Kilichomponza Makonda ndicho hicho kingemponza Magufuli

KILICHOMPONZA MAKONDA NDICHO KINGEMPONZA MAGUFULI.

Na, Robert Heriel

Licha ya kuwa watu hawa kwa sehemu kubwa nawakubali na kuwapigia chapuo, lakini kamwe sitoacha kusema ukweli kuwa kinachowaponza ni kitu kimoja, ambacho kinafanya wasikubalike kwa wengi.

Makonda ni kijana mchapakazi, mbunifu, mthubutu na mwenye ujasiri wa kipekee. Hivyo hivyo kwa Mhe. Rais, John Pombe Magufuli.

Hakuna asiyetambua kazi za Makonda, hakuna asiyetambua harakati zake, kila mtu anamkubali kwa kazi zake, halikadhalika na Magufuli, hakuna asiyemkubali kwa kazi azifanyazo lakini nini kingemponza?

Kilichomponza Makonda ndicho hicho hicho ambacho kingemponza Mhe. Rais kama angetokea mtu akachukua fomu ndani ya chama. Nilikuwa nawaambia rafiki zangu kuwa endapo angetokea mtu akachukua fomu ya kugombea Urais akachuana na Magufuli basi ni wazi kabisa Magufuli angeshindwa mapema sana.

Nini kingemponza Magufuli ambacho kimemmaliza Makonda katika siku ya jana. Huo ndio mjadala wetu kwa siku ya leo.

Katika uongozi unaweza ukafanya kila kitu, ukaleta maendeleo, ukaongeza mishahara, ukafanya elimu kuwa bure, huduma za afya bure, yaani ukaifanya nchi kama Peponi lakini kama hutautawala ulimi wako basi huna ulilolifanya, hakuna atakayekupenda, hakuna atakayejali mambo uliyoyafanya.

Ulimi ni kiungo kidogo kinachoendesha dunia, huweza kuharibu, kubomoa lakini pia huweza kujenga na kuleta amani.

Hata nyumbani, Mume akiwa na pesa na anahudumia familia yake lakini kama hatakuwa na kauli nzuri ni wazi Mke wake na watoto hawatampenda. Lakini Mtu mwenye ulimi mzuri, yaani kauli njema hata kama hatekelezi majukumu yake bado mke wake atampenda na kumheshimu halikadhalika na watoto.

Kheri yule mwenye Ulime mwema na hapo hapo anauwezo wa kuhudumia familia yake. Huyo anabahati.

Kilichomponza Mhe. Makonda licha ya kuwa nilikuwa natamani apewe nafasi ya kuongoza ni ulimi wake. Makonda anashindwa kuelewa kuwa Maneno yanaishi, ulichosema leo kitaishi hata siku ujapokufa bado maneno yako yataishi. Ni vizuri watu kuchunga ndimi zao hasa viongozi wakubwa.

Ni busara kukaa kimya kuliko kuteleza katika ulimi, ni hatari sana. Watu hawasahau na hawatajua kuwa ulitania au uliteleza.

Makonda katika hili naamini atajirekebisha, na itakuwa amejifunza kuwa uongozi hautoshi pekeake bali kuishi na watu kwa upendo, hasa kwenye mdomo.

Kwa upande wa Mhe. Rais Magufuli, asije akadhani watu wanasahau maneno yake, ukisema umesema, na watu kamwe hawasahau maneno makali yaliyowaumiza. Magufuli anaweza kuwa amejenga barabara, kanunua ndege, kafanya kila kitu lakini maneno tuu yakamponza.

Naamini Mhe. Rais ni kiongozi mzuri ambaye kama binadamu wengine hupokea maonyo, na kubadilika. Katika hili ninaushahidi kuhusu mabadiliko ya kitabia ya Mhe. Rais pale anapokosolewa, maana mimi pia niliwahi kumkosoa kipindi cha nyuma akiwa ndio anachukua nchi kuhusiana na kauli zake, nilishawahi kuongelea habari za Tetemeko la Kagera, kuwakashfu viongozi wenzake kwa maneno makali kama kuwaita wapumbavu mbele za halaiki, kuwaambia wafanyakazi waache kazi kama mshahara wanauona ni mdogo, miongoni mwa mambo mengine.

