Mkuu sorry kwa kuchelewa kujibu naona Chief Mkwawa kajitahidi kukuelekeza hapo juu...
Binafsi nina kitu hiki nataka nikufafanulie...
Katika KODI huwa kuna repository na addon, repository ni maktaba ambayo hubeba addons nyingi ndani yake. Ni kama vile ilivyo kwa atlas ni kitabu chenye taarifa za ramani za nchi nyingi.
Sasa kuna repositories nyingi tu watu wamekuwa wakizitengeneza mfano lambda, metakettle n.k.
Superrepo nayo ni mojawapo ya repositoy maarufu tu na ni developer wa mwanzo kabisa.(sikumbuki vizuri ndani ya superrepo kama kuna phoenix addon)
Phoenix ni addon kama ilivyo Vdubt25, Sportsdevel n.k
Sasa unapotaka kuinstall addon yoyote kuna njia mbili za kufanya hivyo.
1. Unanstall kwanza repository kwa kuadd source ya repository, kwa kawaida huwa ni url link.
Ukisha-add repository kutokea ndani yake ndio utaendelea kuinstall addon.
2. Njia ya pili ni kudownload moja kwa moja addon file ambalo ni zip, then kutokea katika local storage unainstall hiyo addon kwa KODI.
Hili nilishaeleza huko nyuma post
#176
Kwa kuwa wewe umeshapakua lile file nililoweka basi anza kufuatilia maelekezo hatua ya pili...