Kila nikianza mazoezi ya viungo baada ya wiki mbili au tatu naacha, nikijitahidi mwezi mmoja baadaye naacha

Nenda kacheze mchezo unaoupenda Mara kadhaa kwa wk. Michezo ni mizuri sababu huoni Kama unafanya mazoezi ukiwa unacheza
 
Sesten Zakazaka natumai na weye ni mzoefu wa hiki kitu.

Msaidie mleta uzi kama unalifahamu hili sababu na mie niko ka yeye nikifanya wiki basi nishapata uvivu naacha.

Karibu. [emoji12] [emoji12]
Mazoezi ni tabia au utamaduni, kama utamaduni huo haikujijenga kwako kua mfanya mazoezi wa mara kwa mara ni rahisi sana kuingia uvivu kila unapoanza, inabidi ujilazimishe sana na ikiwezekana jaribu kua unafanya mazoezi na kikundi ambacho mtakua mnahamasishana, ila mazoezi ni muhimu HASA KWA WANAUME, umenielewa Hajar?
 
Hahahaaaa. Nimecheka Best.

Mie naona jioni ndio poa kutokana na mihangaiko ya kutwa nzima ambayo inataka ianzwe asubuhi.

Pia Ahsante kwa kunikimbia best baada ya kupokea kichapo. [emoji12] [emoji12]
Hahaahh.. Sijakukimbia bhn soka ndo lilivyo jamaa waliupiga mwingi sana ila bahati haikuwa yao. Now nmehamia paris kwa mkopo[emoji3][emoji3]

Kuhusu mazoezi mie pia napendaga jioni
Kudamka Asubuhi ni kazi aisee[emoji3][emoji3]
 
Hahahaaa. Nimekuelewa sana Sesten.

Haya wacha wachukue ushauri wako nadhani utawafaa hasaaaa. Maana ka mie nlishashindwa hayo mazowezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…