Kila ninapoweka juhudi za kupungua uzito, ndio naongezeka!

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
10,198
Reaction score
35,323
Kwa siku 45 nilikua silii mchana, nakula tu asubuhi chai ya ragi na skonzi moja na yai moja, mchana napiga ndefu, usiku ndio nakula wanga kidogo na chai ndio nalala. Kila siku kabla ya kuoga nafanya pushup 30 na kuruka ruka kidogo kwa lengo la kupunguza kilo, nitoke Kg 94 nirudi Kg 89 za awali kabla ya holiday.

Jana ndio nilienda kupima nione ni mepungua ngapi, to my surprise nimeingia Kg 103! Natimiza hivyo unene ni mwili wa mtu na ni majaliwa na kadari za Mungu. Mke wangu anakula mara mbili yangu milo mitatu hadi minne kwa siku ila anachezea 49kg hadi 55kg ni model kweli kweli ukimuona. Mimi naona nitajiachia tu litakalokuwa na liwe bwana.
 
Kulaaa mzeee kilé ktu rohoo inataka acha kujinyima nyima kisa kupunguza kiloo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu hamna namna hata ni kijima kula na nenepa tu kwahiyo sioni sababu ya kujiumiza napenda sana chapati na maini roast ila nimejinyima kwa mwezi moja na nusi ila sijaona matokeo mpaka leo.
 
Mkuu hamna namna hata ni kijima kula na nenepa tu kwahiyo sioni sababu ya kujiumiza napenda sana chapati na maini roast ila nimejinyima kwa mwezi moja na nusi ila sijaona matokeo mpaka leo.
Kulaaa mzeee km ndio starehe Yako mkuu,,mm asubuh naamka na chapati tatu za jero jero na supu ya buku mbili mix juice ,mchana nakulaa Dona la mama ntilie ,ucku geto naruka hata na wali mboga mboga mix matunda maji yakutosha n vile tu cna mwili wenye shukran mkuu cjawahi ongezeka zaidi ya kilo 69 Wala kitambi cna Wala mwilii[emoji23][emoji23]
 
kupunguza unene inawezekana hasa has ukifuata , utaratibu ufuatayo

-Kupunguza , vyakula vya wanga, ugari wa sembe,wali, n.k, kupunguza uraji wa nyama hasa hasa nyama choma, na kuku hawa wa kisasa

-Asubuhi inatakia ulee chapati moja, na chai au kuacha kabisa

-Mchan kula matunda, inaweza kua ndizi 2 au parachichi moja

-Usiku unaweza kula ugari kidogo au wali kidogo

utaamua , mchana ule matunda au usiku ndo ule matunda

-UKIFANYA MAZOEZI, LAZIMA UTAKULA SAANA NA UTANENEPA , MAZOEZI HAYAPUNGUZI UZITO MBALI YANAONGEZA

nimefanya hao kwa mda wa miezi 5 nimepungua kutoka 70 to 56,
 
Mkuu hongera mimi mwili una ongezeeka ghafra ata nisipo kula sana, kunawalio ni shauri kuachana na gari some time ni tembee kwa mguu au nipende daladala lakini wapi.
 
Mkuu hongera mimi mwili una ongezeeka ghafra ata nisipo kula sana, kunawalio ni shauri kuachana na gari some time ni tembee kwa mguu au nipende daladala lakini wapi.
Unajitesaa mkuuu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pole sana mtoa mada
 
Unaweza kua mkweli mazoezi kunifanya kunwya sanaa maji kwa siku nakua na hamu ya kula sanaa.
 
Je una kitambi ?

Je una maziwa yale ya unene ?

Je una makalio yaliyojaa ?

Je una mapaja zembe yenye nyama ?

Je UNA UREFU KIASI GANI ?
 
Je una kitambi ?

Je una maziwa yale ya unene ?

Je una makalio yaliyojaa ?

Je una mapaja zembe yenye nyama ?

Je UNA UREFU KIASI GANI ?
Maziwa sina yale ya kunenepea kifuani ila sehemu zingine ni kiasi sio vya kutisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…