star health talks
Member
- Apr 28, 2017
- 30
- 73
Kila nikienda hospitali naambiwa nina Infection, Infection ni nini? na kwanini kila mara naambiwa nina infection?
Ili kuelewa maana ya Infection na kwanini mara kwa mara unaambiwa una Infection ukienda hospitali, ni muhimu kwanza kufahamu japo kidogo jinsi mwili wa mwanadamu unavyofanya kazi.
Kwa kawaida mwili wa binadamu una seli kinga nyeupe kitaalam zinaitwa ‘white blood cells’, ambazo hizi kazi yake ya msingi ni kuulinda mwili dhidi ya magonjwa mbali mbali.
Kuna seli kinga nyeupe ( white blood cells) aina mbali mbali. Mfano wa aina hizo za seli kinga nyeupe ni Lympocytes, neutrophils, monocytes, basophils, esinophils. Kila aina ya seli kinga nyeupe iliyotajwa hapo juu inahusika na kupambana na aina fulani tu ya vijidudu ili vijidudu hao wasishambulie mwili. Kwa mfano seli kinga nyeupe aina ya neutrophils inahusika na kuukinga mwili dhidi ya maambukizi ya bacteria, lymphocytes inahusika na kuukinga mwili dhidi ya maambukizi na virusi, esinophils dhidi ya minyoo nakadhalika.
Endapo mtu atashambuliwa au kupata maambukizi ya vijidudu basi seli hizi hutumwa kwa wingi mwilini na kwenye mfumo wa damu kwa ajili ya kupambana na hivi vijidudu. Mfano mtu akipata maambukizi ya bacteria seli kinga zitaongezeka kwa kiasi kikubwa sana hasa seli kinga aina ya neutrophils, kama itakuwa virusi basi seli kinga aina ya lymphocytes zitaongezeka zaidi.
Mtu akipata maambukizi ya vijidudu aidha iwe virusi au bacteria mwili huonesha dalili mbali mbali ikiwemo joto kupanda, kunyongonyea, kukosa nguvu naka dhalika.
Ukienda kituo cha kutolea huduma za afya utapimwa vipimo vingi ikiwemo Full blood picture au complete blood count. Tutazumgumzia Full blood picture/complete blood count ni nini siku nyingine. Ila mojawapo ya kazi ya hiki kipimo ni kuonesha wingi wa hizi seli kinga mwilini,
ikitokea kipimo kinaonesha seli kinga zimeomgezeka iwe neutrophils( bacteria) lymphocytes (virusi) basi mtoa huduma wa afya atakwambia una infection kwenye damu akimaanisha umepata maambukizi ya virusi au bacteria kwa muda huo, kama ni bacteria utapewa antibiotis, kama ni virusi mara nyingi vinaponaga vyenyewe so utapewa dawa za kutuliza maumivu( supportive treatment) ingawa kuna baadhi ya nyakati unaweza kupewa dawa za kuua virusi (antivirals).
Kutokana na mtoa huduma kutokuwa na either muda wa kutosha kukuelezea kwa undani ugonjwa wako au mtoa huduma kutokuwa na uelewa wa kutosha wa hiki nlichokieleza hapo juu atakwambia una infection tu.
Na tunaposema infection sio vitu vya ajabu, haya yanaweza kuwa magonjwa kama UTI, typhoid, n.k
Kwanini kila siku nikipima naambiwa nina infection napewa dawa natumia siku nyingine nikienda tena naambiwa nina infection tena.
Kama nilivyosema awali hapo juu, haya ni maambikizi ya virusi au bacteria ambayo ukipewa dawa unapona na umaweza ukapata tena baada ya muda.
Kwanini zamani huu ugonjwa haukuwepo?
Sababu mojawapo ni kuwa vipimo hivi vya full blood picture vilikuwa vinapatikana sehemu chache kwenye hospitali kubwa tu, ila kwa sasa vipimo hivi vinapatikana karibia kila mahali kuanzia baadhi ya dispensary mpaka vituo vikubwa vya kutolea huduma za afya.
Pili, kuna uwezekano pia mtoa huduma hana ujuzi wa kutosha wa kusoma/kutafsri majibu ya kipimo hiki hivyo anaishia kukupa jibu rahisi kuwa una infection,
Tatu, kuna uwezekano pia baadhi yam mashine hizi za kupima full blood picture zikawa zinakosa ubora wa kitaalam ( technical quality) wa kutoa majibu sahihi wakati wote.
Nne, inawezekana umepima kipimo uko vizuri ila mtoa huduma anakwambia una infection ili akuuzie dawa ili apate faida ya kifedha.
Angalizo,
kama kweli inathibitika pasipo kuwa na shaka kuwa una infection baada ya kupima katika maabara inayoaminika na majibu kutafsriwa na mtoa huduma anayeaminika na ikaonekana unapata maambukizi ya vijidudu/bacteria mara kwa mara ni muhimu kufanya vipimo vikubwa zaidi ili kufahamu chanzo ni nini hasa.
Disclaimer; always consult your health care professional for expert opinion; this post doesn’t substitute your health care provider advice.