Kila nikitafuta cha kujivunia mimi kuwa mwafrika nakikosa

Huyo aliyekuletea dini yeye mwenyewe haizingatii, alafu kuna muafrika anapeleka sadaka za kujimaliza kwa mwamposa
 
Maendeleo ya kiuchumi hayana dini, kutoboa kimaisha ni mchakato, sisi watu tunaopenda starehe kuliko kazi vipi tutatoboa? Ndiyo maana wasanii wanatengeneza mkwanja mrefu kuliko hata walimu, wanasiasa wanatengeneza sheria za kujinufaisha zaidi wao kuliko watu wao waliyowachagua. Tunapenda njia za mkato za maendeleo vijana tunajazana kwenye mashine za kubeti halafu tunalalamika hakuna ajira. Angalia wale ndugu zetu wa Afrika Kusini wamefikia kuwafukuza waafrika wenzao eti wanawachukulia ajira, wakati wao ni wameshughulika na Amapiano. Elimu ni kufuta ujinga tu siyo ni tiketi ya ajira, ziko shughuli nyingi tu mtu unaweza kujishughulisha mwenyewe na ukatoboa. Wakina Dangote wanafanya vizuri tu.
 
Shida ya binadamu bwana wanapenda kujifananisha hata hawafikirii kuwa hawawezi kuongeza hata urefu wa sikio
Wenzetu wameendelea sana na hata mchango wa mtu mmoja mmoja unahusika kwenye maendeleo yao , mtoa mada yeye mchango wake ni upi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…