Tetesi: Kilichomponza Diamond ni Sakata la ATCL

Tupe ushahidi kama kweli aliwahi airport?
 
Tupe ushahidi kama kweli aliwahi airport?
Mbona amekuambia, kwamba katika watu aliofika nao wakati mmoja airport kuna waliochukuliwa, pale walipoambiwa tuna nafasi za watu wawili tu kwenye kundi lenu?

Kukiwa na overbooking mnaweza mkawa watano mmefika wakati mmoja akaondoka mmoja tu kati yenu
 
Kwani yule Konki master anasemaje??
 
Labda ndiyo waliowahi una ushahidi walifika wote pamoja?
 
Kaisha ota mapembe huyo.......kakua.
 
Mkuu mimi nimekuelewa na umeandika kitu nilichotaka kuandika.

Kuna mambo Diamond anafanya ninasema labda ni sababu ya kutokusoma lakini hapana wapo wasiosoma na wanaweza kuchambua baya na zuri.

Watu wanakosewa sana kwenye taasisi mbali mbali ukipeleka malalamika tena kwa mtu maarufu kama yeye lazima a ange respond na ku apologise sio kuliharibia shirika la umma wakati serikali ndio inapambana kuliweka sehemu nzuri.

Tena Diamond aombe BASATa iwe imeamua yenyewe lakini kama ndio wameelekezwa kutoka juu basi mengi yatamuandama na hakuna wa kupambana na mamlaka.
 
Ahsante mkuu " nifuraha sana " kuona unaongea jambo halafu watu wakalipokea kwa mapokeo chanya " inatia hamasa sana yakujifunza zaidi .. ubarikiwe
 
Kwa hiyo Atcl ukifanya booking ukalipa unawai kuzibiti siti kwa kuwai kufika!!!.so akuna tofauti na mabasi?
 
Siko hapa kuongelea usanii wa Diamond na kufungiwa kwake kwa sababu mimi sio mdau wa miziki ya duniani BALI nataka niiongelee ATCL ambayo imetajwa kwenye mada hii.

Hakuna mtu/kitu kisichokuwa na mapungufu; Kwa hiyo yapo pia mapungufu kadhaa kwa ATCL, LAKINI hayo mapungufu hayawezi kuondoa MAZURI mengi waliyoyaonyesha tangu uhuishaji wa shirika uanze.

Kwa mfano;

1. Nauli rafiki - Last time nilipanda ATCL (Dar - Mza) kwa Tshs. 254K kwenda na kurudi tena ile Dreamliner. Fastjet waliniambia nitoe 365K, wakati Precision Air is even more expensive.

2. Wahudumu wa ATCL (wa ndani ya ndege) - Walikuwa rafiki na walionyesha ushirikiano. Changamoto iko kwa watumishi wa mamlaka ya ndege kwa ujumla (sio wote), na taasisi zingine pale (sihitaji kuzitaja) ambao huwa na lugha za hovyo.

Ila, ukiongelea wahudumu wa ATCL as ATCL hasa wale wa ndani ya ndege niliwapenda sana kwa huduma zao, japo wapo watumishi wasio na huduma nzuri hasa wale wa ukatishaji tiketi/check in (sio wote) na wajirekebishe.

3. Huduma kwa wateja - Hata, nilipopiga ile namba yao ya customer care walirespond vyema na kunipa majibu ya maswali niliyowauliza.

4. Muda wa kusafiri - Muda wa kusafiri umepungua hadi dak. 65 kwa ndege kubwa (Dar - Mza) ... Yaani hata usiku naweza kusafiri kwa sasa nikiamini nitafika.

Changamoto kadhaa zipo, ambazo huyakumbuka mashirika mengine duniani kama vile kuchelewa kuondoka/kufika kutegemeana na issue fulani.

Ila kwa ujumla naona ATCL ime IMPROVE sana, na tusiwavunje moyo bali tuwasapoti. Kosa la mtu mmoja/kikundi lisiwe sababu ya kulisulubisha shirika zima.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…