Kilichomkuta rafiki yangu kazini kwake

Kilichomkuta rafiki yangu kazini kwake

Uone mpenz wako ana chart na danga jipyaaa na ukasoma notes zote unadhani utakuwa ktk hali ya kawaida
Huyo jamaa ni mshamba sana,kama mim ndiyo ningekuwa bosi wake hapo hapo ningempa barua ya onyo kali anatumia rasilimali zangu vibaya(vifaa na umeme)
Au namtimua tu ili akaombe kazi vizuri akiwa hana kazi
 
Awe na wasiwasi kama;
  • Barua ya mambo inatakiwa kupitishwa na Mwajiri wake huyo kama ilivyo serikalini.
  • Kama huyo mwajiri wa sasa atatakiwa kutoa maoni yake kwa mwajiri mpya( anaweza kumsagia kunguni).
Kama hayo hapo juu jayapo,Hana jaja ya kuwa na wasiwasi,aendelee kuomba.
 
Kwanza uwa mnajiona kama vile Jf mabosi wenu hawawezi kuwa members umu?
 
Kwa jinsi ulivyomulezea huyo rafiki yako inaonesha kabisa Huyo jamaa mwenyewe ndio wewe, lakini hamna baya hapo labda boss wako tu awe na roho ya mbaya
Mwamba afadhali umerudisha Avatar picha yako. Ila shem alizingua kichiz kukubania kuweka avatar picha.
 
Rafiki yangu mmoja kanipa kisa chake kaomba nimshauri nimemwambia anipe muda nikakumbuka wazee wa busara wako hapa nitashare kisa chake ili nipate hoja imara za kumshauri.

Rafiki yangu huyu anafanya kazi katika kampuni Z. Juzi akiwa kazini kwake ambako wanaingia saa moja asubuhi na kutoka saa moja na nusu jioni. Akiwa na kompyuta ya kazini kwao aliona tangazo la kazi sehemu basi bhana akataka kutuma maombi ya kazi maana aliona huko wanamaslahi bora kuliko alipo.

Akiwa katika harakati za kuandika barua ya kuomba kazi kampuni B, mwajiri wake wa kampuni Z si akamfuma akamwambia tu naona unafanya ma application ya kazi, jamaa kwa hofu na mshtuko akakaa kimya😁

Sasa jamaa yangu huyu hana raha tena maana mwajiri wake wa kampuni Z anaonekana kummind sana sasa hivi hata akimsalimia hajibiwi, kiufupi jamaa yangu kaonekana kama msaliti anasema boss wake hamchangamkii tena kama mwanzoni hapa anauliza aache kazi ama afanyaje.

Napokea mawazo wakuu ili nikampe namna ya kushinda hiyo pressure😁
Mwambie "mind your own business" yaani amwone huyo boss kama hamwoni!
 
Kwani mkisemaga ni nyinyi kuna shida gani? Yan ishu ya rafiki yako uje uombe ushauri JF?
 
Rafiki yangu mmoja kanipa kisa chake kaomba nimshauri nimemwambia anipe muda nikakumbuka wazee wa busara wako hapa nitashare kisa chake ili nipate hoja imara za kumshauri.

Rafiki yangu huyu anafanya kazi katika kampuni Z. Juzi akiwa kazini kwake ambako wanaingia saa moja asubuhi na kutoka saa moja na nusu jioni. Akiwa na kompyuta ya kazini kwao aliona tangazo la kazi sehemu basi bhana akataka kutuma maombi ya kazi maana aliona huko wanamaslahi bora kuliko alipo.

Akiwa katika harakati za kuandika barua ya kuomba kazi kampuni B, mwajiri wake wa kampuni Z si akamfuma akamwambia tu naona unafanya ma application ya kazi, jamaa kwa hofu na mshtuko akakaa kimya😁

Sasa jamaa yangu huyu hana raha tena maana mwajiri wake wa kampuni Z anaonekana kummind sana sasa hivi hata akimsalimia hajibiwi, kiufupi jamaa yangu kaonekana kama msaliti anasema boss wake hamchangamkii tena kama mwanzoni hapa anauliza aache kazi ama afanyaje.

