Kile kirusi vipi?

Kile kirusi vipi?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Sasa hakibambi tena kama ilivyokuwa!

Zile hekaya za makaburi ya watu wengi [mass graves] hazivumi tena.

Hata makamanda nao naona wamekubali matokeo. Wameona kirusi hakina shobo kivile. Nimemwona ‘jasusi’ mbobezi akiselfika na wanasiasa wa upinzani bila barakoa wala tahadhari yoyote dhidi ya huyo korona.

Hakuna cha kukaa mbalimbali [social distancing] wala nini.

Kiki za kirusi Rais Magufuli kaziua kabisa. Niseme tu ukweli kuwa kwenye hili nimemkubali saaana.

Kesho ACT wanakutana Mlimani City [katika kile kinachosadikiwa kuwa ni kutangaza ujio wa ‘jasusi’ mbobezi kwenye chama chao]. Sitarajii kuona nyuso zilizofunikwa na barakoa na sitarajii kuona ukumbi ulio mtupu [ingawa wanaweza kubadili mipango yao dakika za mwisho ili tu wafanye nionekane sijui kitu 😄].

CCM walifanya mkutano wao wiki iliyopita. Hivi kuna mtu hata mmoja aliyekuwa kavaa barakoa? Social distancing ndo kabisa! Ni foreign concept 🤣.

Hebu waone...

Bado msimamo wangu kuhusu COVID uko palepale. Huo ugonjwa au sijui hako ka kirusi, siyo hatari kama tunavyoaminishwa.

Magufuli oyeeee kwa kusimama kidete kupinga na kukataa kutishwa tishwa na mawakala wa kusambaza uoga na uongo.
 
Wakivaa ili uonekane hujui watwange tena kivingine[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu korona ipo tena sasahivi imekuja kivingine
Ni mwendo wa maumivu ya mgongo shingo kifua mbavu kubana pamoja na kutokusikia harufu ya kitu chochote

Lakini vifo havipo ni mwendo wa nyungu kwa kwenda mbele
 
Kuna kale kanyumbu ka g sam kalikuwa kananengua viuno eti kanatangaza tanzia za viongozi kakijifanya kenyewe kako ndani ya system! [emoji23][emoji23][emoji23]

Siku hizi kanalilia eti kanalalamikia wanaochukua form za kugombea huko ccm.

Yani wakisindikizwa na yule nyumbu aliekuwa kuke twiter wakikuwa wanalishana matango pori hadi wanavimbiwa,!

Yule mwenyekiti wao mnywa konyagi, alilodharau maombi yaliyoitishwa na rais manajua kilichomkuta.

Kuna pia tule tu nchi jirani tulimtukana sana JPM kisa hajashiriki tuvikao twao ambato Kabudi alituita tuvikao twa kwenye corido na sijui tulileta impact gani kwa tunchi twao maana mnajua kinachowakuta.

Hakika Magufuli amenifunza kitu kimoja, "mwanaume kuwa na msimamo"
Ila ukiwa mwanaume lialia kama alivyo Kenyata, Mbowe na wafuasi wao utachapiwa hadi mke huku unashuhudia.

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu korona ipo tena sasahivi imekuja kivingine
Ni mwendo wa maumivu ya mgongo shingo kifua mbavu kubana pamoja na kutokusikia harufu ya kitu chochote

Lakini vifo havipo ni mwendo wa nyungu kwa kwenda mbele

Kuwa ipo, sikatai.

Lakini si hatari kivile.

Mi mwenyewe si ajabu niliipata mnamo mwezi wa pili.

Wala haikuwa mbaya kivile.
 
Hako kakirusi nilikapata last week, hakana nguvu kiviile, nilikadhibiti kwa tangawizi tu
 
Mkuu korona ipo tena sasahivi imekuja kivingine
Ni mwendo wa maumivu ya mgongo shingo kifua mbavu kubana pamoja na kutokusikia harufu ya kitu chochote

Lakini vifo havipo ni mwendo wa nyungu kwa kwenda mbele
Mkuu wiki hii nimeumwa shingo 😂😂😂 lol. Ujumbe wako umenistua maana nilikuwa najiuliza shingo hii vipi siku ya nne haipoi
 
Mtu ambaye kazi yake ni kushinda stoo na kubeba mabox tu lazima akili yake ivurugike.
IMG-20200715-WA0045.jpg
 
Hawa "wanaharakati wa barakoa" walikuwa na kiherehere ajabu.

