Kila nikijaribu kumsamehe/kuwasamehe nashindwa

Pole mkuu japo kama elimu dunia umeipata. Songa mbele usigeuke nyuma. Ila tafuta mke ambaye atawapenda wanao
 
Ujue nini mpendwa nilitaka tu uelewe ni wapi umejikwaa na umuelewe mwenzio pia ni wapi alijikwaa. Wewe ndo ulianza lakini wakati mwingine reaction ya mtu unayemkosea inaweza ikasolve tatizo au ndo ikakuza tatizo. Unfortunately reaction ya mkeo ilichochea moto. Lakini hatupaswi kumlaumu sana pia; kwa sababu sio kila mtu ana uwezo wa kuhimili dhoruba kali inapokuja.

Usishangae kwa nini mkeo bado anakuchukia na bado anazidi kuharibikiwa; ni kwa sababu bado hajasamehe; bado amekubeba moyoni mwake. Ule uchungu alioubeba ndo unafanya akufanyie vituko vyote hivyo akifikiri anakukomesha kumbe anajikomesha mwenyewe zaidi. Na kadri maisha yake yanavyozidi kuharibika ndivyo uchungu unavyomuongezeka. Possibly kila muda anawaza "bila mume wangu kuchepuka; leo hii tungekuwa tunaishi kwa amani na watoto wetu". Kila baya analokutana nalo, anakuona wewe ndo kisababishi. So usitegemee yeye kukutakia mema. Siku akipata neema ya kusamehe atajuta sana kwa kuharibu maisha yake mwenyewe. Afu anaweza akasema "bora ufe" ila siku ndo umekufa (God forbid); yeye ndo anaweza akawa analia kwa uchungu kuliko unavyodhani; akatamani uamke ili mmalize tofauti zenu (nimelishuhudia hili sana tu).

So wewe usiumizwe sana na vituko vyake; muombee siku moja Mungu amguse akaweze kusamehe na kutoa uchungu moyoni mwake. Ni kwa faida yenu wote na watoto wenu hata kama kila mmoja ataendelea na maisha yake; amani ni ya muhimu sana
 
Nimesoma kitabu hicho chote naomba urudie maneno haya "Utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe wale waliotukosea" Naomba nikuambie kumsamehe sio kurudiana naye ila nikumtangazia amani. Na vilevile moja ya haki za watoto nikuwajua wazazi wake. Kwanza kuikuwa na tatizo kwako na kwake ingawa wewe umeeleza upande wa matokeo ila nawe unamakosa kwenye hili nalo utubu urekebishe. Maana kuzini wote mlizini sema yeye amepata tunda. Na msingi wa jambo lenyewe ulikuwa mbaya lazima nyumba ianguke. So wewe mtangazie msamaha halafu songa mbele kama unaoa oa endelea na maisha ila watangazie msamaha. Narudia kuwa haimaanishi kuwa anarudi kwenye nafasi yake ila wewe unaondoa kinyongo na unamweleza kuwa nimekusamehe ila utakuwa karibu yangu utakaa kwenye nafasi ulioichagua na unapanga katika hizo wiki mbili za likizo ukitoka huko mgodini wakati watoto wako likizo wanakuwa na muda na mama yao. Ni ngumu ila ukitaka kupona na kuihisha familia yaani watotot wako hilo halina short cut.
 


Sawa mkuu nitajaribu kuzingatia Ushauri Wako.

Hahahaaa...mbona migodi yote imefungwa mkuu.
 

Sawa mkuu....nimekusikia
 


Sawa mkuu nitajaribu kuzingatia Ushauri Wako.

Ila mkuu una maneno,
 

Duuu, mkuu na wewe unajua kutia chumvi, eti kitu Sony bravia 50 inchi curve Mpya kabisa ilipigwa shoka chali kifo cha mende. Hahahahaaaa

We kweli chumvi Namba 2
 
Ila jamani kweli tuseme baadhi ya wanawake nadhan huwa ni pyscho!yaan mtu unaomba hela ua chkula unatumiwa laki 3 alafu unamzengua mwanaume wa hvo??hivi huyu Mungu kwann huwa anakiletea mwenza magimashi?kwann Mungu asikutanishe smart kwa smart?????Mungu tumechoka na haya maisha!..
1.mkeo ana shida 1 tu hajitambui.na vile elimu haipend bas ndo kbs!usimrudie..familia ilikudhalilisha sana!pole mzee baba!
 
Sasa tutajuaje kipi ni kipi labda tupate story upande wa pili.


#NEVER JUDGE ISSUE BY ONE SIDE
 
Sasa tutajuaje kipi ni kipi labda tupate story upande wa pili.


#NEVER JUDGE ISSUE BY ONE SIDE


Sasa wewe unakuwa Kiazi Sasa, we unatuandikia hapa tupate story upande wa pili titaitoa Wapi sisi???

Hii ndo tuliyoletewa kwa hyo kama una chochote cha kucomment comment kulingana na story iliyoletwa huo upande wa pili kama unautaka labda uende mahakamani.
 
Umeona mbali, mwanamke kama hachepuki siku akukamata tena na ushahidi juu, uwii hasamehi kamwe!

Sana sana anakutafutia tukio tu ili akukomeshe japo anaweza kuzuga kukusamehe!
 
We unawajua wanawake vizuri[emoji16][emoji16]
 
Bro pole sana, msamehe amekuzalia wana....ila usimrudie,,,, namaanisha muinue hata kwa ka biashara......yaani mkopo ili asichezee....uliyowafanyia yanatosha......wala usimsogelee.....ila usimwache aelendee kuteseka....inatosha...
 
Sawa Mkuu kama alikuwa hajasamehe angeendelea na maisha yake na kuniacha na wanangu Sasa kisa cha kuuza vitu vyangu nn, kuna uhusiano gani kati ya kusamehe na kuuza vitu?
Si alikuwa anakukomesha mkuu! Bado huelewi tu[emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…