Kilichomharibia VUNJABEI ni hiki hapa

Kilichomharibia VUNJABEI ni hiki hapa

Shida kubwa ya vunja bei anataka kuvuna tu hataki kurudisha kwa jamii sikumbuki ni lini huyu jamaa katoa misaada sehemu Fulani ajifunze kwa waarabu wanaotoa kila siku lakini kila siku wanazidi kuongeza mali
Atakuwa amesoma huu ujumbe pia...
 
Juzi kuna memba aliweka uzi kuwashirikisha wanajukwaa kuwa Vunjabei anahisi kama anaenda kufilisika ila hakuwa na uhakika yote ni sababu ameona maduka yake kama yanapumulia Gesi na mengine kufungwa mikoani huko wengine wanadai hadi zile plate no za majina ameondoa kuepuka Garama uchumi hauruhusu.

Ila kwakuwa mimi ni mkongwe wa kariakoo na Biashara ya mavazi naifaham vizuri basi fuatilieni huu uzi ili ambo mpo kwenye biashara hasa zile biashara ambazo zipo on Fire zinawalipa muwe makini maana biashara kupanda na kushuka ukikosea kitu tu ni Dakika moja na kupanda tena ni mtihani.

Ishu ipo hivi

Vunja ni moja ya vijana wa mwanzo kabisa hapa Tz kulijua soko la China ambalo limewaletea utajiri mkubwa vijana wengi wa Tanzania, Vijana wa mwazo kabisa hapa Tanzania kwenda China kubeba mzigo na kuja kupata pesa nyingi hapa Tanzania. Fredi alikuwa ni mmoja wapo sijasema kwamba ni wa kwanza ila kati ya watu wa mwanzo kufaidika na mizigo ya china humtoi kwenye list, na enzi hizo kwenda china hapo kariakoo walikuwa ni madon wachache ambao walikuwa wanayajua machimbo china wanabeba mzigo wanakuja kuwauzia na wafanyabiashara wengine.

Hata moja ya Stori za fredi na vyombo vya habari aliwahi kusema kuwa alianza biasgara na kigoli kidogo vile vifrem vya uchochoroni kariakoo hapo tena alikuwa wanashare mtaji na Rafiki yake ndio wakajichanga ikabidi mmoja wapo aende china akirudi wakiuza mzigo wagawane na kweli fredi mara ya kwanza anaenda China tu kurudi kumwaga mzigo hapo kariakoo ukaisha chap hapo ndio akasanuka kuwa china pesa ipo kipindi hicho china waliokuwa wanapajua ni wachache hapo ndio ukawa mwanzo wa fredi kupiga pesa na kufungua maduka makubwa sinza na sehem nyingine.

Sasa kilichomponza Fredi ni mdomo na kupenda kutoa siri yaani jamaa alivunja Sheria matajiri kamwe ukitaka kuwa tajiri usitoe siri za mafanikio yako kwa public ndio maana Gsm Akiuambiwa tumotivate tuwe kama ww aasema yanga bingwa yaani matajiri huwa hawatoi code ya walipopitia hadi sehem wanapobeba mzigo huwa ni siri, hata hapo kariakoo mtu hawezi kukupa code ni wapi anatoa mzigo huko China ili auze mwenyewe ukijifanya chaumbea tu utafunga Fremu.

Sasa baada ya Fredi kuwamotivate vijana kuwa China pesa ipo matokeo yake vijna wakamskiliza na wakaanza kufanya Research China wakayagundua machimbo ya nguo na viatu vya bei kitonga wakaanza kwenda wenyewe hata wale aliokuwa anawauzia wakawa wanaufuata mzigo wenyewe huko china mwisho wa siku akaengeneza upinzani mkubwa ambao ni chanzo cha kumfikisha hapo alipo.

Na kulikuwa na kesi nyingi za kushusha nguo zilizochini ya kiwango hakufanya reserch kuwa watu wanataka vitu vyenye quality mwisho wa siku vijana wakamletea upinzani wanaleta jeans zenye viwango wanashusha kkoo hapo kwa bei ile ile akaanza kupoteza soko.

Kwa sasa hapo kariakoo kuna vijana ni Madon vunjabei haingii ndani sema vijana wengi hapo kariakoo ni wasiri na hawana kelele ila wana pesa na wanauza balaa na mzigo wanaubeba china sema wamewin sababu ya kushusha jeans na tshrts kali zenye quality wakishusha utakuta watu wanagombania nusu kuuwana.

Kitu kingine ukijifanya wewe ni Tajiri ndio unawakaribisha TRA wakukamue vizuri kuwa msiri sana hata Diamond platnumz hapa juzi alijitamba anaingiza Mabilioni ndio Tra wakamtembelea kumjulia hali nadhani mliona alivyobanwa kidogo tu namna alivyotoa mluzi kwa kilio kuwa wanataka kumfilisi

Soma Pia: Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

Wafanya biashara wa kariakoo wana siri sio mchezo,ukiwauliza wanatoa wapi huo mzigo hawatokaa wakupe hiyo siri ila Fredi umbea kujimwambafai na kuwaeleza watu michongo yake ndio ni sababu moja wapo inayo muharibia, kama unabiashara yako kamwe usitoe siri za biashara kwa watu huu uzi utakuja kuupitia tena kuwa msiri na mkimya.

Na kwa kumalizia kabisa kuna watu wanasema jamaa hajafulia ila kaamia kwenye uuzaji wa madawa ila hata huko kwenye pharmacy asipouchunga mdomo wake na kukaa kimya, akiendelea kutoa siri za kambi atawakaribisha wapinzani ambao watamsumbua, Utajiri unahitaji utulivu na ukimya wewe jifanye muongeaji utaonyeshwa....
Vunja bei ya miaka mi5 iliyopita na sahivi ni tofauti sana yaani Kila nikinunua nguo vunja bei lazima nikivaa mwezi mmoja tu na kuzifua zinapauka vibaya,vunja bei kaishiwa Kila biashara na nyakati zake aswa iyo ya nguo ahamie kwenye manufacturing na sio trading Tena,ili uwe tajiri lazima uwe kwenye manufacturing na sio izo biashara za maduka kwa kulangua nguo china za low quality ambazo Kila mtu anaweza fanya,Vunga bei na African boy ya Jux sijui nani kaanza ila Jux anajitambua kuliko Fred.
 
Biahara kama nguo kubakia kwenye top ngumu sana walikuwa wakina zizzuou pamba kali,walikuwepo wakina Hussein pamba kali wote chali saiv sema yeye mdomo mwingi

Hapa shida inaweza kuwaga nini mkuu kwenye hii sector ya nguo maane kwel hao wote wamepotea kabisa
 
Hussein Pamba kali, Robbie one, zizzou fashion, Chidi Mapenzi hao woote walikuwa wanauza nguo kutoka China na walikuwa na majina Ila sasa hivi hata hawasikiki tena sijui biashara ya nguo Ina shida gani
 
Back
Top Bottom