Kila nikijaribu kumsamehe/kuwasamehe nashindwa

Chibu hebu Nipe namba za Lyna..katoroka na mimba yangu
 

Chezea hasira kila mtu ana jinsi ya ku react akisikia ampendaye anagawa asali nje hata huyo mme angesikia mke wake analiwa angeweza hata muua huyo mama afadhali hata kapasua tv na hilo shoka kuliko kupasua kichwa cha mtu
 


Sawa mkuu, ila mkuu usiniombee/usinisemee mbaya kiasi hiki, hujui ni kwa jinsi gani hii kitu iliniumiza, nilifanya juhudi Zote kumrudisha mwenzangu ila ikashindikana, na kama umenisoma vzuri mwenzangu alikuwa hanipi nafasi ya kutosha kuongea naye baada ya kuwa ameondoka maana nikiongea naye kidogo tu akakata simu na mwishowe kuzima kabisa.

Mkuu zile pombe nilizokuwa nakunya nilikuwa sinywi kwa starehe mkuu, I bet you know what I mean.

Mkuu nilikosea hilo mpaka kesho nita-admit ila kwenye hii ishu ambaye huwa namlaumu mpaka kesho ni mama Mkwe, yule mama angevaa jukumu lake kama mama mambo yasingefika hapa yalipo, hata kama vitu baadhi vilishauzwa au hata vyote, yule mama angeamua Mtoto wake arudi na kuendelea na maisha angerudi. Mkuu naomba ujue tu kuwa I am not a monster, nina madhaifu yangu kama binadamu mwninge yoyote ila am not a monster boss

Asante
 

Pole sana kwa yaliyokukuta ila hakikisha umetubu kwa Mungu na usirudie hilo kosa maishani mwako Hakuna haja ya kulaumu mama mkwe.
 

Na pia ombea sana watoto wakija kuwa wakubwa wakagundua mama yao Ali react hivyo baada ya kujua ulicheat wata simama na mama yao tu. Mama ni mama na mara nyingi watoto huwa wanaegemea kwa mama hata kama alikuwaje
 
Msamehe na Uwasamehe wote. Ila usithubutu kurudiana nae huyo mzazi mwenzio kabisa kaka. Narudia usirudiane nae
 
Na pia ombea sana watoto wakija kuwa wakubwa wakagundua mama yao Ali react hivyo baada ya kujua ulicheat wata simama na mama yao tu. Mama ni mama na mara nyingi watoto huwa wanaegemea kwa mama hata kama alikuwaje


Sawa mkuu hilo najua linaweza Kutokea na nilishajiandaa kwa ajili yake. Mkuu kuna mambo nilifikiria sana, je niwaache watoto na mama yao wapotee (hapa unaweza sema inawezekana wasingepotea au labda ningefanya juhudi za kuwasaidia wakiwa mikononi mwa mama yao, ila mkuu kila mtu anamjua mtu wake, nadhani unanielewa)au niwachukue nijaribu kuwaandalia maisha, nikamua kwenda na option ya pili.

Kwa hyo hapa nilipo nafanya jukumu langu kama baba, inawezekana watakapopevuka na kuujua ukweli wanaweza kunichukia au sijui itakuweje, nitaongea nao, wanaweza kunielewa au wasinielewe ila nitakuwa nimetimjza jukumu langu kama baba.

Nadhani hasira yao juu yangu haitakuwa Kubwa kama ambavyo labda ningeamua kuwaacha wapotee huku nikiwa na uwezo wa Kufanya kitu juu yao.

All in all tuombee mazuri

Asante.
 


Sawa mkuu.ila sio hadithi hiki ni kisa cha kweli kabisa.
 
Ila ndugu yangu nakushauri mpe access mkeo kuwa anakuja kuwaona watoto wake unazidi kumtesa habari ya wewe kuchepuka ilimtoa kwenye reli mkeo na hii ilichangiwa na asili ya kazi yako ya kwenda mkoani then unarudi hivyo akili yake ilishindwa kupambana na hiyo hali kuwa wewe huko mkoani una mke mwingine hivyo roho yake inakaa juu juu kukuwaza wewe kila uondokapo so ikabidi ajinusuru kwa kuopt kuachana na wewe.KAMA VIPI HEBU TAKE A MOMENT FIKILIA WEWE NDO YEYE NA YEYE AWE WEWE UONE UZITO WA HILI JAMBO HASWA KUKAA MBALI.
Sawa mkuu.ila sio hadithi hiki ni kisa cha kweli kabisa.
 


