Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Msamehe lakini msirudiane,anaweza kukumaliza.Msaidie sana pale inapowezekana.Pia nawewe muombe msamaha kwa kumkosea coz ww ndio uliesababisha familia kuvurugika.
Ukimsamehe na kurudiana unapoteza nini
Kila mtu anafanya makosa. Ila linapokuja suala la kumuona mzazi mwenzako ni shetani wala siafiki maana tayari kakuzalia watoto wawili. Tujifunze kusamehe maana kama wewe ni mkristo kuna ile sala inasema "Tusamehe makosa yetu kama sisi tunavyosamehe wanaotukosea". Kusamehe hupunguza mzigo wa chuki moyoni na kukufanya uwe na furaha. Samehe na endelea na mambo mengine.Huyu mwanamke ni jini haki ingekua mimi ningekuwa nishamrestisha zamani...ila hata akituma msg milioni usimjibu mpotezee huyo mbwa alitaka kukuharibia maisha yako shetani huyo tena nahisi alikua anakucheat wakat haupo
Stori imejaa kujisifu na uzandiki.
1. Mwanzoni, Ulijivunia vitu badala ya UTU (upendo wa dhati). Ukaibuka na Mtoto wa mjini na genge lake
2. Mchumba/mke uliunganishiwa na ndugu (japo wa mbali) hukumchagua,
3. Mahusiano yako yamejaa washauri kibao (sistr, jamaa wa kazini, mamaz, majirani) miluzi mingi humpoteza mbwa.
4. Mpaka mwanamke anakukimbia (na uwezo ulionao) ujue una tatizo.
**Ku-balance story ilipaswa tumsikie mwanamke nae maana wewe unajifagilia mwanzo -mwisho eg. Nilikuwa na kila kitu (nyumba ya kupanga?), Mark II, nilinunua bati 20,nikanunua shamba 1m
Kusamehe ni jambo ni jingine na kurudiana ni jambo jingine. Kumsamehe mzazi mwenzako haimaniishi utarudiana naye. Hapana. Hicho kitu alichokifanya hata ningekuwa mimi nisingeweza kurudiana naye ila kumsamehe ni nitamsamehe kwa moyo mmoja. Kuwapenda watoto halafu bado una chuki na mzazi mwenzako hiyo siyo sawa kwasababu karibia robo 3 ya hao watoto ni nyama ya mzazi mwenzako. Wewe ulichangia mbegu tu kwahiyo mheshimu na msamehe na pia kuwa na msimamo.Ameshazaa na mwanaume mwingine, na kimsingi huyo mwanamke hjajutia alichonifanyia nahisi msamaha huwa anaomba ili arudi atekeleze tukio jingine labda la kunimaliza kabisa. Huwezi ukaachana na mtu Kwenye Mazingira kama aliyoachna na mimi halafu unaenda kuzaa na mwanaume mwingine. Maana yake ni kwamba like jambo alifanya kwa makusudi ili kunikomoa na sio kuwa shetani alimpitia kama ambavyo huwa wanasema
Ulileta shobo ukweni ukadhan utapata sifa. Pengine hata baba mkwe alikufa kwa stress za mkewe. Ww ndo ukajidai Don.
NB:
Mkwe wangu nae alileta za kuleta. Hela zake anapeleka kanisani ila zangu ndo zimlishe na kusomesha wanae. Nikamchana live siku. Hajarudia. Bila ukauzu dunia hii hutoboi
Umeandika vizuri sana, inavutia kusoma kila hatua.
Pole kwa yote, ila samehee bana hao watoto yule ndio mama yao na unajua vile hakunaga mama wa pili.
Ila kuna wanawake wana roho jamani khaaa.
Kusamehe ni jambo ni jingine na kurudiana ni jambo jingine. Kumsamehe mzazi mwenzako haimaniishi utarudiana naye. Hapana. Hicho kitu alichokifanya hata ningekuwa mimi nisingeweza kurudiana naye ila kumsamehe ni nitamsamehe kwa moyo mmoja. Kuwapenda watoto halafu bado una chuki na mzazi mwenzako hiyo siyo sawa kwasababu karibia robo 3 ya hao watoto ni nyama ya mzazi mwenzako. Wewe ulichangia mbegu tu kwahiyo mheshimu na msamehe na pia kuwa na msimamo.
AiseeMkuu pole sana,msamehe,ukisamehe unakuwa wewe ndio unapata amani.Usininukuu vibaya sijasema umrudie,msamehe alafu muulize what came over her.You need to get to the bottom of all this mess,usije ukarudia tena kosa hilo.Huyu mwanamke alifundishwa na ndugu zake akaona maisha atayaweza peke yake.Alikuwa anakutumi kimaslahi yake na ndugu zake.Hata hizo pesa za vitenge hakuibiwa walipanga.Usimsaidie ndugu wa mke wala mama yake wala shangazi yake wala ukoo wake utarajie malipo mazuri.Wanawake wengi hawana akili hadi wataabike mwanamke unayemuona ni single mother anahistoria ifuatilie.Kosa la kutyomba nje haliwezi kumfanya afanye yote hayo.She was a gold digger.Na alitaka kukuharibia maisha mfanane.Dada zake na ndugu zake na mam yake walikuonea wivu.Wachunge wasikuroge.Wewe umeplay part yako kama baba Mungu atakubariki.Mwanamke hata ukimuona ananyongwa barabarani be very careful usije ukamtettea ovyo ovyo.You will be surprised ukisikia unachoelezewa na anayemnyonga.Hawa watu wakibadilik hata kama aelekea kudumbukia shimoni ambapo hawezi kutoka mwache usimsaidie,anaweza kuja kukugeuka ukaingia matatizoni.Na wasi wasi sisi tulitolewa mbavu moja wao walitolewa fuse moja.Mwanamke akibadilika hata kama ni miss world anakuwa kama shetani,milihoi mla watu.When they get pissed off wanakuwa very ugly my friend.
Kurudiana??? Acha pombe kijana!!!Ukimsamehe na kurudiana unapoteza nini
Msamehe tu uwe huru moyoni mwako hata hivo s ushaamua kuendelea na maisha yako sasa kinachoufanya ushindwe kuwasamehe ni nn??
Acha dunia iwafunze barabara ww lea wanao tu wakikua watamtafta mama yao wakipenda lakini wasamehe