PreGE2025 Kile anaandaa Lissu ni kuandaa nchi kwa machafuko

PreGE2025 Kile anaandaa Lissu ni kuandaa nchi kwa machafuko

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Bora tu sababu masikini tupo wengi, ajira hamna alafu viongozi na chawa wao wanatembelea magari ya nusu billion.

Acha tufe tukipambana huenda wachache watakaobaki watatengeneza nchi yao ya haki
Kufa wewe,Bora kuwa maskini kwenye amani nusu kuliko kuwa maskini kwenye vita.

Nadhani ya Sudan mnayaona
 
Bora tuwe na machafuko yanayolenga kutukomboa kwenye minyororo ya CCM kuliko kuwa na amani ya uongo
Maua Mkuu💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐🌸💐💐💐💐💐💐💐💐💐
 
Tumewahi kuona clip za video zilizovuja wazungu wakiwa kwenye mikutano yao wakipanga namna Afrika inatakiwa kuwa eneo la vurugu mapigano na maafa kusudi wenyeji wabakie masikini.

Kwamba Maliasili za Afrika ili ziweze kuvunwa sawa na bure waafrika wasiruhusiwe kuzitumia au kuzivuna kwa maendeleo yao Kwa sababu wakiendelea watahitaji kutumia rasilmali zao na huku wazungu wanazihitaji.

Kwa hakika ni roho mbaya na za ubaguzi dhidi ya waafrika maana tumeona wachina wakiwa na sera ya kutaka waafrika wafaidike na kupata maendeleo kutokana na mali asili yao.

Wao wanaamini watu wakiendelea wanakuja na mahitaji zaidi Kwa hiyo biashara inakua kubwa zaidi duniani na kuwafaidisha wote.

Wazungu wanasambaza vita Afrika na wanatumia vibaraka kama Kagame mbabe wa vita vya kimbari ya kitutsi mwenye kuamini watutsi ni mbari iliyozaliwa kutawala wabantu kusambaza vita na vurugu.

Hapa kwetu tunasoma madai yasiyokua na tija ya chadema ya lissu kutaka kusimamisha uchaguzi. Hata mwenyewe Lissu anajua CHADEMA Haina uwezo kusimamisha uchaguzi Tanzania ila bila shaka kuna nguvu nyuma yake toka wale mabeberu wenye kuombea vurugu nchi zetu waweze kugawana na kuokota ngawira kirahisi huku tukigombana au tukipigana na kuuana wenyewe Kwa wenyewe
Thibitisha maneno yako
 
Hizo video za wazungu kupanga Africa iwe sehemu ya machafuko ziko wapi , hebu zipandishe hapa tuone.

Yaani mtu maji safi na salama ni shida,watoto wanakaa chini hakuna madawati , wanaomudu kula mlo kamili ni kiasi kidogo kwenye nchi halafu ndio uombewe machafuko?

Yaani Lissu kukataa upumbavu wa kushiriki kitu unachojua kitapindishwa ndio iwe anapanga machafuko?

Nakuwekea hapa video uone Lissu anachopinga na je wewe ungekuwa Lissu ungekubali chama kishiriki unaoitwa uchaguzi halafu kuna chama kingine kinaingiza kituoni kura zilizopigwa kwenye mabegi?
 
Screenshot_20250405_004437_X.jpg

Ballot Stuffing ikifanywa na Polisi ambao jeshi ambalo liliundwa kwa ajili ya kulinda Raia na Mali zao linatumika KUPORA HAKI za Raia.
 
Kile ccm wanaandaa Tanzania kwa dhuluma ni machafuko; style ya ccm kuongoza imemtengeneza Lisu, na itaendelea kutengeneza ma Lisu wengine.
 
Pale HAKI inaposhindikana kupatikana kwa njia za amani na za Kidemokrasia, basi Vita huwa inakuwa ndio silaha ya mwisho kabisa katika kupatikana kwa hiyo HAKI. Hakuna njia nyingine yoyote mbadala zaidi ya hiyo.

Mwanafalsafa Jeffs O'Brien aliwahi kusema kwamba "Njia pekee ambayo Wananchi wataitumia katika kuzungumza au kujadiliana na Watawala wao ambao ni Madikteta ili kufikia muafaka wenye maslahi kwa pande zote mbili ni kwa KUPITIA MTUTU WA BUNDUKI."

[Ufafanuzi umeongezwa]


Mfano mzuri zaidi uliotokea siku za hivi karibuni kuhusiana na masuala kama haya ni kule nchini DRC, katika Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.
Kutokana na kukosekana kwa HAKI, Watu/Wapiganaji wa M23 walikuwa wanaomba mazungumzo na Utawala wa nchi yao hiyo kwa muda mrefu Sana (tangu zamani miaka ya 2012) lakini bila mafanikio yoyote yale. Utawala wa nchi hiyo ya DRC daima ulikuwa unakataa kukutana na hao watu wa M23. Lakini mara tu Wapiganaji hao wa M23 walipoanzisha vurumai dhidi ya Utawala wao, mara moja Rais wa nchi hiyo ya DRC sasa amekubali kukutana na Watu wa M23 ili wazungumze na kumaliza tofaufi zao.
Je, unafikiri mazungumzo hayo kati ya M23 na Rais wa DRC Felix Tsishekedi yangewezekana kufanyika endapo kama Watu wa M23 wasingechukua maamuzi magumu na hatua kali kama hizo walizochukua huko Goma na Bukavu? Ingewezekana kweli?
Tatizo hao M23 hawabebi malalamiko ya umma ila ya mbari yao ya kitutsi kwa hivyo ni tatizo juu ya tatizo. Na wanachopigania sio suluhu kwa wote maana wanataka wao ndio watawale mbari zingine. Hawasemi wazi ila angalia Rwanda ndio utaelewa kile wanapigania m23.
 
Back
Top Bottom