Kilichomponza Magufuli: Hakuchukua hatua kwa waliohusika na mauaji, watekaji na waliopotezwa

Status
Not open for further replies.
Umenena vema,hili jambo LA watu wasiojulikana limeleta taharuki kwa sababu watanzania hatukuyazoea haya. Hata akifanikiwa kushinda ni bora akashughulikia jambo hill haraka iwezekanavyo
Kama Mungu atampa nafasi tena, basi kulishughulikia kwake hili ni kwa njia ya TOBA tu, baasi..

Hakuna short - cut way.

Aombe msamaha wa wazi mbele za Mungu na wanadamu. Aseme, mimi John Pombe Magufuli nimekosa mbele za Mungu na binadamu wenzangu, nisamehe Mungu..

Yeye hatakuwa wa kwanza. Mfalme Hezekia alijishusha kwa namna hii. Ilikuwa auwawe, lakini alipotubu, Mungu alimsamehe na kumpa maisha tena..

Mungu ni mwaminifu na wa haki, atasamehe na atampa nafasi nyingine tena kama atatubu..

Kinyume chake, hakuna namna. Mshahara wa maovu, dhambi ni mauti.. Bwana Mungu wa majeshi muumba wa mbingu na nchi asema...!!
 
Nchi hii ukiwa na mawazo tofauti na watawala thamani yako inaisha!!
 
JPM atashinda kwa 55% mtashangaa... kisa wapinzani wengi awapiga jura kwa sababu awana kitambulisho cha wapiga kura.
Hapana mteteeni kwenye mambo mengine kama sijui kujenga uwanja wa ndege Chato, kula rambirambi za wahanga wa tetemeko, kuhamishia wanyama kwao nk lakini hili la utekaji na mauaji, mwacheni afe kifo chake.

Kweli kwa huu ukatili hafai kabisa kupewa ofisi yoyote katika nchi hata kuwa desk officer tu hafai.
 
 
HII DHAMBI HUFANYWA NA WATU WACHACHE SANA,NI DHAMBI MBAYA SANA
 
Vitu viwili tu.."mauaji na kupotea watu chini ya mamlaka yake Bila wahusika kutiwa nguvu ni....pili uuaji wa democracy kwa kutumia human slavely!! Hivi vitamtesa maisha yote. Mimi ningekua kiongozi dhambi kubwa kweny mamlaka yangu ni hzo.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo lissu alitoroka kazini??? Aseee watu mtakufa vibaya nyinyi
Hajakataa kumchangia damu,sasa damu ingepelekwaje nairobi?,kumwombea mtu mmoja mmoja haikuzuiwa,kilichokatazwa ni mikusanyiko,
Alivuliwa ubunge na ndugai sababu alitoroka kazini,
Kama kumtibia,si chadema walikuwa na hela na zilitosha?
 
Na huu ndio ukweli wenyewe
 
Magufuli alianza vizuri hasa, Maneno aliyoyatamka Singida mwaka 2017 kwamba ikifika 2020 hakutakuwa na upinzani, niliamini kabisa upinzani hautakuwepo kwa sababu ya utendaji kazi mzuri wa rais na serikali yake, niliamini kabisa kwamba huyu jamaa ni mtu mwema hasa, anamjua Mungu, ana hofu ya Mungu, kwake anapenda maendeleo ya nchi yake na siyo maendeleo binafsi,
Lakini mambo yalianza kubadilika, Wasiojulikana wakazidi kufanya matukio ya ajabu sana dhidi ya wananchi waliompigia kura, Wakosoaji wote wakadhibitiwa, Vyombo vya habari vikatungiwa sheria ya kuvithibiti, TBC ikageuka kuwa kituo cha propaganda, Bunge likawa rubber stamp ya kila kitu cha serikali, Bado hakutosheka, Akawanyima ongezeko la mishahara wafanyakazi wote tena kwa jeuri ya kujenga bwawa la umeme na kununua ndege, akafukuza wanafunzi wa UDOM kwa kuwaita Vilaza, Akatunga sheria ya kutoshitakiwa yeye mwenyewe, Spika wa bunge, Naibu speaker, pamoja na jaji, Bado hakutosha akatunga sheria kuvithibiti vyama vya siasa, Akaanza kuviingilia vyama vya kitaaluma mfano TLS ili visimkosoe, Sasa Nikiyatazama haya yote sioni uzuri hata kidogo wa huyu mtu. Cha kufanya ni twende na Mitano Kwanza
 
