Kila unalotakiwa kujua kuhusu IPTV (kuangalia TV kwa kutumia internet)

Kila unalotakiwa kujua kuhusu IPTV (kuangalia TV kwa kutumia internet)

Chief mkwawa heshima kwao mkuu,ninaomba unisaidie nifanyeje ili niki UPLOAD PICHA ILI KUI INSERT KWENYE HABARI IFANIKIWE,HII NI WIKI YA 2 HAIKUBALI,PLS
 
Tumezoea katika maisha yetu tukiangalia Tv basi huduma ile tunaipata kupitia madishi, cable au antenna. siku zinavyosogea mbele na technology ndivyo inavyokuwa na ndio jinsi madish na antenna vinavyopitwa wakati. leo kwenye uzi huu tutaangalia IPTV.

Ni nini hii IPTV?
IPTV ni kifupi cha Internet Protocal TeleVision. Hii ni aina ya uangaliaji TV kupitia mtandao wa internet ambapo kituo cha TV badala ya kutumia satelite dish au cable wenyewe wanarusha matangazo kwa internet.

Unawezaje kuangalia IPTV?
Utahitaji kifaa chenye internet na uwezo wa kustream ili kuweza kuangalia kama vile smartphone, tablet, laptop, desktop hadi TV zenye internet zinaweza kustream.

Internet yenye speed gani inahitajika?
Internet yoyote hata ya edge inaweza kustream ila iwe na latency nzuri, zipo stream zinahitaji speed ya 200kbps tu (25KBps). Kama una latency ndogo hata internet iwe na speed vipi huwezi kustream live utastream tu vitu ambavyo si live. Kujua zaidi kuhusu latency nenda thread hii
Je! mtandao ukiwa na download speed kubwa ndio mzuri ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Je software gani inatumika kustream hizo TV?
Kikawaida browser yenye flash au html5 inaweza kustream tv lakini ukitaka kustream vizuri zaidi software kama VLC au KODI ni muhimu. Kutokana na uhaba wa links za VLC nitazungumzia zaidi jinsi ya kutumuia KODI kuangalizia IPTV.

KODI ni nini?
KODI ni software (media centre) ambayo hutumika kuubadili muonekano wako wa simu uwe kama TV na kuweza kuenjoy TV unazotumia na inapatikana kwenye simu, tablet, computer hadi TV.
Kodi-devices-smudged.jpg


Kuidownload nenda website yao hii hapa chini, ni bure haiuzwi
Downloads | Kodi

Nikishadownload kodi nini kinafuatia?
Utahitaji ku install plugin ili uweze kuangalia TV online. Click video add on halafu chagua watchmojo, install halafu ifungue tuone kama itafanya kazi.
9vW4MHp.jpg


KODI imefanya kazi, je siwezi angalia mpira na vipindi vyengine?
Unaweza angalia mpira chanel unayotaka kuanzia za ki-Africa kama Super sport, za Ulaya kama Sky sport, za Asia kama Bein sport hadi za kimarekani kama NBC cha muhimu uwe na plugin (add ons) husika, hizi plugin za mpira na michezo mengine zinapatikana tu internet mfano mimi plugin yangu ninayotumia inaitwa Vdtube25 ina channel nyingi sana kuanzia mpira hadi movie.
zNbDtYR.jpg

PppArCw.jpg


Hio hapo juu sky sport 3

Uzuri wa hizi plugin za kodi zipo TV ni HD na nyengine ni full HD kabisa hivyo internet yako tu.

Malipo?
Kila kitu kuanzia juu hadi hapa ulipofikia ni bure hutoi pesa, ila hizi plugin za bure haziaminiki zipo za kulipia ambazo hazikati ovyo. Mimi sijawahi kulipa natumia tu bure ila kama unahitaji service nzuri zaidi unaweza kulipa ila pia kuwa makini na matapeli

Tutorial ya kuweka na mahala pa kupatia plugins
Plugin yangu ninayotumia ya vdtube25
Tutorial How to Install VdubT25 Add-On Kodi XBMC

Website hio hio pia utapata plugins nyingi.

Kama una swali lolote usisite kuuliza chini
 
Acha nilale, I wish Ajazeera wangekuwa wanaonyesha mpira maana yenyewe ndo tu inaonekana zingine zote zimefail, nitaangalia matokeo ya The Gunner kwenye apps ya LIVESCORE
 
Naomba kuuliza ivi HAWA bein sports ligi ya EPL wanaonyesha Chanel namba ngapi??
 
Naomba kujua kuhusu TTCL IPTV nilidownload app. yao nikaangalia kama siku tano wakanikatia kabisa
 
Wadau hii kodi kwangu add ons zote zinakataa kufunguka si,sports devil wala phoenix,money sports nk yaani zote na hata ikikuonyesha kuwa inataka update inagoma ukiiupdate sasa naomba kama kuna njia nyengine yakuweza kuziingiza upya.
 
Yani hata mimi mkuu nimepata Aljazeera peke yake lakini nilizoingiza zote zimegoma naomba maelekezo zaidi huenda nimekosea wana jf
 
kama uliinstall addons kama .zip file hutapata updates hivyo unahitajika kucheki version mpya manual mahala ulipodownloadia

kama uliinstall repository kwanza utapata updates.

ni kawaida kwa addons kufa unatakiwa utafute mwenyewe nyengine.

just google utazipata nyengine mpya
 
kama uliinstall addons kama .zip file hutapata updates hivyo unahitajika kucheki version mpya manual mahala ulipodownloadia

kama uliinstall repository kwanza utapata updates.

ni kawaida kwa addons kufa unatakiwa utafute mwenyewe nyengine.

just google utazipata nyengine mpya

got u mkuu mimi niliinstal kama zipi file daaah ngoja nizitafute mtandaoniii
 
Naomba kuzifahamu hizo add ons nyingine ambazo ni free si kwasababu ya kushindwa kugoogle hapana nimeona ni vyema kuzifahamu kwa MTU anayezifahamu vizuri.
 
Chief mkwawa hebu niweze nami niweze kuioakua hiyo kodi kwani hiyo link sijui uliyoeka hapo nafungua but sioni namna ya kuweza kuidownload kabisa msaada , samahani kwa usumbufu makala zako hua nazifatilia kwa umakini sana na kuanza kujaribu kupractice kidogo kidogo hivyo na niko kwa hii iptv
 
Chief mkwawa hebu niweze nami niweze kuioakua hiyo kodi kwani hiyo link sijui uliyoeka hapo nafungua but sioni namna ya kuweza kuidownload kabisa msaada , samahani kwa usumbufu makala zako hua nazifatilia kwa umakini sana na kuanza kujaribu kupractice kidogo kidogo hivyo na niko kwa hii iptv
Vipi unatumia PC au smartphone
 
Ndugu zangu namaanisha wana jf wote kwa ujumla hasa mliofanikisha thread hii ya mambo ua iptv natoa shukurani nyingi kwenu kwani nimepata mwangaza mkubwa ktk kufahamu iptv na sasa tv iko mbali kabisa nami kwani nina apps mbili katika simu yangu zinaniwezesha kuona soka live bila kukwamakwama nazo ni MOBDRO na KODI asanteni sana Mungu awajalie mpate mengi zaidi ya kutusaidia sisi wengine
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Duh! Leo nimetazama gem ya MAN U na STOKE live ndani ya supersport 7 kupitia ktk simu
 
Back
Top Bottom