Kili Marathon kugawa barakoa kwenye Mbio zitakazofanyika mwaka huu

Kili Marathon kugawa barakoa kwenye Mbio zitakazofanyika mwaka huu

Watu wana kojorea pazuri piga picha hapo awe uchi wa munyama.
Naona jamaa hapo juu amesahau kwenda kwake karibu atadondosha mfuko na mwanariadha mwingine hapo chini ameshika kiuno badala ya kuendelea na jogging!
 
Marathon na barakoa wapi na wapi
Wabongo kwa kulazimisha mambo
Juzi nandy koffie mmelazimisha
Bado hali si shwar mnalazimisha

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Sijapata Logic ya kuvaa barakoa ambayo imeziba pua na mdomo huku ukiwa una trot/Jogging/ Kukimbia... vitendo ambavyo vinahusisha utoaji na uingizaji wa hewa nyingi kupitia mdomo,pua na mapafu

Anyways nisiwe msemaji sana.....

Tuendelee kujifukiza, barakoa, sanitizer, social distance, kuepuka misongamano na kutumia tiba asili

Au nasema uongo ndugu zangu? Mzaha sio mzaha...
Watu wa ajabu sana wao wanangalia pesa tu
Hawana tofauti na wasanii wa bongo fleva

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Maajabu hayotoisha..unavaaje barakoa huku unakimbia.
Wakati wa kukimbia unahitaji oxygen nyingi sana ,sasa unavalishwa barakoa ambayo itakufanya upumue kwa shida.
Nimeliona Sana hili,mtu yuko jogging na barakoa au yuko mwenyewe tu kwenye gari amevaa barakoa.
Kazi kweli kweli.
 
Meya alisema mkoa wake ni salama so kikaoni hataki kuona barakoa kwani vipi tena?
 
Kuna wajinga watakimbia kweli na barakoa ili kumfurahisha jiwe.
 
Si wahairishe tu?
Utakimbiaje na Mask?
Wataanza kuanguka kama kuku sasa.Maana hewa zitawaishia naturally tu.

Na kudanga je
Hizo marathon ni starehe tu na kudangiana
 
Nchi hii watu sjui akili zao wameziweka wapi
Utakimbiaje hku umevaa barakoa ni sawa umwambie diver azame kina kirefu bila ya kutumia oxygen
Kingine tuko kwenye hatari lkn utaona sjui nandy anafanya show mara tigo fiesta
Mijitu migumu kuelewaa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Ni jambo la kushangaza sana, watu wanapenda sana Pesa kuliko uhai wa watu.... Misongamano watu hawavai barakoa, hawachukui tahadhari

Ifike wakati mamlaka husika ivalie njuga suala hili kabla ya maafa zaidi

Hii mikusanyiko isiyokuwa na ulazima wowote (inayokutanisha watu wengi) ifutwe
 
Wanataka wauwe watu, sasa ukivaa barakoa halafu unakimbia si utakosa hewa kabisa
Mtoa mada hajafafanua vizuri.matangazo yao ni kuvaa barakoa kabla ya mbio .wakati wa kukimbia wanashauri watu wasivae
 
moto unawaka huku, njooni mkimbie na zirael
 
Ni jambo la kushangaza sana, watu wanapenda sana Pesa kuliko uhai wa watu.... Misongamano watu hawavai barakoa, hawachukui tahadhari

Ifike wakati mamlaka husika ivalie njuga suala hili kabla ya maafa zaidi

Hii mikusanyiko isiyokuwa na ulazima wowote (inayokutanisha watu wengi) ifutwe
Watu wenyewe wanavuta kila kukicha

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
hizi ndio taasisi ambazo zinaungwa mkono na wapinzani wa jf na kule twitter[emoji16][emoji16][emoji16].

aliyetoa hili wazo anaumwa corona ya kichwani.
 
Kampuni ya Kilimanjaro Marathon inayoendesha Mbio maarufu za kila mwaka za “Kili Marathon” zinazofanyika Mkoani Kilimanjaro imetangaza kuwa kutakuwa na zoezi la ugawaji wa barakoa kabla na baada ya mbio kwa wakimbiaji wote wa mbio fupi na ndefu.

Vilevile wameeleza kuwa kutakuwa na kamati maalumu itakayokuwa inagawa vitakasa mikono kwa washiriki kwenye vituo maalumu, njiani mpaka mwisho wa mbio, na uwanjani kwa siku nzima ya mashindano. Watoa huduma wote katika vituo vya maji pamoja na uwanjani watavaa barakoa, gloves, aprons na watahakikisha wanatakasa mikono mara kwa mara muda wote wa mashindano

Wamesema hatua hiyo ni kutokana na wingi wa watu watakaoshiriki katika tukio hilo litakalofanyika Februari 28, 2021 Mjini Moshi. Mbio hizi zinafanyika huku kukiwa na madai ya COVID19 kuenea mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro amekanusha madai hayo na kusema mkoa uko salama na magari ya maiti yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ni kutoka mikoa mingine.

Pia soma

Kili Marathoni huhusisha ukimbiaji wa mbio fupi/nusu (half marathon) kwa umbali wa Kilomita 21.1 na ndefu/kamili kwa urefu wa Kilomita 42.2.
Meya wa hilo eneo hataki barakoa
 
Nchi hii watu sjui akili zao wameziweka wapi
Utakimbiaje hku umevaa barakoa ni sawa umwambie diver azame kina kirefu bila ya kutumia oxygen
Kingine tuko kwenye hatari lkn utaona sjui nandy anafanya show mara tigo fiesta
Mijitu migumu kuelewaa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Wengi wetu ni kama mang'ombe hatuendi mpaka fimbo(ngoja liwakute jambo ndowataelewa)

Kingsmann
 
Back
Top Bottom