Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
hakuna haja ya kubabaika na maisha ya mtu mwingine, eti sijui nani aliishi vipi na aliishia wapi. Hiyo ni Mungu ndie anaejua my friend...Kama kuna la kujifunza wengine wajifunze sasa. Na ni lazima wajilazimishe kutambua ya kwamba kuna kesho. Na kesho ni kubwa kuliko leo
Watoto wa wanasiasa.. Wazazi wenu baadhi mikono yao imejaa damu za watu. Wengine walifika walipofika kwa kuwakandamiza na kuwaumiza wengine.
Watoto wa wanasiasa wa sasa.. Msisahau kuna karma hii kitu haijui neno msamaha unavuna ulichopanda.. Mbaya zaidi matendo ya mzazi huathiri future ya watoto mzazi akiwa hayupo tena dunliani..
Hawa wanaolalama sasa hivi pengine wazazi wao baadhi walikuwa wema lakini kila nyakati zina majira yake.
Niwataje wachache waliojitokeza mbele ya hadhira kutujulisha wanayopitia
Pengine malalamiko yao yanaweza kuonekana hayana msingi ila kuna ujumbe mkubwa sana kiroho inapitia kwenye midomo yao.
- Mtoto wa marehrmu Deo Filikunjombe
- Mtoto wa marehemu kapteni John Komba
- Mtoto wa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mchonga meno rais wa kwanza wa Tanganyika na baba wa Taifa la Tanzania
Wazazi wao walikuwa makada muhimu kwenye chama tawala. Na watu wenye nguvu na umaarufu mkubwa. Lakini Wakati si milele na kesho ni kubwa kuliko leo.
Wao si wa kwanza na wala hawatakuwa wa mwisho.
Watakaosalimika ni watu tu ambao wazazi wao watakuwa na maono ya tafakuri kubwa kwamba
- Kuna maisha baada ya madaraka
- Kuna maisha baada ya umaarufu
- Kuna maisha baada ya siasa vyeo, ukwasi na connection mbalimbali
- Kuna maisha baada ya kifo kwa wale utakaowaacha duniani uzao wa tumbo lako.
kuishi kwa ushauri, maelekezo au vitisho vya kibinadamu ni sawa na ushirikina tu gentleman..
ile muhimu zaidi na ya maana sana ni kwamba, kila moja wetu aishi aishi maisha yake awezavyo, kadiri ya Neema na Baraka za Mungu..
Umepewa zawadi ya uhai, afya, nguvu na vipawa malimbali, vitumie haswa maana muda unakwenda kwa kasi sana...
ukisoma kwa biblia Ayubu 14:1
Inasema,
"Mwanadamu aliezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, nae hujaa taabu" 🐒