Kila nikikumbuka aibu niliyoipata sitamani tena hata kuonana na yule binti

Kila nikikumbuka aibu niliyoipata sitamani tena hata kuonana na yule binti

Siku hiyo nilienda msibani ambapo nilifiwa na mjomba wangu, sasa kama unavyojua kwenye msiba ndugu mbalimbali hukutana. Na siku hiyo alikuwepo ndugu yangu ambaye alikuwa ni binti mrembo sana na tunafahamiana na kiukweli huwa namtamani sana.

Wakati shughuli za mazishi zimekamilika, tukabaki ndugu tu na watu wengine walitawanyika, sasa nikabanwa na haja ikabidi niende msalani, kufika msalani naingia tu nakutana na kitu kizito yaani mzigo 💩 umeshushwa na kuachwa bila kusafishwa na maji hakuna. Na niliona kabisa ni mzigo mpya usio na muda mrefu.

Nikaona isiwe tabu acha nitoke nikatafute ustaarabu mwingine, ile natoka tu namuona yule mrembo naye anakuja njia ya msalani, tukapishana na moja kwa moja akaelekea msalani na najua alichokiona alidhani tu ni mimi nimeacha ule msala pale kwenye sink.

Kuanzia siku hiyo sitamani hata kukutana tena na yule binti, kila nikikumbuka najihisi niliingia aibu kubwa ambayo kiukweli sikustahili.
Ulitakiwa kumwambia huku chooni nimepakuta pachafu sasa wewe umekaa kimya hapo lazima akuhisi ni wewe
 
Sawa Ningesema sio kusafi lakini swali ni nani kachafua
Kiongozi ukutaka tu kusema kama ni kuchafu ivi nani angeuliza nani kachafua ni Bora kusema kuliko kuonekana wew ndo umechafua ndo maana unaona aibu adi leo
 
Kiongozi ukutaka tu kusema kama ni kuchafu ivi nani angeuliza nani kachafua ni Bora kusema kuliko kuonekana wew ndo umechafua ndo maana unaona aibu adi leo
Huwezi amini kuna wakati ilikuwa tukutane ila nikala kona maana mpaka leo bado nahisi anadhani mimi ni mtu wa hovyo kwa kitendo kile
 
Back
Top Bottom