Benaya-
JF-Expert Member
- Jul 31, 2019
- 4,415
- 7,631
Mlevi akiwa amelewa huongea kweli yote.Mimi ni CCM lakini nilichanga kwa sababu Halima James Mdee alikuwa ni mbunge wangu wakati ule nami naamini maendeleo hayana vyama.
Lakini nilivutiwa zaidi na busara ya CHADEMA kwamba tuwatoe kwanza hawa akina mama wa Bawacha halafu Mbowe na wanaume wengine wafuate.
Tena Mbowe akasema yeye atakuwa wa mwisho kutoka na fedha isipotosha basi atatumikia kifungo.
Pia nakumbuka jinsi Polepole alivyotimba gerezani na kumtoa Dkt. Mashinji pekee huku hawa Bawacha wakikodoa macho.
Leo hii kweli ndio akina Halima James Mdee wako bungeni kwa niaba ya watu wasiojulikana na siyo Chadema?
Afadhali hata angesaliti mchungaji Msigwa inaeleweka ni mwanafamilia.
Kwa kweli nikifuatilia kinachoendelea Russia nauona Upinzani wa Tanzania ni ubatili mtupu yaani ni " danganya toto"
Maendeleo hayana vyama!
Leo tumejua kazi ya wasiojulikana kupitia mlevi wa maji ya bendera ya kijani mwee