chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Naona kama hakuna makala sheheni ambazo zitaelezea hali ya nchi tangu uhuru zilizoandaliwa na kila Wizara/Idara ili kutanua wigo wa ufahamu wa jamii ya sasa. Hata kama zipo, basi kuna taasisi (hasa TBC na Idara ya Habari Maelezo) wamezihodhi, na hawataki jamii izifikie.
Kama nchi tunahitaji vijana wajue hali ya barabara tangu ukoloni, away ya kwanza, mpaka ya sasa. Hii inasaidia watu kujua nchi ilipotoka mpaka sasa ilipofikia. Tusije kuona daraja la Busisi au Tanzanite, bila kujua safari iliyohusika.
Katika ardhi pia, viwanda, maendeleo ya elimu na kila kitu.
Iwe documentary hasa sio zile za TBC mtu anaandaa kama anakimbizwa, iwe documentary ambayo itaishi miaka kadhaa mbele.
Ionyeshwe siasa kuanzia wakati huo wa ukoloni mpaka sasa, watu waelewe nchi yao kwa nini ilipitia hatua fulani.
Siku kama ya leo pasiwe na ombwe la habari katika makala, zisambazwe bure katika vyombo vyote vya habari watu walijue taifa lao