Niliwahi kufanya mazoezi kila siku asubuhi na jioni kwa lengo la kupunguza uzito, na matokeo nilipata kama ya kwako (kuongezeka) ,nikasema huu ni ushenzi! Nikapiga chini mazoezi ,nikaendelea na maisha yangu.
Baadaye kidogo nilipata ka likizo miezi kama 2 hivi, nikaamua kwenda nyumbani (kijijini) ,nakumbuka ulikuwa msimu wa mvua/kilimo;
Nikasema ngoja namimi nishike jembe nilime viazi (jasiri haachi asili) [emoji23].
Ndg yangu nilivyorudi mjini watu walibaki midomo wazi kwamba nimekonda!!
Nikasema msinitanie, nikaenda kupima uzito[emoji848]
nilikutwa na kg 67 kutoka kg 83..
Najua wewe huwezi kulima[emoji23][emoji23][emoji23][emoji41]
Sasa basi,
Katika harakati zako za kupunguza uzito/unene; hakikisha katika matunda, "limao" iwe namba moja!
Limao ina matokeo mazuri kuliko kukimbia! Fanya hvyo.