Superintendent kimura
JF-Expert Member
- Feb 24, 2023
- 549
- 2,005
“Kuna VITABIA vinavyofanana na MSAADA… lakini ni UTAPELI dhidi ya maisha yako.”
Havikupi faida.
Havikuongezei thamani.
Havikujengi.
Ni mianya ya kutolewa nguvu, pesa, muda, na akili bila kurudi na chochote.
01. Kukopesha Ndugu na Marafiki – “Mnaingia marafiki, mnatoka maadui.”
Kwenye familia za Afrika, ukikopesha pesa unajenga chuki kuliko upendo.
Utakopesha 50k, atakudai huruma.
Ukidai, utaitwa mkali.
Na mwisho unabaki bila hela na bila urafiki.
Wakikuthibitishia “Nitakurudishia jioni”
Hiyo ndiyo guarantee ya kutodai tena.
02. Kusponsa Mishangazi / Matukio ya Kifamilia – “Unajenga jina ambalo halikulipi.”
Familia ikishajua wewe ni “mtu wa kutoa”, watakufanya ATM.
Kila kitchen party, sendoff, birthday ya mtoto wa mtu—
Wewe ndio unatakiwa ulete bahasha.
Lakini hakuna anayekupa network, mentor, au biashara.
Ni gharama ya kijinga yenye heshima ya muda mfupi.
03. Kusomesha Binti Ambaye Sio Mke Wako – “Wewe ni sponsa tu, sio mchumba.”
Ukimlipia ada, hosteli, chakula, unamuhudumia mtu ambaye hatakaa na wewe.
Wanawake wengi wa sasa wana “support system” 5:
Mmoja wa ada, mmoja wa airtime, mmoja wa chakula, mmoja wa usafiri, na mmoja wa emotions.
Wewe ndio namba 3 kwenye payroll.
Na mwisho unatangaziwa harusi Facebook.
04. Kusomesha Mtoto Shule za Ada Kubwa Lakini Hakuna Malezi ya Uwezo – “Unamtengeneza kuwa mzigo.”
Shule za gharama si tatizo.
Tatizo ni mtoto hana:
✔ Ujuzi
✔ Nidhamu
✔ Kujiamini
✔ Majukumu
Anahitimu Form Six lakini bado anauliza:
“Baba, nitapewa hela ya vocha?”
Hapo ni mzigo, sio uwekezaji.
05. Kupokea Mshahara Mdogo Unaofanana na POSHO – “Huo sio ushindi… ni modern slavery.”
Kuna mshahara unalipa bili, sio maisha.
Unatumia miaka 5 kwa 250k–400k…
Huo si mshahara, ni kukubali kunyimwa thamani yako.
Kijana ana degree, analipwa 300k lakini kila mwezi anatumia 40k kwenye daladala, 150k kwenye chakula, 80k kwenye vocha
Anabaki na 20k.
Hapa unafanya kazi ili usife, sio ili uishi.
06. Kuwa “Bank ya Familia” – “Tatizo sio wao, ni wewe.”
Kila mtu akikwama, anakupigia.
Wakilipa deni, hawakumbuki
Wakikuona mjini wanakuita:
“Mkuu mambo shwari? Naomba sapoti kidogo.”

Wakilipa deni, hawakumbuki.

Huo ni utapeli wa kihisia.
07. Kutegemea Serikali kukubadilishia Maisha – “Hiyo si ndoto, ni usingizi.”
Unangoja serikali ikupe ajira…
Ikupe mtaji…
Ikupe motivation…
Itakudanganya kwa miaka 10.
Jim Rohn alisema:
08. Kuwa Mtu wa Kila Mtu – “Unageuka mtumwa wa approval.”
Unajitoa sana kupata upendo kutoka kwa watu ambao hawana muda na wewe.
Uko kwenye vikundi 12 vya harusi, sendoff, michango, sherehe, misiba—
Lakini hawana hata interest ya kukutumia seminar moja ya kukuza skills.
09. Kuwa Mfadhili wa Mahusiano Ambayo Hayana Ndoto – “Love without vision is a liability.”
Kama mpenzi wako hana direction, hana malengo, hana kazi ya kujenga,
basi unachofanya si mapenzi…
Ni ufadhili.
Unalipa bili, vocha, nails, wigi, outing…
Ni gharama ya mtu asiyezalisha chochote.
10. Kutoa Sadaka Zaidi ya Bajeti Yako – “Mungu hapokei ujinga.”
Huwezi kutoa 50k kanisani halafu huna pesa ya chakula nyumbani.
Sadaka sio clearance ya kutorudia makosa ya kifedha.
Ni ibada, sio investment plan.
"Kama haikuletei faida—ya pesa, akili, network, au character—ni UTAPELI wa maisha yako."
Sio lazima mtu akudanganye…
Wakati mwingine unajidanganya mwenyewe.
Value yako inakuwa kubwa pale unapoweka mipaka.
Credit to
Mwl.Benjamin Madaha

“Education without responsibility is entitlement.”

“Don’t wish it was easier. Wish you were better.”