Ulichosema ni kweli, lakini wabongo wengi tunamisinterpret kati ya matani na kujidharaulisha. Matani hayana personality, mtu yeyote bila kujali hadhi yake, anaweza kufanya utani wakati na mahali panapostahili. Ndio maana hata waheshimiwa wabunge wakati fulani wanataniana. Matani yana umuhimu wake ikiwa ni pamoja na kujiburudisha, kurelease tension, nk. Hata rais mstaafu Donald Trump, anataniana na rais Joe Baiden. Tatizo letu sisi wabongo tukitaka kumchafua au kumharibia mtu utu au heshima yake katika jamii, tunabatilisha mambo; yaani jambo linaloonekana kawaida wakifanya watu wengine, lakini akifanya mtu usiyempenda, jambo hilohilo linageuka kuwa kituko!