Kila nikikumbuka CHADEMA walivyowapigania Halima, Bulaya na Matiko kuwatoa jela nauona Upinzani ni Ubatili mtupu!

Kila nikikumbuka CHADEMA walivyowapigania Halima, Bulaya na Matiko kuwatoa jela nauona Upinzani ni Ubatili mtupu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mimi ni CCM lakini nilichanga kwa sababu Halima James Mdee alikuwa ni mbunge wangu wakati ule nami naamini maendeleo hayana vyama.

Lakini nilivutiwa zaidi na busara ya CHADEMA kwamba tuwatoe kwanza hawa akina mama wa Bawacha halafu Mbowe na wanaume wengine wafuate.

Tena Mbowe akasema yeye atakuwa wa mwisho kutoka na fedha isipotosha basi atatumikia kifungo.

Pia nakumbuka jinsi Polepole alivyotimba gerezani na kumtoa Dkt. Mashinji pekee huku hawa Bawacha wakikodoa macho.

Leo hii kweli ndio akina Halima James Mdee wako bungeni kwa niaba ya watu wasiojulikana na siyo Chadema?
Afadhali hata angesaliti mchungaji Msigwa inaeleweka ni mwanafamilia.

Kwa kweli nikifuatilia kinachoendelea Russia nauona Upinzani wa Tanzania ni ubatili mtupu yaani ni " danganya toto"

Maendeleo hayana vyama!
 
Mimi ni CCM lakini nilichanga kwa sababu Halima James Mdee alikuwa ni mbunge wangu wakati ule nami naamini maendeleo hayana vyama...
Weka hoja yako vizuri kuwa wapinzani ni danganya Toto badala ya kutoa tukio la kawaida. Hebu nami niseme upadri au ushehe ni danganya toto! Kisa, mmoja wao amezini na mke wa muumini wake! Huu ni mfano dhaifu sana na ndivyo ulivyo wako.
 
Hao wabunge wa gereji wamefikiri kwa kutumia matumbo.
 
Attachments

  • EtuI3tyXAAIthiA.jpeg
    EtuI3tyXAAIthiA.jpeg
    14.9 KB · Views: 1
Mkuu wametimza haki yao ya msingi ya kikatiba wanayo haki ya kufanya chochote Kama tu aitovunja sheria. By the way mkuu tatizo uchunguzwa kwa kusingatia chanzo chake
 
Weka hoja yako vizuri kuwa wapinzani ni danganya Toto badala ya kutoa tukio la kawaida. Hebu nami niseme upadri au ushehe ni danganya toto! Kisa, mmoja wao amezini na mke wa muumini wake! Huu ni mfano dhaifu sana na ndivyo ulivyo wako.
Wewe mnyasa uliona wapi chama kinapoteza nafasi 19 za wabunge kizembe namna hii?
 
Mimi ni CCM lakini nilichanga kwa sababu Halima James Mdee alikuwa ni mbunge wangu wakati ule nami naamini maendeleo hayana vyama...
Nguvu ilitumika kuwavuta, kuwachanganya.

Haikuwa sawa, kuengua watu, tunakosea. Tunahitaji upinzani wenye tija kama Zanzibar.

Wanasaidia kuondoa makosa.
 
Mimi ni CCM lakini nilichanga kwa sababu Halima James Mdee alikuwa ni mbunge wangu wakati ule nami naamini maendeleo hayana vyama...
Nikupe haki yako bila ubahiri, wewe ni tofauti sana na hawa wengine wengi kama akina Magonjwa, Jinga, Alumni na wengi wengine wenye vibarua vyao humu JF. Pamoja na vimada vyako mbalimbali unavyomwaga humu kutwa kucha, 24/7/52..., baadhi ya hivi vimada hufikirisha kidogo.

Nadiriki kusema, isingekuwa shida ya njaa, huenda wewe ungekuwa mmoja kati ya wazalendo wazuri wa nchi hii; na nina imani, siku moja wakati waTanzania wakishajikomboa kutokana na 'utekwaji', chini ya CCM iliyobinafsishwa kwa mtu, akili yako itanyooka na kuanza kuiweka Tanzania mbele ya kitu kingine chochote.

Sasa, mada uliyoanzisha hapa leo ni mo0ja kati ya zile zinazokusuta moyo wako wa usaliti wa mama Tanzania na kujaribu kujisafisha kiaina.

Kuhusu Halima na hao wenzake, unajuaje kwamba hawapo kazini kama walivyokuwa kazini wale waliotumwa enzi zile toka CCM?

Na kama kweli Halima na wenzake wanatumikia matumbo yao; dalili zote zinaonyesha kwamba CHADEMA wakiweka juhudi kidogo na kuacha ubahiri, wewe utakuwa mstari wa mbele kama askari wao mkuu wa kulipwa!
 
Hapo ubatili wa upinzani unakuja vipi? Sema hao wanawake ndio batili.
 
Back
Top Bottom