Kila rafiki nayempata anataka vita na mimi

Tumetofautiana kidogo tu. Mimi kila rafiki anataka niwe msaada kwake, ila mimi nikihitaji msaada kutoka kwao huwa wanapotea.

Niliwapotezea wote, sitaki hata wajue shuhuli zangu na maisha yangu. Na nimewadanganya sina kazi ndio wamepotea kabisa. Kwangu ndio swaaafi kabisa.
 
Msomi wa chuo hujui tafauti ya hicho na hiko
 
Jisome, jielewe, yaelewe maisha yako na uchague kujifunza kutoka hayo yote. Pengine watu unaoita marafiki huwasomi mapema.
Wasome mapema mbona tabia hazijifichi mkuu?

Yaani utamjua mtu mapema mno na utajiadhari nae, epuka tu hao unaoita marafiki wa kufanya kila kitu we ni mwanaume hayo Mambo tuachie wanawake bro we chagua washkaj tu sio marafiki.

Ficha maisha yako si lazima kila hatua ijulikane au kila mahusiano yajulikane.

Hakikisha washkaj A hawakutani na washkaji zako B
 
Dunia ya urafiki ilishaputwa na wakti...Sasa twaishi kiushkaji na washkaji kwa Machale.

.
 
Rafiki yangu ni Yesu tu. Mtu wangu wa karibu ni mke wangu.
Wengine ni wanadamu wema tu wenye madhaifu kibaoa ambao kila mmoja ninamuweka kwenye kundi la interest husika. Kama ni biashara, Ibada, kazi, stori, etc. Naakikisha nalinda mipaka hiyo kwa wivu bila kujali kama amejipa urafiki au ukaribu au la.
 
Rafiki wa ukweli asilimia kubwa wanapata pindi mkiwa wadogo wote,
yaani kuanzia miaka 4-14
Kama ulikosa rafiki umri huo ndo basi tena,
Maana marafiki wa ukubwani wengi wao sio wa ukweli.
 
Kwa nini hukumripoti kwa wahusika ikiwa pamoja na polisi kwa kuzambaza picha zako ukiwa umelala bila nguo? Kwa nini hadi leo hujawahusisha polisi ikiwa unajua kuwa ana file la picha zako ukiwa uchi ambazo amezipata bila ya ridhaa yako na anatishia kuzisambaza siku moja? Ningelikuwa mimi ningelifanya ujanja wa kuweza kurikodi audio baina ya mimi na yeye tukizungumza kiurafiki kabisa kuhusu issue zote hizo na nitahakikisha katika mazungumzo hayao anakiri kufanya aliyoyafanya na nini anapanga kufanya juu ya file alilonalo na baadae nipeleka audio polisi. Kama hiyo ni ngumu basi ningelianzisha amzungumzo nae ya text
juu ya issue yote na nikasave kila anachosema na nikipata ushahidi wa kutosha napeleka polisi tu maana huyo sio rafiki hata kidogo.
 
Ningeliongezea tu kuwa unapaswa kujua kuwa kuna tafauti kubwa baina ya marafiki na watu unaowajua. Sio kila unaemjua kazini, maskani au chuo ni rafiki, hao ni watu ambao unawajua tu. Kuna msemo wagiriki wanasema hivi " if you have a friend then you are lucky, if you have two friends then you are very lucky but if you have many friends then you are a fool"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…