Ujuaji ujuaji tu, kelele nyiingiii kana kwamba wanaijua corona kuliko mtu yeyote yule.

Kwa kweli magufuli kawakomesha.

Hii ni safi sana!
 
Huko Marekani ulipo wameshakufa watu wangapi kwa korona? Last time I checked ni zaidi ya 138k. Just because uliugua korona kisha "ukapona" doesn't mean you are immune to it Kwa sababu a lot is not known about both the virus and the pandemic.

Badala ya kufanya mzaha kwa kuwakebehi wapinzani ambao kosa lao pekee lilikuwa ku-raise public awareness kuhusu gonjwa hilo, ungejihangaisha kuelewa nini kinaendelea Tz. Mtafute daktari asiyejihusisha na siasa akuelikishe. Kuyaangalia mambo muhimu kwa taifa letu kwa miwani ya mbao ya itikadi za siasa na UKABILA ni ugonjwa hatari zaidi ya korona.
 
Attachments

  • Screenshot_20200716-011833_Chrome Beta.jpg
    Screenshot_20200716-011833_Chrome Beta.jpg
    15.1 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200716-012448_Chrome Beta.jpg
    Screenshot_20200716-012448_Chrome Beta.jpg
    95.1 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200715-004545_Chrome Beta.jpg
    Screenshot_20200715-004545_Chrome Beta.jpg
    103 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200715-004630_Chrome Beta.jpg
    Screenshot_20200715-004630_Chrome Beta.jpg
    118.1 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200715-004751_Chrome Beta.jpg
    Screenshot_20200715-004751_Chrome Beta.jpg
    67.7 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200708-130139_Chrome.jpg
    Screenshot_20200708-130139_Chrome.jpg
    104.3 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200716-013741.jpg
    Screenshot_20200716-013741.jpg
    159.9 KB · Views: 1
Huko Marekani ulipo wameshakufa watu wangapi kwa korona? Last time I checked ni zaidi ya 138k. Just because uliugua korona kisha "ukapona" doesn't mean you are immune to it Kwa sababu a lot is not known about both the virus and the pandemic.

Badala ya kufanya mzaha kwa kuwakebehi wapinzani ambao kosa lao pekee lilikuwa ku-raise public awareness kuhusu gonjwa hilo, ungejihangaisha kuelewa nini kinaendelea Tz. Mtafute daktari asiyejihusisha na siasa akuelikishe. Kuyaangalia mambo muhimu kwa taifa letu kwa miwani ya mbao ya itikadi za siasa na UKABILA ni ugonjwa hatari zaidi ya korona.
Hiyo idadi yako ya 138K mimi nina mashaka nayo. Siiamini kivile.

Hiyo ni kwa sababu hiyo korona huko Marekani inatumiwa kama silaha ya kisiasa dhidi ya Rais Trump.

Isitoshe, kuna utata kiasi kuhusu hao wanaokufa. Inasemekana wengi wao wanakufa kwa comorbidities. Hawafi kwa sababu ya korona pekee.

Unakuta mtu ana terminal illness. Ikitokea amekufa na wakampima kuona kama ana traces za COVID, basi wanasajili kifo chake kuwa kimesababishwa na huyo kirusi.

Kwa hiyo, hiyo idadi ya 138K wala si ya kuiamini kivile.

Kwa Marekani, hii COVID itaisha tarehe 3, Novemba.

Vuta subira ujionee....
 
Mkuu wiki hii nimeumwa shingo [emoji23][emoji23][emoji23] lol. Ujumbe wako umenistua maana nilikuwa najiuliza shingo hii vipi siku ya nne haipoi
Pole sana mkuu...

Ukiona na mbavu zinabana pamoja na mgongo kuanzia kwenye mabega hadi maeneo ya kifua vinauma usiogope.!

Piga dozi ya mseto na NYUNGU YA MSHANA

Kwisha habari yake!
 
Back
Top Bottom