa wakati in reality si kweli.
Naombeni tafadhali mwenye kujua tafsiri ya ndoto hizi anisaidie, nashindwa kuelewa maana yake, nimebaki kuwaza tu hiki ni nini na kwanini watu potential tu?
mkuu
Ibun Sirin msaada tutani