Mhe. Rais kwa kiasi kikubwa alibadilika, sisemi alichukua ushauri wangu kwani ninauhakika hawezi kupata nafasi ya kusoma hapa, ila naamini wapo watu wanaomshauri kile nilichoandika bila kujali waliupata wapi ushauri huo.

Ni jukumu letu kuhakikisha tunapendana, tunajaliana, tunaheshimiana. tunalindana bila kujali tofauti zetu.

Hii pia ipo kwa watu kama Kina Gwajima, ambaye pia mdomo wake hajautawala, alishawahi kumtukana Kadinali Pengo, alishawahi kuhitilafiana na Waislamu, huwezi watolea watu maneno machafu alafu bado wakubali uwaongoze, wewe ndio utajifanya umesahau lakini wenzako wanakuangalia tuu ni vile wamekosa nafasi ila wakipata nafasi watakujibu kwa vitendo.

Kabla sijamaliza ninukuu Katika Biblia, kwenye kitabu cha Yakobo

YAKOBO 3:
5 Ulimi nao ni kiungo kidogo sana lakini hujivunia mambo makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa! 6 Ulimi pia ni kama moto. Ulimi ni ulimwengu wa uovu kati ya viungo vyetu. Humchafua mtu nafsi nzima na kuwasha moto maisha yake yote, nao ulimi huwashwa moto wa kuzimu. 7 Wanyama wa kila aina, ndege, nyoka na viumbe vya baharini wanafugwa na wamekwisha kufugwa na binadamu. 8 Lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu unaohangaika huku na kule, uliojaa sumu inayoua.

9 Kwa kutumia ulimi tunamsifu Bwana na Baba yetu na kwa ulimi huo huo tunawalaani watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu. 10 Katika kinywa hicho hicho hutoka sifa na laana. Ndugu zangu, haipaswi kuwa hivyo. 11 Je, chemchemi yaweza kutoa kutoka katika tundu moja maji matamu na maji machungu? 12 Je, ndugu zangu, mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu waweza kuzaa tini? Pia haiwezekani chemchemi ya chumvi kutoa maji matamu.

Uongozi sio sehemu ya kuonyesha majivuno, kutukana watu, jeuri, matusi, ubabe, ushenzi, kutenga watu, kupiga watu na mambo mengine yasiyofaa.

Uongozi ni kuipenda jamii yako, kupigania watu wako, maliasili zako, kuleta umoja baina ya watu, kujinyenyekeza kwa watu, kukemea uovu na uhalifu, kuwasemea wanyonge, kuwa na maono miongoni mwa mambo mengine.

Ulimi ndio huongoza dunia iwe kwa njia njema au njia mbaya

Ulimi umeponza wengi, Ulimi uliangusha wengi na kuwapoteza, lakini Ulimi uliokoa wengi, ukawanyanyua kutoka chini mpaka juu.

Watu wote twapaswa kuwa na kauli njema zenye manufaa, kauli zisizoumiza wengine. Hasa viongozi twapaswa kuzingatia hili.

Nimalize kwa kusema; kila dakika ni dakika ya kujirekebisha, dakika ya kujifunza na kuwa mtu bora.

Wasalamu!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
I
NI KWELI MKUU ULIMI NDIO UNAOPIMA ALICHONACHO MTU NAFSINI MWAKE THAT WHY BIBLE INASEMA KIMWINGIACHO MTU HAKIMTII MTU UNAJISI BALI KIMTOKACHO NDICHO KIMTIACHO UNAJISI KWA MAANA HIYO HATA WATU WAKUSEME VIPI KAMWE MANENO YAO HAYAWEZI KUKUTIA UNAJISI ILA UNAJISI HULETWA NA MANENO YAMTOKAYO MTU TOKA MOYONI MWAKE NA KIUNGO KITUMIKACHO NI ULIMI,MFANO GWAJIMA HATA WATU WANGEMSEMA VIP WASINGEWEZA KUMTIA UNAJISI TATIZO NI MANENO YAKE NDIYO YAMEMCHAFUA (UNAJISI)
 
