Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Luhanga Mpina ameyasema haya bungeni na kuhoji kuhusu mamlaka za uangalizi mahabusu kuwa wasimamizi wa mahabusu hizo akisema manyanyaso yanaweza kutokea na hakutakuwa wa kuwawajibisha kwasababu wao wenyewe ndiyo wasimamizi.
Akaongeza kuwa kutakuwa na mkanganyiko mkubwa wa kushughulika na kesi hizo pamoja na kushughulikia upelelezi na vithibitisho vyake sababu hakutakuwa na kufanya kazi kwa haki na uwajibakaji kwasababu wao ndiyo wasimamizi. Mtuhumiwa anaweza kushinikizwa na kulazimishwa kukiri kosa hata kama hajafanya ikiwa msimamizi ndiyo muangalizi hakuna wa kumuangalia na kumuwajibisha.
Akasema itakuwaje taasisi kama TAKUKURU, TAWA, Wizara ya Uvuvi zikapewa mamlaka ya kujenga na kusimamia mahabusu, kesi zao nyingi watu huwa wanasingiziwa, sasa ikitokea kesi kama hizo na wasimamizi wakashiriki kufanya mahabusu kukiri makosa ambayo hawajafanya nani ataziwajibisha mamlaka hizi?