Mkuu huu ujumbe Wako ni Mkubwa sana sana and I wish mwenzangu angekutana na mtu kama wewe baada ya ile ishu maana hii thread isingekuwa Kwenye server ya JF. Nimeelewa 100% ulichoandika na nakubaliana na wewe 110%

Mkuu Nina madhaifu yangu kama binadamu mwingine yoyote yule Ila Nina ubinadamu Wangu pia, mkuu unamsaidia mtu ambaye anahitaji msaada Wako au hata anaonyesha basi kuhitaji msaada Wako. Mwenzangu baada ya hii ishu Kutoka aliangukia Kwenye mikono mibaya na mpaka Sasa yupo Kwenye mikono mibaya sana.

Mwenzangu hajawai kujutia alichokifanya (inawezekana labda yeye anaona hana cha kujutia, sijui). Kwa hyo hata msamaha aliokuwa anaomba au wanaomba walikuwa wanaomba kwa sababu fulani, trust me I know what I am talking about. Sio kuwa nilikuwa tu na vile niliongelea Kwenye thread, nilikuwa na assets nyingine pia ambazo mwenzangu alikuwa anazijua ila alinikuta Nazo pia.

Baada ya kutokea yaliyotokea bado alikuwa Anataka na sehemu ya zile assets ila alipoenda polisi wakamwambia alifanya kosa kuuza vile vitu kwa hyo hata akifungua kesi haitakuwa na uzito wowote, na haya yote alikuwa anafanya chini ya muongozo wa watu fulani fulani. Kwa hyo she was determined to finish me for good. Hvi mkuu mtu amefanya haya yote (Sawa nilikuwa chanzo) mimi nimepata ajali nimeumia sana, nimelala ndani karibia miezi sita, huyu mtu ananiandikia sms "Nitaendelea kulia na Mungu yakukute zaidi ya hilo". Hivi mkuu hata kama mimi ni malaika huyu mtu nitamwelewa kweli? Ngoja ebu nikae kimya aisee.
 
Kusema ukweli wewe ndiye chanzo cha matatizo na uone aibu kulalamika. "Unamla demu kiaina, sijui kipoozeo" shiiit. Ulitaka yeye afurahi kwa wewe kukosa uaminifu?.
Watu wengi hufanya makosa makubwa halafu wanataka wenza wao wayachukulie kawaida na wawapende kama mwanzo haifai.
 


Sawa mkuu ila hakuna sehemu nimesema yeye ndo chanzano cha matatizo. Ndo.maana nikasema migongano ilianza baada ya sms ya mvhepuko, mwenzangu akaenda kwao nikaenda kumchukua nikamuomba msamaha mbele ya mama yake yakaisha.
 
Mkuu dah nimesoma uzi wako wote nimejisikia vibaya sana lakini yote kwa yote tumshukuru yule mshikaji ambaye alikupa ushauri mzur, ila wanawake ni viumbe vya ajabu sana sijui wanataka nini
 

Pole sana ndio maana nikakushauri uwaweke kwenye maombi ili hata wataka popevuka Mungu awape hekima na busara. Kisa chako ni kama cha shemeji yangu yeye alichukua twin boys wake akawaleta kwa mama yake yaani mama mkwe wangu akawalea mpk wamekuwa kubwa ila wambeya wa mtaani waka waambia ukweli maana wao watoto walijua mama yao aliwatelekeza na mbaya zaidi mpk kimada aliyevunja ndoa ya baba yao walionyeshwa . Hao twins ni wakubwa sasa wako na familia zao ila cha ajabu walimtafuta mama yao na wanamtunza na bibi yao pia wanamtunza ila baba yao mpk namuoneaga huruma maana wala hawanagaiki nae. Twin mmoja akafuata nyayo za baba ake na yeye Ali cheat ndoa ikasambaratika. Twin mwingine aliona hii ni laana ya familia akaamua kuokoka yeye ndio yuko na stable family but cha ajabu wanamtunza mama na bibi yao jukumu la kumtunza baba yao tumeachiwa sisi.
 
mi nikushaur umsamehe tu. ila ucmrudie kabisa. nenda mjin mtafute na kama Mungu amekujalia kidogo mfungulie biashara hata ndogo ndogo. hawa viumbe unaweza kukuta ni dada yake alimdanganya na sasa hib ndio anajutia we msamehe ila ucmkaribie kabisa mfungulie biashara kama unaweza. coz umesema mwenyewe amekuzalia watoto wazur mkumbuke tu hata kwa hilo.
kwa upande wangu mke wangu anajua na kwao wanajua ikitokea tumekosana yeye aondoke tu au niondoke mimi nimuachie nyumba ila cwez kumuachia watoto hilo haijalish sheria zinasemaje. ukitaka kufa zungumzia watoto. mi nikiwa Dar tena nyumban kila iitwapo leo lazima nikae hata lisaa limoja na watoto so ukitaka kifo niambie sijui kisheria hilo mzee naahirisha kwenda mbinguni.
 
Mkuu ,labda mkeo wa zamani unafikili anakuomba msamaha ili Aje kukamilisha mission yake, Na kwanini unafikili ivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…