Napokea mawazo wakuu ili nikampe namna ya kushinda hiyo pressure😁
Jamaa yako hana kosa lolote na yupo hapo kwa ajili ya kuitafuta kesho yake na kama ingekuwa boss hamkubali kiutendaji kazini nafikiri angeshamtafutia vijisababu kwani inaonekana hiyo ni kampuni binafsi thats why hata wanawafanyisha masaa mengi.
 
Sasa hapa jamaa aishije maana ishaonekana ana mpango wa kuondoka mbaya zaidi boss wake kajua na hajapata bado sehemu ya kwenda
Aache kujipa pressure za bure anaondoka kwenda wapi? Yeye akaze buti afanye kazi mpaka mwajili ajiulize mara mbilimbili na wakati huo huo akiendelea kutafuta fursa kwingine.
 
Makosa ya kipuuzi alifanya kwa kutaka dezo ya kompyuta ya ofisi.Amegeuka kua kama muhalifu aliyeacha ushahidi eneo la tukio.An alibi!
Huyo boss ni masikini kifikra kama wajinga wengine, kutumia computer ya ofisi ka mind kihivyo sasa wangekutana naye mitaani huko akipeleka hizo barua zake kwa gari ya ofisi ingekuwaje?? Angemfungulia jarada la uhujumu uchumi
 
Siku moja nliaga kazini kwenda kwenye matatizo binafsi ya kifamilia ,kama ilivyo sheria za kazi inaruhusiwa kumbe nmetarget kuiwahi imterview ya shirika moja la kimataifa huko unalipwa kwa umate umate wa dollars 😂, bana kufika kwenye oral interview na mahojiano pap boss wqngu huyu hapa yuko kwenye panel ya wasaili !!, Nilifanya lakini hajawahi niuliza kitu mpaka sasa na maisha yanaendelea , uwoga hautasaidia Kumbukeni ,You have family to feed ,and not community and bosses to impress!
Automatically huyo BOSS wako apewe maua yake, yuko vizuri thats why hata hayo mashirika ya kimataifa yamamshirikisha kwenye interview zao. Na amini pasi na shaka kuwa kama ungekizi vigezo asingekubania kupata nafasi hapo.
 
Rafiki yangu mmoja kanipa kisa chake kaomba nimshauri nimemwambia anipe muda nikakumbuka wazee wa busara wako hapa nitashare kisa chake ili nipate hoja imara za kumshauri.

Rafiki yangu huyu anafanya kazi katika kampuni Z. Juzi akiwa kazini kwake ambako wanaingia saa moja asubuhi na kutoka saa moja na nusu jioni. Akiwa na kompyuta ya kazini kwao aliona tangazo la kazi sehemu basi bhana akataka kutuma maombi ya kazi maana aliona huko wanamaslahi bora kuliko alipo.

Akiwa katika harakati za kuandika barua ya kuomba kazi kampuni B, mwajiri wake wa kampuni Z si akamfuma akamwambia tu naona unafanya ma application ya kazi, jamaa kwa hofu na mshtuko akakaa kimya😁

Sasa jamaa yangu huyu hana raha tena maana mwajiri wake wa kampuni Z anaonekana kummind sana sasa hivi hata akimsalimia hajibiwi, kiufupi jamaa yangu kaonekana kama msaliti anasema boss wake hamchangamkii tena kama mwanzoni hapa anauliza aache kazi ama afanyaje.

Napokea mawazo wakuu ili nikampe namna ya kushinda hiyo pressure😁
Unatumia vipi muda na kompyuta za kampuni moja kufanyia maombi kwenye kampuni nyingine?

Unaelewa kuwa mwenye kampuni anaruhusiwa ku monitor computer zake za kazini?

Tumia computer yako na muda wako kufanya hizo application kivyako nje ya sehemu ya kazi.
 
Shida iko wapi...? Amalizie maombi kwanza akipata kazi aende ila aondoke kwa wema kabisa na akikosa abaki asubir kufukuzwa kama kweli kamaindiwa kikubwa asibadili mienendo yake ya uchapakaz Boss hawez kumtosa ikiwa ni productive.
 
Back
Top Bottom