Hilo linawaumiza sana watanzania kuliko anavyodhani yeye

Amefanya watanzania wamchukulie ni katili, asiyejali na asiye na utu

Kingine ni kutojali wasomi waliokosa ajira tangu 2015 na kutopandisha madaraja na mishahara ya watumishi wa umma.
Nafikiri hajui kama mauaji, utekaji na mambo mengine yanawaumiza watanzania. naamini kwa dhati kabisa ndani ya CCM kuna watu great minds, with rational thinking lakn hawajafurahishwa na matukio hayo ya utekaji,kujeruhi, na kuuwawa. hawana budi na wanaogopa kuyasema wakiwa ndani ya chama chao.
 
...
 
Umenena vema,hili jambo LA watu wasiojulikana limeleta taharuki kwa sababu watanzania hatukuyazoea haya. Hata akifanikiwa kushinda ni bora akashughulikia jambo hill haraka iwezekanavyo

Andiko bora kabisa hili................

Hongera sana Mkuu
Wallah , this is one of the scholarly article of the year. Very informative and educational. Keep it up brother.
 
Rais Magufuli ndiye Rais. Wengine wanapoteza muda tu. Nchi hii inahitaji viongozi shupavu na wazalendo hasa, wenye uchungu hasa na taifa lao sio mawakala na vibaraka wa mabeberu.
Umetahiriwa wewe? Unanuka ushuzi
 
A country is not a company, in other words if you give a shield to unknown criminals you become a part of it
 
Nakubaliana na wewe Kuna move moja Mh. Raisi akichukua ita mwongezea Kura mpaka atashangaa.

Mimi Hadi Kampeni zinaanza Kura yangu ilikua iende CCM. Bila kujali ahadi nyingi za CCM ambazo hazijatekelezwa.

Ila NEC ndio walianza kuharibu kwa kuengua Wagombea wa Upinzani tu. Niliona ni nuonevu.
Hata hivyo Kampeni zilipoanza na vyombo vya usalama kuwa neutral kwa wagombea na kulinda na kuheshimu wagombea woote ilinirudishia matumaini na nikasema wacha nisubiri Kampeni ziishe ndio niamue kulingana na ntakavyoshawishiwa.

Sasa sijui wanaoishauri NEC au Polisi au CCM ni Nani. Ila vitendo wanavyofanyiwa Upinzani Hasa CHADEMA. vinanikatisha tamaa. Na Cha Ajabu NEC or Serikali haisemi Chochote inaonyehsa waazi Kuna uonevu wa ushirikianao na CCM. Maana wao ndio watawala kwa Sasa.

Sasa Kama Raisi hata akikemea tu na Kuamuru waache wagombea wote wafanye Kampeni bila kubughudhiwa. Ita waaminisha wengi kwamba yeye Ni Raisi wa wanyonge na mpenda haki, na mcha Mungu.
Na mi nitakua mmoja wa watu wa kwanza kumpa Kura yangu ya Uraisi. Hata Kama sita wapa CCM ya Ubunge na udiwani.

Hivyo naamini kukemea kutamuongezea Kura hata Kama sio za Kishindo Bali za kutosheleza kumpa ushindi.

Binadamu Ni wepesi wa kusahau na kusamehe. Pia Ni wepesi wa kubadilika Kama ukiwaaminisha.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…