Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Sisi wahafidhina tumesikitishwa sana na matokeo ya jana ambapo Leo Messi na timu yao Barcelona imewapeleka Liverpool fainali kwa uzembe wao.
Matatizo yote yalianzia mechi ya kwanza, wakati wa dakika za mwisho pale Dembele alipokosa goli la wazi kabisa akiwa kabaki na golikipa Alisson Becker.
Liverpool itatoka kapa kwenye fainali kwa kile kinachoitwa "The Klopp Curse" yaani laana ya Klopp ambaye ni kocha wa Liverpool.
Kwa miaka ya karibuni huyu ndiye kocha aliyeingia fainali nyingi za vikombe lakini anaishia kufungwa, hii "The Klopp Curse" imekuwa ikifanya kazi tangu akiwa Dorrmund.
Tayari ameshapoteza fainali kubwa mbili za Uefa, moja mwaka jana dhidi ya Real Madrid na nyingine mwaka 2013 dhidi ya Bayern Munich.
Mimi naamini baada ya filimbi ya mwisho katika mchezo wa Fainali pale Wanda Metropolitano, Liverpool itakuwa katika upande wa waliopoteza, huku Ajax au Spurs ambaye mmoja wapo ataingia Fainali watakuwa wanashangilia na kwenda kuvaa medali za Uefa.
Siku zote muda ni mwalimu mzuri!