Nimegundua kushindwa kwa Makonda UK mkono wa ACT. Hivyo tu. Kilicho lengwa na kupimwa hapo ni umadhubuti wa JPM na maamuzi yake
 
Hawa acha wapambane na albadili zao wanavuna walichopanda. Ukipanda miba uvune vipi mahindi
 
KILICHOMPONZA MAKONDA NDICHO KINGEMPONZA MAGUFULI.

Na, Robert Heriel

Licha ya kuwa watu hawa kwa sehemu kubwa nawakubali na kuwapigia chapuo, lakini kamwe sitoacha kusema ukweli kuwa kinachowaponza ni kitu kimoja, ambacho kinafanya wasikubalike kwa wengi.

Makonda ni kijana mchapakazi, mbunifu, mthubutu na mwenye ujasiri wa kipekee. Hivyo hivyo kwa Mhe. Rais, John Pombe Magufuli.

Hakuna asiyetambua kazi za Makonda, hakuna asiyetambua harakati zake, kila mtu anamkubali kwa kazi zake, halikadhalika na Magufuli, hakuna asiyemkubali kwa kazi azifanyazo lakini nini kingemponza?

Kilichomponza Makonda ndicho hicho hicho ambacho kingemponza Mhe. Rais kama angetokea mtu akachukua fomu ndani ya chama. Nilikuwa nawaambia rafiki zangu kuwa endapo angetokea mtu akachukua fomu ya kugombea Urais akachuana na Magufuli basi ni wazi kabisa Magufuli angeshindwa mapema sana.

Nini kingemponza Magufuli ambacho kimemmaliza Makonda katika siku ya jana. Huo ndio mjadala wetu kwa siku ya leo.

Katika uongozi unaweza ukafanya kila kitu, ukaleta maendeleo, ukaongeza mishahara, ukafanya elimu kuwa bure, huduma za afya bure, yaani ukaifanya nchi kama Peponi lakini kama hutautawala ulimi wako basi huna ulilolifanya, hakuna atakayekupenda, hakuna atakayejali mambo uliyoyafanya.

Ulimi ni kiungo kidogo kinachoendesha dunia, huweza kuharibu, kubomoa lakini pia huweza kujenga na kuleta amani.

Hata nyumbani, Mume akiwa na pesa na anahudumia familia yake lakini kama hatakuwa na kauli nzuri ni wazi Mke wake na watoto hawatampenda. Lakini Mtu mwenye ulimi mzuri, yaani kauli njema hata kama hatekelezi majukumu yake bado mke wake atampenda na kumheshimu halikadhalika na watoto.

Kheri yule mwenye Ulime mwema na hapo hapo anauwezo wa kuhudumia familia yake. Huyo anabahati.

Kilichomponza Mhe. Makonda licha ya kuwa nilikuwa natamani apewe nafasi ya kuongoza ni ulimi wake. Makonda anashindwa kuelewa kuwa Maneno yanaishi, ulichosema leo kitaishi hata siku ujapokufa bado maneno yako yataishi. Ni vizuri watu kuchunga ndimi zao hasa viongozi wakubwa.

Ni busara kukaa kimya kuliko kuteleza katika ulimi, ni hatari sana. Watu hawasahau na hawatajua kuwa ulitania au uliteleza.

Makonda katika hili naamini atajirekebisha, na itakuwa amejifunza kuwa uongozi hautoshi pekeake bali kuishi na watu kwa upendo, hasa kwenye mdomo.

Kwa upande wa Mhe. Rais Magufuli, asije akadhani watu wanasahau maneno yake, ukisema umesema, na watu kamwe hawasahau maneno makali yaliyowaumiza. Magufuli anaweza kuwa amejenga barabara, kanunua ndege, kafanya kila kitu lakini maneno tuu yakamponza.

