Kila nikirejea kuangalia Mechi za AS Vita Club dhidi ya Al Ahly kule Misri na Kwao Congo DR napatwa na uwoga kwa Mkapa Jumamosi

Kila nikirejea kuangalia Mechi za AS Vita Club dhidi ya Al Ahly kule Misri na Kwao Congo DR napatwa na uwoga kwa Mkapa Jumamosi

Kwa Mpira ule mkubwa wanaoucheza AS Vita Club ambao hata Waarabu wenyewe na Mabingwa Afrika Al Ahly wamekiri kupata nao Taabu nimeamini kuwa nje ya Kucheza Mpira mwingi lakini hata Bahati nayo ina nafasi Kubwa mno katika Mafanikio (Ushindi) wa Mchezo wa Soka (Kabumbu) duniani.

Hofu yangu Kubwa tu ni kwamba kwa sasa Watanzania bado tupo katika Kipindi cha Maombolezo (Majonzi) ya Kufiwa na Hayati Mpendwa Rais wetu Dkt. Magufuli hivyo huenda Wapenzi wa Soka Tanzania na hasa wa Klabu ya Simba tusipojiandaa Kikamilifu kuwakabili AS Vita Club basi baada ya tarehe 3 April, 2021 tukawa na 'Double Majonzi' ya Kufiwa na Kiongozi na pia Kutotinga Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

Naiamini Klabu yangu ya Simba SC tena kwa 100% Ila kwa Mpira mwingi walionao AS Vita Club tukiwafunga au hata tu kutoka nao Sare ya Suluhu (bila bila) au Pacha (ya Magoli) hatimaye tukafuzu rasmi Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika nitaomba Serikali ya Tanzania itoe Tamko la kuwa na Public Holiday nchini.

Moyo wangu una Wasiwasi mwingi sana.
Nimepoteza MB zangu kwa kuamini utakuwa umeandika vitu vya msingi ndani[emoji848][emoji848] ila sio mbaya kichwa cha habari umeandika vizuri sana
 
Wale wanalogwa kama walivyologwa waarabu mpaka wakawa wanainama tu uwanjani.......unakumbuka makusu badala ya kutoa pasi akabutua mpira nje full miguu kugongana....
Nakazia. Mechi ya Simba vs Al Ahly mpira waliocheza Simba unaweza sema ni timu inayotoka barani ulaya hasa hasa kwenye ligi kuu ya uhispania. Kumbe ni ya hapa hapa Africa tena Africa mashariki. Al Ahly walikuwa kama timu ya amateur wanapiga pasi kama vipofu pasi hazifiki na mpira wanautafuta kwa tochi. Simba wanawachezea wanavyotaka. Nilijua kwaaina ya mpira waliocheza nilitegemea Al Merreikh wangekula chuma sita kule Sudan kumbe ile nguvu inafanya kazi uwanja wa Mkapa tu
 
Wasiwasi ndio akili mkuu,na jinsi kundi lilivyo kwa timu tatu za juu kila mtu ana nafasi..sasa unaweza ukaona itakua game ngumu kiasi gani! Uzuri ni kwamba Simba wnalijua hili na tayari wamejindaa vya kutosha..itakuaje? Ni suala la kusubiri na kuona!
 
Vita hakucheza mpira wowote mkubwa pale misrii al ahly alikosa magoli mengi ya wazi pengine ubovu wa yule striker aitwaye bwalya maana alipata chance nyingi za wazi na alikosa zote

Lakini pia kipa wa vita alikuwa imara sana siku ile

Ndo maana vita alikufa kwake 3 bilaa na hao al ahly

Vita wala hatishi ni team ya kawaida tuuu hata akipata matokeo bado haiondoi kuwa yy ni wakawaida na huo ndo mwisho wake

Sent from my X-TIGI_V13 using JamiiForums mobile app
 
Kwa Mpira ule mkubwa wanaoucheza AS Vita Club ambao hata Waarabu wenyewe na Mabingwa Afrika Al Ahly wamekiri kupata nao Taabu nimeamini kuwa nje ya Kucheza Mpira mwingi lakini hata Bahati nayo ina nafasi Kubwa mno katika Mafanikio (Ushindi) wa Mchezo wa Soka (Kabumbu) duniani.

Hofu yangu Kubwa tu ni kwamba kwa sasa Watanzania bado tupo katika Kipindi cha Maombolezo (Majonzi) ya Kufiwa na Hayati Mpendwa Rais wetu Dkt. Magufuli hivyo huenda Wapenzi wa Soka Tanzania na hasa wa Klabu ya Simba tusipojiandaa Kikamilifu kuwakabili AS Vita Club basi baada ya tarehe 3 April, 2021 tukawa na 'Double Majonzi' ya Kufiwa na Kiongozi na pia Kutotinga Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

Naiamini Klabu yangu ya Simba SC tena kwa 100% Ila kwa Mpira mwingi walionao AS Vita Club tukiwafunga au hata tu kutoka nao Sare ya Suluhu (bila bila) au Pacha (ya Magoli) hatimaye tukafuzu rasmi Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika nitaomba Serikali ya Tanzania itoe Tamko la kuwa na Public Holiday nchini.

Moyo wangu una Wasiwasi mwingi sana.
Angalia wasiwasi wako usije athiri maisha yako binafsi,kwani Simba wasiwasi hamna, thalatha bin sufri kwa mkapa,tatu!
 
Ngoja tusubiri tuone mpira dakika 90 zitaongea vizuri kwa mkapa na sio maneno maneno ya Jf.
J'mosi sio mbali tuombe Mungu tufike salama!!!
Nawakilisha!!!
 
Hii mechi sioni simba kama atashinda ata kama ni kwa mkapa sijui kwa magufuli trust me simba anakufa bao tatu bila ubishi
Tukutane hapa baada ya tarehe 3
Sawa... tusubiri tuone.
 
Back
Top Bottom