Kila unayemuana Duniani na hali zote unazozipitia ni mtokezo wa mawazo yako kwa nje

Kila unayemuana Duniani na hali zote unazozipitia ni mtokezo wa mawazo yako kwa nje

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Hakuna hali unayoipitia inayotoka nje yako ila ni taswira zako wewe mwenyewe unazozitoa nje yako .Hali ya kutolielewa kwa mapana yake na uhakika wake thabiti ni gereza kubwa la maisha yetu tulio wengi kwa sababu tumezoezwa sana na mazingira ya nje kiasi cha kuamini tunayoyaona ndiyo halisi na ndiyo yanayotubadilisha badala ya sisi kuyabadilisha.

Dunia ni kama kioo kinachokuonesha wewe, kwa maana nyingine yote tunayoyaona Duniani ni wewe ndiye unayejiona. Kuchelewa kufahamu hili ni zaidi ya gereza la Binadamu. Ni kifungo Cha hatari sana kuliko kifungo chochote kile kuwahi kutokea Duniani.

Wengi wetu leo ni watumwa wa mitazamo potofu juu yetu kutokana na sababu mbalimbali ( Dini, Jamii, Elimu) vimetumika kuufunika ukweli kwa kiasi kikubwa sana kutokana na kizazi kupokea maarifa potofu kwa kujua au kutojua kumetufanya kuishi maisha ya utumwa kwa miaka mingi na cha ajabu utumwa huo unaonekana ni kawaida ya maisha.

Hakuna kinachoweza kubadilika tusipobadilika kwanza sisindani yetu kwanza. Matokeo yoyote tunayoyataka hayawezi kutokana na kinachoonekana nje ila kile cha ndani. Ni kama tunataka kuondoa tongotongo linaloonekana kwenye taswira ndani ya kioo badala ya kuondoa tongotongo Hilo ndani yetu.

Leo tunasema Dunia tambara bovu ila kwa hakika sisi wenyewe ndiyo ubovu huo. Ndani yetu kumejawa na ubovu na ukichaa usiomithilika unaojionesha kwenye kioo Dunia.

Tumekuwa tukiamini Mungu yupo juu mbinguni ila kwa hakika Mungu yupo ndani yetu (ni sisi wenyewe) tumesahaulishwa na ukichaa. Tunatazama juu badala ya kutazama ndani yetu kiuyabadili maisha yetu.

Binadamu ni taswira ya Mungu "image of God" na taswira ya kitu inatokana na kitu chenyewe. Hakuna kitu hakuna taswira. Hakuna Mungu hakuna mtu. Uelewa sahihi na chanya, kujitambua na kuamka kutoka kwenye giza la kutokufahamu au ufahamu potofu ni kujijua kuweka wewe ni Mungu.

Mungu ni kila kitu ndani ya kila kitu. Kila kitu kina uungu ndani yake usijidharau. Uelewa potofu ni kifo, ni kuwa gizani, ni gereza kubwa, ni Jehanamu. Kuamka ni kuishi katika pepo ni kuwa mbinguni, ni Duniani kama Mbinguni na Mbinguni kama Duniani.

Ukipitia vitabu vyote vitukufu utabaini vinauelezea ukichaa wa binadamu kutokujifahamu, kutokuamka, kuwa gerezani na kumtaka ajifahamu yeye ni nani. Kifo kinachotajwa na vitabu hivyo ni ufahamu potofu. Mtu asiyejifahamu amekufa, hivyo vinatutaka kuwa hai tena.

Ufahamu sahihi ni kuamka na kujua wewe ni sehemu kamili ya Mungu na kuishi kama Mungu hapa Duniani siyo kusubiria peponi mwili ukishakufa. Ufalme wa Mungu upo pia Duniani na watu wanauishi ufalme huo. Tamani kuwa sehemu ya tamanini la Mungu aliyeziumba mbingu na kwa kutoka usingizini au ndotoni na kuanza kuishi. Na hii ndiyo maana ya ujio wa Masihi kwa mara ya pili. Ndiyo maana ya Yesu kurudi Duniani na kulinyakua Kanisa.

Asilimia kubwa ya wanadamu tunaishi katika ulimwengu wa ndoto na maruweruwe (mawenge) kwa sababu tumeleweshwa sana na usingizi na kuamini ndiyo maisha halisi. Tupo Duniani kuonesha ukuu wa Mungu na hii ndiyo maana halisi ya Mungu yupo kila mahali.

..................................................
Amka ndugu, tumeishi ndotoni kwa muda mrefu sana kiasi cha kuona ni kawaida kumbe siyo kawaida.
 
Back
Top Bottom