Naamini Mhe. Rais ni kiongozi mzuri ambaye kama binadamu wengine hupokea maonyo, na kubadilika. Katika hili ninaushahidi kuhusu mabadiliko ya kitabia ya Mhe. Rais pale anapokosolewa, maana mimi pia niliwahi kumkosoa kipindi cha nyuma akiwa ndio anachukua nchi kuhusiana na kauli zake, nilishawahi kuongelea habari za Tetemeko la Kagera, kuwakashfu viongozi wenzake kwa maneno makali kama kuwaita wapumbavu mbele za halaiki, kuwaambia wafanyakazi waache kazi kama mshahara wanauona ni mdogo, miongoni mwa mambo mengine.

Mhe. Rais kwa kiasi kikubwa alibadilika, sisemi alichukua ushauri wangu kwani ninauhakika hawezi kupata nafasi ya kusoma hapa, ila naamini wapo watu wanaomshauri kile nilichoandika bila kujali waliupata wapi ushauri huo.

Ni jukumu letu kuhakikisha tunapendana, tunajaliana, tunaheshimiana. tunalindana bila kujali tofauti zetu.

Hii pia ipo kwa watu kama Kina Gwajima, ambaye pia mdomo wake hajautawala, alishawahi kumtukana Kadinali Pengo, alishawahi kuhitilafiana na Waislamu, huwezi watolea watu maneno machafu alafu bado wakubali uwaongoze, wewe ndio utajifanya umesahau lakini wenzako wanakuangalia tuu ni vile wamekosa nafasi ila wakipata nafasi watakujibu kwa vitendo.

Kabla sijamaliza ninukuu Katika Biblia, kwenye kitabu cha Yakobo

YAKOBO 3:
5 Ulimi nao ni kiungo kidogo sana lakini hujivunia mambo makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa! 6 Ulimi pia ni kama moto. Ulimi ni ulimwengu wa uovu kati ya viungo vyetu. Humchafua mtu nafsi nzima na kuwasha moto maisha yake yote, nao ulimi huwashwa moto wa kuzimu. 7 Wanyama wa kila aina, ndege, nyoka na viumbe vya baharini wanafugwa na wamekwisha kufugwa na binadamu. 8 Lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu unaohangaika huku na kule, uliojaa sumu inayoua.

9 Kwa kutumia ulimi tunamsifu Bwana na Baba yetu na kwa ulimi huo huo tunawalaani watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu. 10 Katika kinywa hicho hicho hutoka sifa na laana. Ndugu zangu, haipaswi kuwa hivyo. 11 Je, chemchemi yaweza kutoa kutoka katika tundu moja maji matamu na maji machungu? 12 Je, ndugu zangu, mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu waweza kuzaa tini? Pia haiwezekani chemchemi ya chumvi kutoa maji matamu.

Uongozi sio sehemu ya kuonyesha majivuno, kutukana watu, jeuri, matusi, ubabe, ushenzi, kutenga watu, kupiga watu na mambo mengine yasiyofaa.

Uongozi ni kuipenda jamii yako, kupigania watu wako, maliasili zako, kuleta umoja baina ya watu, kujinyenyekeza kwa watu, kukemea uovu na uhalifu, kuwasemea wanyonge, kuwa na maono miongoni mwa mambo mengine.

Ulimi ndio huongoza dunia iwe kwa njia njema au njia mbaya

Ulimi umeponza wengi, Ulimi uliangusha wengi na kuwapoteza, lakini Ulimi uliokoa wengi, ukawanyanyua kutoka chini mpaka juu.

Watu wote twapaswa kuwa na kauli njema zenye manufaa, kauli zisizoumiza wengine. Hasa viongozi twapaswa kuzingatia hili.

Nimalize kwa kusema; kila dakika ni dakika ya kujirekebisha, dakika ya kujifunza na kuwa mtu bora.

Wasalamu!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Na kinaweza kumkuta mama misambano
 
Back
Top Bottom