Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tumezoea katika maisha yetu tukiangalia Tv basi huduma ile tunaipata kupitia madishi, cable au antenna. siku zinavyosogea mbele na technology ndivyo inavyokuwa na ndio jinsi madish na antenna vinavyopitwa wakati. leo kwenye uzi huu tutaangalia IPTV.
Ni nini hii IPTV?
IPTV ni kifupi cha Internet Protocal TeleVision. Hii ni aina ya uangaliaji TV kupitia mtandao wa internet ambapo kituo cha TV badala ya kutumia satelite dish au cable wenyewe wanarusha matangazo kwa internet.
Unawezaje kuangalia IPTV?
Utahitaji kifaa chenye internet na uwezo wa kustream ili kuweza kuangalia kama vile smartphone, tablet, laptop, desktop hadi TV zenye internet zinaweza kustream.
Internet yenye speed gani inahitajika?
Internet yoyote hata ya edge inaweza kustream ila iwe na latency nzuri, zipo stream zinahitaji speed ya 200kbps tu (25KBps). Kama una latency ndogo hata internet iwe na speed vipi huwezi kustream live utastream tu vitu ambavyo si live. Kujua zaidi kuhusu latency nenda thread hii
Je! mtandao ukiwa na download speed kubwa ndio mzuri ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Je software gani inatumika kustream hizo TV?
Kikawaida browser yenye flash au html5 inaweza kustream tv lakini ukitaka kustream vizuri zaidi software kama VLC au KODI ni muhimu. Kutokana na uhaba wa links za VLC nitazungumzia zaidi jinsi ya kutumuia KODI kuangalizia IPTV.
KODI ni nini?
KODI ni software (media centre) ambayo hutumika kuubadili muonekano wako wa simu uwe kama TV na kuweza kuenjoy TV unazotumia na inapatikana kwenye simu, tablet, computer hadi TV.
![]()
Kuidownload nenda website yao hii hapa chini, ni bure haiuzwi
Downloads | Kodi
Nikishadownload kodi nini kinafuatia?
Utahitaji ku install plugin ili uweze kuangalia TV online. Click video add on halafu chagua watchmojo, install halafu ifungue tuone kama itafanya kazi.
![]()
KODI imefanya kazi, je siwezi angalia mpira na vipindi vyengine?
Unaweza angalia mpira chanel unayotaka kuanzia za ki-Africa kama Super sport, za Ulaya kama Sky sport, za Asia kama Bein sport hadi za kimarekani kama NBC cha muhimu uwe na plugin (add ons) husika, hizi plugin za mpira na michezo mengine zinapatikana tu internet mfano mimi plugin yangu ninayotumia inaitwa Vdtube25 ina channel nyingi sana kuanzia mpira hadi movie.
![]()
![]()
Hio hapo juu sky sport 3
Uzuri wa hizi plugin za kodi zipo TV ni HD na nyengine ni full HD kabisa hivyo internet yako tu.
Malipo?
Kila kitu kuanzia juu hadi hapa ulipofikia ni bure hutoi pesa, ila hizi plugin za bure haziaminiki zipo za kulipia ambazo hazikati ovyo. Mimi sijawahi kulipa natumia tu bure ila kama unahitaji service nzuri zaidi unaweza kulipa ila pia kuwa makini na matapeli
Tutorial ya kuweka na mahala pa kupatia plugins
Plugin yangu ninayotumia ya vdtube25
Tutorial How to Install VdubT25 Add-On Kodi XBMC
Website hio hio pia utapata plugins nyingi.
Kama una swali lolote usisite kuuliza chini
kama uliinstall addons kama .zip file hutapata updates hivyo unahitajika kucheki version mpya manual mahala ulipodownloadia
kama uliinstall repository kwanza utapata updates.
ni kawaida kwa addons kufa unatakiwa utafute mwenyewe nyengine.
just google utazipata nyengine mpya
Vipi unatumia PC au smartphoneChief mkwawa hebu niweze nami niweze kuioakua hiyo kodi kwani hiyo link sijui uliyoeka hapo nafungua but sioni namna ya kuweza kuidownload kabisa msaada , samahani kwa usumbufu makala zako hua nazifatilia kwa umakini sana na kuanza kujaribu kupractice kidogo kidogo hivyo na niko kwa hii iptv
Ingia playstore download hiyo KODI halafu ingia google andika shaniTVSmartfone